Nahitaji anayefuga NDEGE huyu au mayai yake

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Naomba nimuelezee ndege huyu Kwanza kwa ufupi, kuna aina nyingi za ndege aitwaye TAI, mfano kuna tai mwenye mkia mweupe, kuna tai wa rangi ya dhahabu, kuna tai wa Ufilipino na kadhalika.

Inakadiriwa kufikia aina sitini za tai duniani wengi wao wanapatikana Afrika, Asia na Ulaya.

Tai ni ndege kama walivyo ndege wengine, ingawaje wao wana sifa za pekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, kupaa na uwezo wao mkubwa wa kuona mbali. Kwa sababu kuna aina mbalimbali, hata maumbile yao yanatofautiana. Aina ya tai mwenye uzito mkubwa kabisa ni aina ya “Steller’s sea Eagle” ana uzito unaofikia kilogramu 6.7.

Tai mwenye mabawa marefu kuliko wote ni aina ya “White Tailed Eagle” mabawa yake yana jumla ya urefu wa sentimita 218.5, sawa na mita 2.185. Tai aina ya “Phillipine Eagle” ndio wanaoongoza kwa urefu, wao wanafikia sentimita 100.

Sasa kama unajua namna ya kuwapata au kupata mayai yao tafadhali tujulishane asante.
 
#tai
tai.jpeg
 
Back
Top Bottom