Nahitaji kuanza kilimo cha zao la beetroots maeneo ya Dodoma, Morogoro, Singida au Shinyanga

Msipende kuilaumu serikali kila kitu, kila kanda kuna kituo cha utafiti, siamini kama wadau hawa wanaoshinda jf wanashindwa kutembelea vituo hivyo na kupata elimu bure
Hapo tunaongelea kuhusu bidhaa zetu kuuzwa kwa jina la nchi nyingine

Tunataka bidhaa zetu zionekane kwenye soko la kimataifa
Na hivyo vituo wanatoa huduma zipi za export au
Tutafurahi kuona wakihamasisha watu na kulegeza kila kitu
 
N
No namaanisha beetroots zenyewe, nilishaziona zimetandazwa barabarani kariakoo, bei veeeeeery cheap, pitia pale upate elimu na uzoefu wa wakulima toka lushoto
Ooh
Hapo mdau alikuwa anataka mbegu
Lakini sipo huko ila nilikuwa natoa mawazo tu
 
Msipende kuilaumu serikali kila kitu, kila kanda kuna kituo cha utafiti, siamini kama wadau hawa wanaoshinda jf wanashindwa kutembelea vituo hivyo na kupata elimu bure
mkuu sidhani kama shida ni ukosefu wa taarifa/elimu juu ya kilimo kwa wakulima!

usemavyo ni sahihi kua tuna vituo vingi vya ARI ambavyo vinatoa elimu aither kwa kufuatwa au kufuata wakulima kulingana na hali ya kilimo na mwenendo wa mazao nchini.

Kuna haja ya serikali kupitia ofisi hizi za kilimo kila halmashauri na hizi za ARI kuwa na msukumo wa nyenzo za kusaidia wananchi.

kwa mfano zao kama hili linaonekana ni geni lakini lipo maeneo baadhi nchini linafanya vizuri na linaonekana kua na soko, kwa hiyo ni wakati mwafaka wa serikali kulifanyia kazi maana sio kila mwananchi anaetamani kulima anauelewa na anaweza kumudu gharama za inputs pamoja na soil analysis ili kujua kama zao eneo lake litastahimili au lah!
 
Nashukuru kwa mrejesho, ni vzr sisi wadau tutumie mifumo rasmi iliyowekwa na serikali, kiukweli wataalamu wetu hawatumiwi ipasavyo na walengwa

Hakuwa na maana hiyo
Kosa hapo hakuweka alama ya kuuliza
Ungefuatia mjadala kwanza
Tupo kuelimishana hapa
Shukran
Nadhani wewe ndio ungefuatilia mjadala kwanza.
Alieandika sio yeye na kama hakuweka alama ya kuuliza basi hiyo sentensi ilileta maana tofauti. Jifunze kusoma kwanza
 
Nashukuru kwa mrejesho, ni vzr sisi wadau tutumie mifumo rasmi iliyowekwa na serikali, kiukweli wataalamu wetu hawatumiwi ipasavyo na walengwa
Watumie vipi mkuu hebu toa ufafanuzi, tuwafuate maofisini?

Maafisa kilimo na maafisa biashara wanapaswa kwenda mashambani na masokoni kuwashauri wakulima na kuwafungulia njia na network za masoko hasa ya nje ya nchi, ndio kazi yao.

Swali
Umeshawahi kumuona afisa kilimo/biashara akitoa elimu kwenye field/eneo lako? Kama jibu ni NDIO upo mkoa/wilaya gani, kama ni HAPANA kazi yao hasa ni nini?

Unaposema tusiilaumu serikali kwa kutotengeneza mazingira rafiki ya biashara je tunapaswa kuipongeza kwa kufunga mipaka na kutia umasikini wakulima na wafanyabiashara?

Nakumatt supermarket zinapofungwa nchi nzima ni watu wangapi wanakosa ajira, sababu ni nini? hivi umeshakwenda nchi nyingine ukaona ilivyo easy kufanya biashara including kilimo..hapa kwetu ni disaster.

Sio kila jambo linahitaji ushabiki mkuu!, tuseme kweli kuisaidia serikali na nchi yetu.
 
M
Mbegu Zipo kopo sh. Elfu 4 ila kuota Ni ngumu sana
Mkuu kama ni beetroots mbona zinaota bila shida
Nilishawahi kulima Dodoma zinaota vizuri na zinatoka kubwa kwa sababu ya nature ya udongo (sio mfinyanzi)

Soko lake kubwa kwa tz ni
-Kisutu, wahindi wanazipenda sana
-Supermarket zote
-Wajawazito, wagonjwa na watoto - kwaajili ya kuongeza damu.
Wabongo wengi hawazijui mpaka waandikiwe na daktari ndio wanazitafuta.

Bei ya Dodoma 1kg-6000tsh (sio constant)

Note;
Watu wengi wanapenda zaidi beetroots za Arusha kwasababu Dodoma maji ni ya chumvi hivyo zinakuwa na ladha ya chumvi chumvi tofauti na za Arusha zinakuwa tamu, lakini bado hata za dom zina soko.
 
Kwa kuwa kubwa kwa Dodoma Ni kweli Zina kuwa kubwa mno ila sijui mbegu nilizo NUNUA hazikuwa nzuri hazikuota ilibidi ninunue beets sokoni nioteshe maganda YAKE ndo vikazaliwa vile viazi shida yangu haikuwa viazi ilikuwa Ni majani Kama mboga
 
Watumie vipi mkuu hebu toa ufafanuzi, tuwafuate maofisini?

Maafisa kilimo na maafisa biashara wanapaswa kwenda mashambani na masokoni kuwashauri wakulima na kuwafungulia njia na network za masoko hasa ya nje ya nchi, ndio kazi yao.

Swali
Umeshawahi kumuona afisa kilimo/biashara akitoa elimu kwenye field/eneo lako? Kama jibu ni NDIO upo mkoa/wilaya gani, kama ni HAPANA kazi yao hasa ni nini?

Unaposema tusiilaumu serikali kwa kutotengeneza mazingira rafiki ya biashara je tunapaswa kuipongeza kwa kufunga mipaka na kutia umasikini wakulima na wafanyabiashara?

Nakumatt supermarket zinapofungwa nchi nzima ni watu wangapi wanakosa ajira, sababu ni nini? hivi umeshakwenda nchi nyingine ukaona ilivyo easy kufanya biashara including kilimo..hapa kwetu ni disaster.

Sio kila jambo linahitaji ushabiki mkuu!, tuseme kweli kuisaidia serikali na nchi yetu.
Mkuu mimi naishi lindi vijijini na kuna bwana shamba kila kata,
 
Swala sio uwepo wao, ishu ni uwajibikaji wao.Nafahamu wapo kila mahali
mimi ni mtafiti, nimetembea mikoa zaidi ya mikoa 27 bara na Z'bar, hawa watu hawatekelezi wajibu wao ipasavyo na ndio sababu kuu ya wakulima kupata hasara na biashara kufilisika kila uchwao.
 
Back
Top Bottom