Bima ya Afya Tanzania: Kampuni bora na zenye changamoto katika kuhudumia wateja wake

Hili suala ni nyeti na muhimu sana. Ingalikuwa vema watu wakaweka siasa kando na kulisemea kwa pamoja. Yawezekana kuna sehemu waliopewa dhamana hawajaliona na wapo kwenye masuala mengine. Juzi wale CHIF wamepandisha bei ya Bima yao. Hawa walikuwa kimbilio la watu wengi wasiokuwa na uwezo, lakini hata ukiwa na Bima yao Dawa hupati.

Kwa kawaida vijiweni tunaposhinda kama mmoja wetu akipatwa na maradhi huwa tunamchangia hela za dawa lakini tulishawishika kutumia CHIF kuwaokoa wenzetu wasio na uwezo. Sasa hawa CHIF nasikia nao wamepunguza package na dawa hazipatikani kwa kutumia kadi zao. Kwa hili tuweke siasa pembeni watu wanaumia na wengine hufa kwa kukosa huduma nzuri za matibabu.
 
Hili suala ni nyeti na muhimu sana. Ingalikuwa vema watu wakaweka siasa kando na kulisemea kwa pamoja. Yawezekana kuna sehemu waliopewa dhamana hawajaliona na wapo kwenye masuala mengine. Juzi wale CHIF wamepandisha bei ya Bima yao. Hawa walikuwa kimbilio la watu wengi wasiokuwa na uwezo, lakini hata ukiwa na Bima yao Dawa hupati.
Kwa kawaida vijiweni tunaposhinda kama mmoja wetu akipatwa na maradhi huwa tunamchangia hela za dawa lakini tulishawishika kutumia CHIF kuwaokoa wenzetu wasio na uwezo. Sasa hawa CHIF nasikia nao wamepunguza package na dawa hazipatikani kwa kutumia kadi zao. Kwa hili tuweke siasa pembeni watu wanaumia na wengine hufa kwa kukosa hudumanzuri za matibabu.
Mkuu bima zipo kibao na nzuri sio lazima hao NHIF kuna moja nilishawahi itumia inaitwa Resolution Insurance, hio bima ni nzuri sana ingawa nilipewa wakati nafanya kazi sehemu fulani
 
Mkuu bima zipo kibao na nzuri sio lazimia hao NHIF kuna moja nilishawahi itumia inaitwa Resolution Insurance, hio bima ni nzuri sana ingawa nilipewa wakati nafanya kazi sehemu fulani
Tuwekee packages zao na gharama kwa mwaka
 
Mkuu bima zipo kibao na nzuri sio lazimia hao NHIF kuna moja nilishawahi itumia inaitwa Resolution Insurance, hio bima ni nzuri sana ingawa nilipewa wakati nafanya kazi sehemu fulani
Ni kweli, hizo Bima zipo nyingi ila mimi naongelea zitumiwazo na wafanyakazi wa umma na zile zetu za sisi wa hali ya chini CHIF. Hizo nyengine waajiri makini huwakatia Bima wafanyakazi wao.
 
Ni kweli, hizo Bima zipo nyingi ila mimi naongelea zitumiwazo na wafanyakazi wa umma na zile zetu za sisi wa hali ya chini CHIF. Hizo nyengine waajiri makini huwakatia Bima wafanyakazi wao.
Mkuu hio CHIF ni sawa na NHIF? Hio ya Resolution unaweza kwwnda kukata ya binafsi
 
Strategis ndio the best. Au kama vipi nenda Lumumba ofisi ndogo ya CCM kuna bima ya makada kama wewe.
 
Mkuu hio CHIF ni sawa na NHIF? Hio ya Resolution unaweza kwwnda kukata ya binafsi
Samahani, ni CHF badala ya CHIF, CHF ni Community Health Fund, mwanzo gharama zao ilikuwa ni shiligi 10,000, lakini kuanzia mwaka huu wamepandisha ni shilingi 30,000. Wenyewe wanadai imeboreshwa lakini dawa na vipimo havipatikani.
 
Unapata nini sasa kama hizo huduma za kwanza hupati
 
Bima hizi hazitaki kulipia vipimo, hawataki kulipia dawa, nini maana ya bima?

Wanakuchagulia ugonjwa wa kuugua.
Unaambiwa mwaka wa kwanza huduma ziko limited lakini hata baada ya kumaliza mwaka ukienda hospitali, utasikia x-ray, MRI au CT-San hawalipi, utaambiwa parasol watalipa lakini ciprofloxacin hawalipi, sasa unajiuliza kwanini una bima ya afya.

