Nahitaji kubadili jina naomba kujuzwa utaratibu wake

mahingah

Senior Member
Oct 4, 2016
199
275
Mimi ni kijana nimemaliza chuo mwaka huu ngazi ya Degree, katika makuzi yangu ya kimasomo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba nimekulia kwa bibi yangu mzaa mama huko kijijini, wakati naandikishwa darasa la kwa bibi aliniandikisha la ukoo na la utotoni la upande wa mama.

Nilikuwa nakuja Dar mara moja kwa mwaka wakati wa likizo hata wazazi hawakulijua hili hata mimi niliona kawaida, nikamaliza hadi form four vizuri na kupangiwa shule ya A level Iringa, nilivyo maliza form six ndio nikatambua hili kuwa jina langu ni tofauti kabisa na alilo niandikisha bibi mzaa mama.

Wakati naanza kuomba chuo mwaka 2016 pamoja na mkopo nilitakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa, nikamfuata bibi akaniambia yeye cheti changu hana niwafuate wazazi wangu, nilivyompigia baba simu akasema kipo, nikaja Dar kuja kukichukua ili niambatanishe, nikakuta vitu viwili tofauti na jina langu, hata nilipoenda kanisani nikakuta cheti cha ubatizo kinalingana na cheti cha kuzaliwa lakini vyeti vya elimu vyote majina tofauti, kwa sababu nilikuwa na haraka ya chuo mzee akabidi aongee na RITA kuambia huyu kijana hana cheti na tukatoa kidogo nikapata cheti kipya chenye jina kama la vyeti,

Sasa nina vyeti viwili vya kuzaliwa, shida yangu nataka kutumia jina langu la kubatizwa, je ninaweza kubadili majina ya vyeti vyangu vyote vya elimu kwa ngazi niliofikia ya kielimu?

Naomba msaada kwa anayejua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna haja ya kuhangaika sana. Wananchi wenyewe watakubadilishia kutokana na hali yako. Assume unaitwa Mohammed. Kama utafanikiwa kua na pesa utabadilishiwa na kuitwa MO. kama utakua brazamen watakuita uncle Muddy. Kama utakua hina pesa utaitwa mwamedi. Vile vile kamanunaitwa Athumani ukawa huna pesa utaitwa asumani ukiwa nazo bro Othman.
 
😁😁😁
 
Back
Top Bottom