Nahisi nina bahati

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,437
1,597
Salam nyingi ziwafikie hapo mlipo, mara baada ya salam hofu na mashaka ni kwenu mlio mbali na upeo wa macho yangu.
Leo majira ya saa tatu na nusu usiku nikiwa natokea tegeta kwenda makonde (Dar) nikiwa kwenye daladala nimetokewa na jambo ambalo ninalichukuli kama bahati na kwa kweli nina mshukuru Mungu. Huko nyuma maeneo ya kuanzia suma jkt mpaka africana tulikuwa tunambea kwa kasi kidogo hasa ukizingatia mida hiyo magari huwa ni machache barabarani. Mbele kidogo tukawa kwenye mwendo mdogo sana kuruhusu magari mengine yapite. Mara tairi ya mbele upande wa kulia ikapiga mzinga (ikapasuka). Dereva akapaki gari pembeni tukashuka. Ninajihisi mwenye bahati ninapofikiria ile tairi ingepasuka mapema zaidi ingekuwaje.
Nahisi nia bahati.
 
Israel alikuwa bado hajaamua kuchukua kiumbe chake, akiamua hata pancha ya baiskeli unamuondoa mtu!.
 
tairi tu ndio ujione una bahati kama mtende?
acha woga mtoto wa kiume, mm nshawahi kupata ajali ya basi watu walikufa
nikapona wengine walipoteza viungo vya miili yao, kupasuka tairi ni kitu cha kawaida hasa hizi daladala wanaweka tairi vimeo.
nahisi ww ukija kuendesha gari utakuwa unatembelea spidi ya km 40 kwa saa,
hii sii habari mkuu we bora ungetoa mada ya daladala zetu na usalama wake kwa abiria ukatolea mfano wako wa tairi kupasuka,
 
Pole sana, nimiongoni mwa mambo ya barabarani. Ni vizuri kumshukuru mungu kwa lila jambo analotutendea maishani mwetu.
 
tairi tu ndio ujione una bahati kama mtende?
acha woga mtoto wa kiume, mm nshawahi kupata ajali ya basi watu walikufa
nikapona wengine walipoteza viungo vya miili yao, kupasuka tairi ni kitu cha kawaida hasa hizi daladala wanaweka tairi vimeo.
nahisi ww ukija kuendesha gari utakuwa unatembelea spidi ya km 40 kwa saa,
hii sii habari mkuu we bora ungetoa mada ya daladala zetu na usalama wake kwa abiria ukatolea mfano wako wa tairi kupasuka,

Ushauri wako sio mbaya mkuu.
 
uko sawa kabisa kusema unabahati ila mshukuru sana Mungu, mana neno linasema shukuruni kwa kila jambo. Na kama umeweza kushukuru kwa kidogo basi ni vema, ubarikiwe sana
 
Chukulia tu poa..wengine tairi inapasuka wakiwa kwenye spid 180 wanapona lakini hawaji kuleta huo upuuzi hapa JF

Umeamka na hasira naona Rejao, au mambo ya Igunga nini? Siamini asubuhi yote hii naitwa mpuuzi!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom