Nahisi napenda nisipopendeka. Je, ni uamuzi sahihi nilioufanya?

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Habari zenu wadau!

Nimefanya maamuzi magumu ambayo nilidhani yatanisaidia, lakini yanaishia kuniumiza.

Ni kuhusu binti ambaye nimemfatilia kwa muda mrefu, nilijitahidi kwa kila hali kumuonesha kwa vitendo kwamba nampenda. Nilijitahidi kuwa karibu naye hasa kwa upande wa mawasiliano ya simu, muitikio wake ulikuwa mzuri japo alisema mapenzi na mimi no. Niliukubali urafiki japo kwa shingo upande, niliendelea kuwasiliana naye, lakin ilikuwa mpaka mimi nimtafute, nikikaa kimya naye anapotea, nikirudi anarudi.

Kama mnavyojua kuwa kamba ikivutwa sana hukatika pabovu, ilifika muda nikachoka na nikaamua kukaa kimya. Sasa ni wiki ya 3 toka nimchunie, naye yuko kimya.

Wadau hali hii inanitatiza, nataka nimpotezee mazima lakini naona naelekea kushindwa, moyo unaniuma kumuacha aende.

Naomba ushauri wenu.
 
Unakuumaje wakati hajawahi kukupenda hata kuonyesha kuwa anakupenda hajawahi
Achana nae bana wewe tafuta anayekupenda
 
akipata rejection ingine tutamsahau sasa hivi! hivi akiji-keep busy si anaweza kufanikiwa kimaisha zaidi? anaweza kwenda shule,kubadili kazi ama ku-concentrate kwenye biashara. kwani huyo dada ni oxygen?kha!
tafuta kiburudisho kwanza,akili ndo itakaasawa
<br />
<br />
 
akipata rejection ingine tutamsahau sasa hivi! hivi akiji-keep busy si anaweza kufanikiwa kimaisha zaidi? anaweza kwenda shule,kubadili kazi ama ku-concentrate kwenye biashara. kwani huyo dada ni oxygen?kha!
Umeongea mambo ya msingi, hapa nazidi kugundua kwamba mambo mengine ni kujiendekeza, mwanzo nilimfanya oxygen>kumbe nilikuwa najidanganya, hata siamin kama nimemaliza wik 3 pasipo kuwasiliana naye.
 
Never expect unexpected mkuu<br />
Hiyo ulijipa matumaini ila hapo ondoka si pako na kama umependa hapo umekosea njia tafuta pengine pa kupenda
Huyo hana mpango kabisa na wewe
ni ukweli mchungu ila nitajitahidi kuumeza.
 
ni ukweli mchungu ila nitajitahidi kuumeza.

Umependa pasipopendeka na wala hajali kama unaumia
Jiepushe kukutana nae mara kwa mara na kama ni no yake ya simu idelete na usiwasiliane nae
Pambana na kazi na jisahaulishe kama ushawahi kuwa na mtu kama huyo then jitulize utafute mtu wako
 
mkuu nashukuru kwa maneno yako yenye hekima. Kimya changu kimenifanya nijue yeye ni mtu wa aina gani.
 
Kuna Memba humu jukwaani huwa anapenda kusema 'Mpende akupendaye, asiyekupenda usimchukie'... ngoja nimtafute, nikimpata namleta aje kukushauri.
 
Huyo ana bwana lake na ukizidi kumfuata anakuona bonge la king'ang'anizi alafu anachukua point za bure kuwa kuna jitu limekufa na mimi mbaya.IMALISHA MAISHA ATAJISOGEZA YEYE AU MWENYE MVUTO KUSHINDA YEYE.
 
Kuna Memba humu jukwaani huwa anapenda kusema 'Mpende akupendaye, asiyekupenda usimchukie'... ngoja nimtafute, nikimpata namleta aje kukushauri.

Unahisi huyo ndiye mshauri mzuri au na yeye alikutwa na mkasa wa aina hiyo, so ana experience?
 
HIvi unahofu ukimkosa utaulizwa kwa nini? Au umeambiwa kabeba maisha na mafanikio yako? Ya nini umkamie kama vile uliagizwa na Mungu kuwa nenda duniani ukawe na binti fulani maishani, ujue kwa kufanya hivyo unampa kichwa na ni ishara ya kusema njoo uendeleee kunipa pressure. Ya nini uteseke bana, acha tu kwani angekua anakupenda angekua mwelewa so hushangai no call, no beep, no sms bado tu una moyo, uamuzi wako ni sahihi, jikaze jembe.

Huyo member asemaye mpende akupendae ni mimi mwenyewe na TANMO kamaanisha kwamba umpende tu yule akupendaye lakin na yule asokupenda pia usimchukie kwan tu safari moja.
 
Umependa pasipopendeka kaka,imekula kwako na itaendelea kula kwako kama utaendelea kumwazia huyo binti ambaye anaonyesha kabisa hana mapenzi. Yanini kujipa maradhi ya moyo mkuu? uamuzi uliochukua ndio sahihi kuliko kitu kingine. umefanya vizuri kuimwagia tindikali hiyo kamba ya mapenzi inayokutesa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom