Nahitaji kuanzisha biashara ya vipodozi au vifaa vya pikipiki ila sina uzoefu navyo

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
424
1,044
NAOMBENI USHAURI

Nimekuwa katika mawazo na wakati mgumu sana, najaribu biashara ambayo iko salama nakoswa majibu na najikuta nakuwa mpole tu.

1. Nilipanga nifungue Duka la vipodozi kwa sababu biashara hii ya vipodozi inaenda sana na ukiangalia kina mama wengi na wadada wengi hutumia vipodozi hivyo naona ingenifaa.

Changamoto yake ni ipi?
Changamoto ambayo nakuwa siijui nikuwa biashara hii inachangamoto gani nikiifanya ili niwe na tahadhari zaidi. Kwa mwenye uzoefu wa hii biashara anisaidie mawazo zaidi pamoja na changamoto zake.

2. Ni biashara ya spea za pikipiki na hii naambiwa ni nzuri ila changamoto yake nayo sijui ni ipi! Na kwa mwenye uzoefu wa hii biashara anisaidie mawazo zaidi pamoja na changamoto zake.

Mtaji wangu ni Million 4+
Maeneo nayo taka kufanya biashara hiyo ni KATORO - GEITA

Natanguliza shukrani kwenu
 
Back
Top Bottom