tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,855
- 1,117
Habari zenu wadau!
Nimefanya maamuzi magumu ambayo nilidhani yatanisaidia, lakini yanaishia kuniumiza.
Ni kuhusu binti ambaye nimemfatilia kwa muda mrefu, nilijitahidi kwa kila hali kumuonesha kwa vitendo kwamba nampenda. Nilijitahidi kuwa karibu naye hasa kwa upande wa mawasiliano ya simu, muitikio wake ulikuwa mzuri japo alisema mapenzi na mimi no. Niliukubali urafiki japo kwa shingo upande, niliendelea kuwasiliana naye, lakin ilikuwa mpaka mimi nimtafute, nikikaa kimya naye anapotea, nikirudi anarudi.
Kama mnavyojua kuwa kamba ikivutwa sana hukatika pabovu, ilifika muda nikachoka na nikaamua kukaa kimya. Sasa ni wiki ya 3 toka nimchunie, naye yuko kimya.
Wadau hali hii inanitatiza, nataka nimpotezee mazima lakini naona naelekea kushindwa, moyo unaniuma kumuacha aende.
Naomba ushauri wenu.