Nahisi tumekwama kabisa:... tunawezaje kujinasua?

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Nimekuwa nikifuatilia suala la matumizi ya lugha katika maeneo yetu na sasa naona kuwa tumekwama kabisa. Iwe ni Kiswahili, hatukizungumzi inavyotakiwa.

Na wale wanaojidai walienda shule hao ndo balaa. Wakiongea Kiswahili hakuna kitu na Kiingereza ndo mchemsho.

Juzi juzi nilikuwa na rafiki yangu toka Kenya, tukakutana na washikaji wengine na kulazimika kutumia Kiigereza. Baada yapo, huyo jamaa toka Kenya akawa ananiuliza kwamba inakuwaje watu wanashindwa vitu ambavyo huko kwao vinamalizika katika ngazi ya shule ya msingi. Hili hasa lilihusu tenses. Unakuta mtu anaseme kwa mfano, "last week we go to Dar, then meet our friends. We do different types of sports such as beach football and volley ball. The we go to dance music at Billicanas. That DJ is good, he play great tracks and we all enjoying his music because we go back home almost in the morning"!

Hivi tunajua kuwa tuna matatizo? Na je tunachukua hatua gani kuyasahihisha?

Nasikitika sana ninapokutana na washikaji wa namna hii kwani naamini bado tunaweza kujisomea na kusahihisha makosa ya lugha tunazotumia!
 
Wabongo Bwana we just have a congenital paranoia disease! So much delutions! We want speak perfect english, perfect swahili, drive big cars!!!!!! perfect english for what? Its not my mother tounge, I am a sukuma for Christ's sake! Nimekutana na Maprof wasio wasio jua English wanaongea broken English kipindi kizima and its just fine with them! And this is what makes us look like fools in front of people, coz the moment you start talking the only thing you think is perfect english, perfect english!! watanicheka nikikosea!!!! Ongea english kama unavyoongea kiswahili!! be free usijali error it is NOT ur mother tounge! Ukikwama waulize waliojirani yako!!!!!!!!!
Wakenya mbona wanaongeaga Broken swahili na wako poa tu haaaaaaaaaaa!@#$$$%%%^^^&&$@@
 
Mkuu naomba kutofautiana na wewe. Hakuna anayesema kwamba mtu aongee Kiingereza kama Kisukuma, Kinyakyusa au Kihaya (ingawa hata hizo lugha zimeshaharibika). Ila hakuna sababu ya kutetea makosa ambayo yanaweza kurekebishwa kirahisi. Mfano hili la mtu kuchanganya tenses za Kiingereza. Nimekutana na watu wengi wanaotumia Kiingereza kama lugha ya pili au ya tatu ila sisi tumezidi kwa kuchukulia vitu kirahisi rahisi na kufanya makosa ya hovyo hovyo. Na ukizingatia kuwa Kiingereza ni lugha ya kufundishia kuanzia shule za sekondari hadi chuo kikuu. Huweza kabisa kujenga hoja ya kutetea huo uzembe!
 
DC unauwa....hivi watanzania tunaweza nini kwa ufanisi zaidi ya wizi, uzembe, na mizaha?
 
Hata hicho kikristu wakenya wanatamba na slang tu, nenda kwenya kuandika uone maduduz, but in reality TZ always tunakua over proud we want to do thing to 101% perfection and at the end of day inakula kwetu tunakua atuja master kitu chochote, kuna msela namjua yeye "pseudocode" analitamka hivyo hivyo na wazungu wanamsikiliza na kumuelewa na on professional side ni kichwa
 
DC unauwa....hivi watanzania tunaweza nini kwa ufanisi zaidi ya wizi, uzembe, na mizaha?

Pia na kulalamika kwamba tunaonewa wakati sisi wenyewe ndo tunaachia nafasi. Kama waajiri wanataka watu wanaoongea kizungu vizuri, kwa nini tusiingie msituni tukajifunza ili tuwanase?
 
Back
Top Bottom