Nahisi mfanyakazi mwenzangu ana njama za kuniroga, naombeni ushauri wenu

Achana nae huyo kenge tu "kuna bibi mmoja maika ya nyuma alikuja kwa bi mkubwa akamwambia kauli kama hizo, sasa bi mkubwa akasoma mchezo akamwambia usiniletee mambo yako hapa, baada ya wiki mbili yule mama mganga alikufa, tukahisi yalikuwa yanamshinda akatafuta sehemu ayaweke yatuangamize

Sent using Jamii Forums mobile app
mjomba angu alikuwa anatembea na fisi kwenye sanduku, tulimwogopa sana, kumbe alikuwa mbwa aina ya german shepherd alipewa na mishenari wa kizungu wakati anafanya kazi za ulinzi na shamba boy, kwa ujanja akamfungia ndani watu akawa anawazuga ni fisi.
 
Kuna jamaa mmoja ni mfanyakazi mwenzangu japo hatufanyii kazi sehemu moja na hatukua na mazoea sana japo tulifahamiana maana mara kwa mara tumekua tukikutana kwenye vikao vya pamoja ambavyo hutokea mara chache tu kwa mwaka,

Sasa ilikua ijumaa iliyopita yule bwana tulikutana tena hapa ilikua ni kwenye kikao tena,

Sasa mida ile tunaondoka tukapanda gari moja kurudi makwetu nikajikuta napiga nae stori mbili tatu hadi nikamkaribisha nyumbani kwangu apaone,

Na yeye hakusita kweli akaja kwangu sasa ajabu alipofika ndani akakaa kidogo akatoka nje akaniita nilipotoka nje akaniambia hapa nyumbani kwako ni pachafu sana!

Mi nikashangaa nilikua sijamuelewa nikamwambia labda waifu leo hakufanya usafi, jamaa akaniambia hamaanishi hivyo ye anamaanisha nyumbani kwangu pametegwa madawa ya kichawi duh nilishangaa kusikia hivyo,

Jamaa akaniambia ila nikihitaji msaada atanisaidia tukarudi ndani, tumekaa tena kama dakika kumi akasema tena humu ndani ni pazito hadi jasho limenitoka ni pazito sana hapa inabidi pazindikwe,

Duh story zikaendelea baada ya mda akaniambia nimuoneshe chooni anataka kwenda nikamielekeza alipotoka chooni akarudi ananiambia chooni kwako ni pachafu sana kuna vitu umetegewa!

Kwakweli mi sikumuelewa but ile namsindikiza akaniambia eti nataka kunisaidia anipe dawa ya kuoga nyingine ya kuweka ndan, nyingine anichanje halafu anipe hirizi nifunge ndani,

Duh kwakweli mimi nikamkubalia kinafiki lakini moyo wangu ulisita maana mambo ya kufuga hirizi mi kwakweli hapana sijawai kuyafanya tangu kuzaliwa kwangu,
Halafu then ninunue wembe kabisa jamaa aje anichanje chale? Nikaona hii hapana

Sasa jamaa tangu siku hiyo ananisumbua sana kila mda ananitafuta eti anataka aje kunitengenezea madude,
Amenikomalia sana aisee na hata leo jioni kanitafuta anataka aje nikamwambia nimetoka sipo!

Sasa mi najiuliza huyu anataka kunisaidia au kunipandikizia vitu vyake?

Ushauri wenu jamani huyu mtu nimfanyeje au nimpe mabango asinirudie tena?

NB: huyu jamaa alihamishwa kwenye kituo chake cha kwanza cha kazi maana alikua hapatani na wafanyakazi wenzake walikua wakimshutumu kuwa ni mchawi! Sasa nikilinganganisha tuhuma zake za awali nahisi kabisa jamaa anataka kunipandikizia vitu vyake
Akuroge kwa kipi ulichonacho bana wew unaacha kuwaza vitu vya maana unawaza kurogwa
Huna hata haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshirikina hafai hata kidogo kuwa rafiki, hata kidogo. Yeye akiona kitu kimekaa vibaya anaanza kuwaza kulogwa, kuchezewa. Msipende kuwa marafiki na watu wenye chembe za ulozi na ushirikina.

..na wale walioshika "dini" kupitiliza pia, wapo na vielementi vya ajabu sana. Extremists hawafai kuwa marafiki, watakupa stress!!
 