Unalipia premium kila mwezi no question lakini ukifika muda wa wewe kupata service zinakuwa limited.

Nadhani kuna haja insurance kueleza huduma wayakazolipia kabla hawaja mlazimisha mtumishi kuwa na insurance, maana wengi wasio na choices mnazozitafuata hapa wanaumizwa sana.

Insurance inalipia Malaria tu, ukiumwa beyond malaria wanaanza, ohoo hivyo vipiko hatulipii, sasa huyo daktari atajuaje naunwa nini kama hamtaki nifanyiwe vipimo?!
Insurance kama waneona 1.5 inatosha wasiweke masharti, na kama haitoshi basi waseme ni kiasi gani kinatosha ili ukijibana ukalipia au ukakatwa kazini wakubali nawewe upate huduma unlimited kuliko ilivyo sasa.

Sasa watumishi ukatwe NIHF, isikusaidie halafu uingie gharama kulipia Jubilee, au AAR kwa pesa nyingine, rushwa itaishaje huku makazini.

Wote tungepata huduma sawa ingekuwa rahisi kuliko kuwekwa kwenye mafungu, sisi NIHF wao Jubilee au AAR na wote tuko ofisi moja.

Kama wabunge na mawaziri nao wangekuwa na hizi NIHF bila shaka huduma zingeboreshwa, tofauti na hapo tunaumia sisi.
 
Kawaida katika bima kuna waiting period kabla hujaingia katika bima elewa kwanza mpango upi utakufaa. Kampuni za bima zina avoid wagonjwa kata bima ukiwa Mzima
Hahahah Ujinga uko Tanzania tu, na uzuri ni kwamba ujinga ni nywele na kilamtu ana zake. Bima inayolipia malaria pekee hahaha mtaisoma number kweli.
 
Habarini wakuu!!

Heri??? Mvua vipi mahala leo ulipo‍♀️

Twende kwenye mada.

Nahitaji bima ya afya binafsi, ya mtu mmoja ni shirika gani la bima linahuduma nzuri na za uhakika, bei zake, process za kukamilisha zoezi na muda hadi wa kuwa mwanachama, kupata huduma

Kwa mwenye kujua msaada tafadhari bila kusahau na mawasiliano yao Au sehem wanayopatika
 
Chukua NHIF ...

Maelezo na kila kitu ulichouliza yako humu
IMG_20200108_202832.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukua NHIF ...

Maelezo na kila kitu ulichouliza yako humu View attachment 1324633

Sent using Jamii Forums mobile app

Asante

Nimeona huo mchanganuo

Nataka kujua sio wasumbufu kwenye huduma zao? Nilivyokua chuo nililipiaga mara moja 50,400 ila sikuwahi kutibiwa nayo (sikuumwa kwa huo muda hadi kadi ikaexpire)

Pia kadi zilikua zinachelewa kutoka unalipa na kufanya maombi leo, utapata mwezi wa nne

Ni kwa wanafunzi tu? Chuo walikua wazito kufatilia? Au ndivyo walivyo? Ukifanya malipo baada ya muda gani unaweza kupata Kadi kwaajili ya huduma?
 
Asante

Nimeona huo mchanganuo

Nataka kujua sio wasumbufu kwenye huduma zao? Nilivyokua chuo nililipiaga mara moja 50,400 ila sikuwahi kutibiwaga nayo (sikuumwa kwa huo muda hadi kadi ikaexpire)

Pia kadi zilikua zinachelewa kutoka unalipa na kufanya maombi leo, utapata mwezi wa nne

Ni kwa wanafunzi tu? Chuo walikua wazito kufatilia? Au ndivyo walivyo? Ukifanya malipo baada ya muda gani unaweza kupata Kadi kwaajili ya huduma?
Pisi Kali mimi ni mwanachama wa NHIF ni moja ya bima za afya Bora kabisa ina coverage ya hospitali nyingi nchi nzima tofauti na Bima zingine ....

Hilo suala la kupewa kadi after 3 months siwezijua maana mimi nilichukua kadi miaka hiyo chini ya shirika flani hivi hatukutumia muda huo, ila sijui kwa sasa..

Ila niseme tu Licha ya changamoto zingine ndogondogo NHIF ni bima Bora kwasasa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom