Nahisi nilimegewa

kuna nini cha ajabu hapo? jamaa alishammega sana before na akazaa naye....halafu ulivyo boya ulimruhusu vipi aende kumegwa halafu unamuuliza kuhusu kumegwa wakati umeshaona manyoya...duh uzi una miaka tisa!...
 
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msichana mmoja mrembo sana. Hakuwa mrembo tu bali pia alikuwa na akili zilizoendana na urembo wake. Nilimpenda sana kwani niliona hatimaye nimempata anayeendana na mimi.

Wakati tunakutana nilimkuta akiwa tayari ana mtoto mmoja. Mtoto huyo alikuwa na umri wa miezi tisa. Baba wa mtoto huyo aliachana na huyo msichana wakati akiwa bado mjamzito wa miezi mitano na hata alipozaliwa jamaa hakuwepo na hakuja kumwona mwanae hadi alipofikisha umri wa miaka miwili.

Ndani ya miaka miwili ya uhusiano wetu jamaa akaanza kumshinikiza demu wangu ampeleke mtoto Toronto ili akamwone baba yake. Demu wangu akawa kwenye mazingira magumu kwa sababu tokea amzae huyo mwanae, baba yake alikuwa hajamwona na alikuwa anataka sana mwanae amjue baba yake. Wakati huo huo uhusiano wetu ulikuwa umekolea na mimi fikara za kumvalisha pete zikawa zimeanza kutawala kichwani mwangu.

Kwa takribani mwezi mzima akawa anafikiria ni jinsi gani ataweza kwenda kumpeleka mtoto Toronto bila kuharibu uhusiano wetu. Kumpandisha mtoto ndege na kuwakabidhi watu wa ndege halikuwa wazo zuri kwa sababu mtoto alikuwa bado mdogo sana. Mwishoni kukawa hakuna jinsi zaidi ya yeye mama mtu kumpeleka mtoto kwenda kumwona baba yake.

Siku ya siku ikafika. Mama na mtoto wakapanda ndege kwenda Toronto kumwona baba wa mtoto. Nikaachwa nyuma peke yangu. Toronto walifikia kwa huyo jamaa. Na jamaa alikuwa akiishi kwenye condo ya vyumba viwili. Ufikiaji wao hapo haukunipendeza licha ya demu wangu kuniahidi kuwa atakuwa analala sebuleni huku jamaa akilala chumbani kwake na chumba kile kingine cha pili atalala mtoto.

Walikaa huko kwa wiki mbili. Kila siku akiwa huko alijitahidi kunipigia simu angalau mara moja kuongea na mimi. Ilikuwa wakati mgumu sana kwangu mimi kwani sikumwamini hata kiduchu eti kuwa atakuwa analala sebuleni. Nikamwambia amwambie hivyo mtoto wa chekechea na si mimi kwani ingawa nilizaliwa usiku, sikuzaliwa jana usiku!!

Baada ya kurudi nilimwuliza kama alimegwa na yeye alikataa katakata. Mimi kwa upande wangu sikumwamini hata kidogo na nikamwacha.

Wadau, hivi kweli mnadhani alikuwa ananiambia kweli? Mtu kafikia kwa jamaa halafu kakaa wiki mbili, hivi kweli hawakumegana? Komredi Fidel hebu nipe mawaidha yako...unalionaje hili? Nilimegewa? Mimi nadhani nilimegewa ingawa sina ushahidi wa bunduki inayofuka moshi.
Hajafika kwa jamaa amefika kwa mumewe
 
*ni simple tu brooo
Ukitaka kujua kama ameliwa waza hivvi
*Mfano we ndio uwe yule jamaa wa toronto
*Mzazi mwenzio kaleta mtoto wenu uje umwone
Je utamkaza au utamwacha?
Jibu ukipata ndio hicho hicho kimetokea huko toronto Canada

Sichenji buku kwa njaa ya siku moja*
 
Pole mzee Ngabu, kuchapiwa siri ya ndani we ungekomaa uioshe tu uendelee na matumizi!
 
Mbna wakati anamzalisha hukuumia ila pind anampelekea mtt baba inakuuma,jitafakar upya kuna sehem umekosea n hayo tu.
 
Back
Top Bottom