Nahisi Magufuli anafuata nyendo za Gadaffi

Fedora

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
238
172
Nimemuona mara kadhaa Mheshimiwa JPM akiwa amevaa beji ya Africa kifuani sawa na Hayati Gadaffi, (hii huonesha uzalendo juu ya Africa).

Ikumbukwe kuwa Gadaffi alikua na mapenzi na ndoto kubwa na Africa. Je huenda JPM akawa mrith wa Gadaffi katika kujenga umoja wa Africa?

Wadau mnalionaje hili.
 
Nimemuona mara kadhaa Mheshimiwa JPM akiwa amevaa beji ya Africa kifuani sawa na Hayati Gadaffi, (hii huonesha uzalendo juu ya Africa). Ikumbukwe kuwa Gadaffi alikua na mapenzi na ndoto kubwa na Africa. Je huenda JPM akawa mrith wa Gadaffi katika kujenga umoja wa Africa? Wadau mnalionaje hili.
Kwa nini watu mnapenda kukurupuka kwa ku-generalize vitu??
 
Inawezekana una point ya msingi. Sina shaka na uzalendo wa JPM na sina haja ya kuulinganisha na ule wa Gadaffi.

Kama JPJM ataiongoza nchi hii kufikia nusu ya mafanikio aliyofikia Gadaffi, bila kuendlelez "udictator" unaohisiwa kuanza kujitokeza, Tunamuombea kheri. Kuhusiana na suala la kuunganisha africa yote; hili haliwezi kuwa kipaumbele cha JPJM na wala hana influence yanamna hiyo katika bara hili.

Hata hivyo, kama atabadilisha style yake; atoke kidogo na kujichanganya na wenziwe, inaweza kuchangia katika kurekebisha mambo ya ndani kwake (Muungano - sintofahamu iliyoko Zanzibar) kwanza.

Hili ndilo litamuwezesha kuwa vocal kuhusu masuala ya umoja wa Africa aliokuwa akiutamani Gadafi.
 
Nimemuona mara kadhaa Mheshimiwa JPM akiwa amevaa beji ya Africa kifuani sawa na Hayati Gadaffi, (hii huonesha uzalendo juu ya Africa). Ikumbukwe kuwa Gadaffi alikua na mapenzi na ndoto kubwa na Africa. Je huenda JPM akawa mrith wa Gadaffi katika kujenga umoja wa Africa? Wadau mnalionaje hili.
Ni mapema sana kuwalinganisha Viongozi hawa wawili..Rais Magufuli ameanza awamu yake ya Utawala Kwa kasi nzuri tumuombee Mwenyezi Mungu aendelee na Kasi hii kwa Mafanikio ya Taifa letu. Na binafsi nafikiri ni bora Mheshimiwa Raisi aendelee na aina yake ya Uongozi bila kusikiliza wala kuyumbishwa na siasa za nani anafananishwa nae Kiuongozi.... #Godspeed Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli
 
Enzi za JK mbunge wa Iramba alikuaga anavaa skafu ya bendera ya Tanzania kuonesha uzalendo, alipoingia Magufuli tumeyaona madudu ya wizara aliyokua anaiongoza huyu mvaa skafu. Mavazi sio lazima yalenge moyo wa mtu, moyo wa mtu ni kichaka (kwa mujibu wa Vicky Kamatta) though kimatendo nadhani Magufuli yupo tofauti na yule wa skafu.
 
Nimemuona mara kadhaa Mheshimiwa JPM akiwa amevaa beji ya Africa kifuani sawa na Hayati Gadaffi, (hii huonesha uzalendo juu ya Africa). Ikumbukwe kuwa Gadaffi alikua na mapenzi na ndoto kubwa na Africa. Je huenda JPM akawa mrith wa Gadaffi katika kujenga umoja wa Africa? Wadau mnalionaje hili.
Mie huliona mshazari ngoja tuwasikie wadau
 
Kwa nini watu mnapenda kukurupuka kwa ku-generalize vitu??
Kuanza kufikiri kwa Ku-generalize mambo si mbaya kwani ni moja ya njia ya kutafuta maarifa kwa kina, mbaya ni kuishia hapo kwenye jeneral idea.
 
Magufuli is walking onto the Lee Kuan Yew's footprints
The outcome will depend on the attitude and mentality of tanzanians!!
Huyu "Yew" nachojua alikua waziri mkuu wa singapore miaka ya nyuma. Lkn sifaham impact yake ilikuaje
 
Inawezekana una point ya msingi. Sina shaka na uzalendo wa JPJM na sina haja ya kuulinganisha na ule wa Gadaffi.

Kama JPJM ataiongoza nchi hii kufikia nusu ya mafanikio aliyofikia Gadaffi, bila kuendlelez "udictator" unaohisiwa kuanza kujitokeza, Tunamuombea kheri. Kuhusiana na suala la kuunganisha africa yote; hili haliwezi kuwa kipaumbele cha JPJM na wala hana influence yanamna hiyo katika bara hili.

Hata hivyo, kama atabadilisha style yake; atoke kidogo na kujichanganya na wenziwe, inaweza kuchangia katika kurekebisha mambo ya ndani kwake (Muungano - sintofahamu iliyoko Zanzibar) kwanza.

Hili ndilo litamuwezesha kuwa vocal kuhusu masuala ya umoja wa Africa aliokuwa akiutamani Gadafi.
Nakubaliana na wewe, japo huku kujifungia kwake nchini nafikiri ni jambo la mpito tu hata huo udicteta pia. Huenda akawa na vipaumbele vipana sana kwa africa vinavyofungwa na uchumi tegemevu wa waafrika
 
Gadaf ni mfano mbaya, hukutakiwa kumfananisha rais wetu na gadaf, na kama mfano wako ni kweli basi tujiandae kupigwa mabomu na kuwa kama Libya ilivyo sasa
Gadaffi si mfano mbaya hasa kwa nyanja niliyomfananisha - UMOJA WA AFRIKA, hili ni jambo jema tunalolitaka waafrika, na si gadaffi tu bali waasisi wengi wa afrika walilipigania kama utakumbuka akina kwame nkrumah, samora, madiba, nk wote wimbo wao ulikua Umoja wa waafrika. Libya ya sasa ni zao la "Babelonian system" ambayo sote tunajua nani aliipandikiza huko
 
Kwa nini watu mnapenda kukurupuka kwa ku-generalize vitu??
kiziwi unamsahihisha kipofu! Hata wewe hapo umekurupuka kujibu; kwa nini usimueleweshe na kumuongoza mwenzio kuhusu jambo husika?!
 
Ghadaff alikuwa dictator hatutak Mag awe dictator . AFRICA HAIWEZI UNGANISHWA HATA SIKU MOJA.
 
Du! Salute kwake, kwa mantiki hiyo, JPM atahitaji karibu 30 years kuijenga TZ mpya?

Hiyo ndio tabu ilito mbele yetu, ni lazima na muhimu ajaye aandaliwe kuendeleza harakati hizi au atleast ajiandae mwenyewe kuwa na maono hayo hayo. Hapo ndipo unaweza kulazimika kuamini kuwa maamuzi ya wachache ni sahihi kuliko maamuzi ya wengi, maamuzi sahihi zaidi yanafanywa na kundi dogo sana la watu!
 
Back
Top Bottom