Hahaha huyo jamaa ana jicho la tatu, anaona tusivyoona wengine, atakuwa katokea Jupiter huyo mdadisi zaidi.
 
Kama shida iko nyumbani kwako yeye kinamuumiza ni nini.
Achana nae huyo tena mwambie kabisa kwamba una amani na hali uliyo nayo na asikusumbue tena.
Halafu sijui alikuonaje hadi kuanza kukuambia hayo maneno ya kitapeli
 
Kapaona kwako panafaa kujenga madhabahu yake. Kishapo aanze kufanya yake... USIKUBALI

Jr
 
Kuna jamaa mmoja ni mfanyakazi mwenzangu japo hatufanyii kazi sehemu moja na hatukua na mazoea sana japo tulifahamiana maana mara kwa mara tumekua tukikutana kwenye vikao vya pamoja ambavyo hutokea mara chache tu kwa mwaka,

Sasa ilikua ijumaa iliyopita yule bwana tulikutana tena hapa ilikua ni kwenye kikao tena,

Sasa mida ile tunaondoka tukapanda gari moja kurudi makwetu nikajikuta napiga nae stori mbili tatu hadi nikamkaribisha nyumbani kwangu apaone,

Na yeye hakusita kweli akaja kwangu sasa ajabu alipofika ndani akakaa kidogo akatoka nje akaniita nilipotoka nje akaniambia hapa nyumbani kwako ni pachafu sana!

Mi nikashangaa nilikua sijamuelewa nikamwambia labda waifu leo hakufanya usafi, jamaa akaniambia hamaanishi hivyo ye anamaanisha nyumbani kwangu pametegwa madawa ya kichawi duh nilishangaa kusikia hivyo,

Jamaa akaniambia ila nikihitaji msaada atanisaidia tukarudi ndani, tumekaa tena kama dakika kumi akasema tena humu ndani ni pazito hadi jasho limenitoka ni pazito sana hapa inabidi pazindikwe,

Duh story zikaendelea baada ya mda akaniambia nimuoneshe chooni anataka kwenda nikamielekeza alipotoka chooni akarudi ananiambia chooni kwako ni pachafu sana kuna vitu umetegewa!

Kwakweli mi sikumuelewa but ile namsindikiza akaniambia eti nataka kunisaidia anipe dawa ya kuoga nyingine ya kuweka ndan, nyingine anichanje halafu anipe hirizi nifunge ndani,

Duh kwakweli mimi nikamkubalia kinafiki lakini moyo wangu ulisita maana mambo ya kufuga hirizi mi kwakweli hapana sijawai kuyafanya tangu kuzaliwa kwangu,
Halafu then ninunue wembe kabisa jamaa aje anichanje chale? Nikaona hii hapana

Sasa jamaa tangu siku hiyo ananisumbua sana kila mda ananitafuta eti anataka aje kunitengenezea madude,
Amenikomalia sana aisee na hata leo jioni kanitafuta anataka aje nikamwambia nimetoka sipo!

Sasa mi najiuliza huyu anataka kunisaidia au kunipandikizia vitu vyake?

Ushauri wenu jamani huyu mtu nimfanyeje au nimpe mabango asinirudie tena?

NB: huyu jamaa alihamishwa kwenye kituo chake cha kwanza cha kazi maana alikua hapatani na wafanyakazi wenzake walikua wakimshutumu kuwa ni mchawi! Sasa nikilinganganisha tuhuma zake za awali nahisi kabisa jamaa anataka kunipandikizia vitu vyake
jamaa anaweza akawa humu, ila kwa ushauri tu achana nae,fanya maombi tu yanatosha,Mungu wetu hashindwi na uchawi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukianza hayo mambo utakua mtumwa maisha yako yote, usijaribu mambo ya ushirikina au kupenda dini sana.
Tena atapotea kabisa, 2020 kweli watu bado wanaongelea kulogona?! Kweli Tanzania ya viwanda haitaonekana karibuni, hatujajuwa ni swala la elimu, imani, upumbavu au ujinga...
Nafikiri atatusikia, hizo nguvu za giza ndiyo mwanzo wa kuuwa albino kama sisi wasukuma, even kwenda kulawiti watoto na kuuwa vibibi vizee...
 
Back
Top Bottom