Nahisi Limbwata muda mwingine ni ku pretend au kuna vichwa haziwashiki, sijawai ona mzungu alopewa limbwata na mbongo

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
13,480
2,000
Kwanini mara nyingi wanaume wanaopewa limbwata ni waswahili au waafrika? na unashangaa wazungu wanawapenda waafrika wanawake lakin hawapewi limbwata?

Au tafsiri ya limbwata ndo tunakosea, au wenda kuna vichwa havilimbwatuki hata uloge vipi,

Nahisi limbwata uwashika wanaoamini katika ulimbwata limbwata, mtu kama umesimama imara hata walete madawa kiasi gani hayakushilki..

Kazi kwako ,
 

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
8,592
2,000
Wazungu hawaamini uchawi ila huku Africa Ni balaa..wazungu hawaamini Mambo ya uponyaji makanisani ila huku Africa hatuelewi kabisa.. Iman kitu kibaya sana
 

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
1,709
2,000
Acha uongo wewe, uchawi na miujiza makanisani wazungu ni washiriki wakubwa
Wazungu hawaamini uchawi ila huku Africa Ni balaa..wazungu hawaamini Mambo ya uponyaji makanisani ila huku Africa hatuelewi kabisa.. Iman kitu kibaya sana
 

kancha

Member
Aug 13, 2018
15
45
Unaanzaje kumpa libwata kama anayo mapenzi ya kweli na wewe?,pochi imenona.Libwata ni kwaajili ya wale wanaume watukutu na wengi wao ni waafrika.So libwata ipo kwaajili yenu wanaume wa afrika
 

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,634
2,000
Maskini low exposure,wadada wa kinondoni wamewaloga sana na wamepiga hela ,Kuna mganga Yuko kinondoni studio jirani na sterio baa ndo fundi ,mwingine unamfata kigoma Kuna mahali panaitwa kalya ataleta dola zote
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,077
2,000
Kule kwetu kuna mzungu settler sijui aliongeaje enzi zile za ujamaa aliachiwa mashamba yake.

Mke wake wa kizungu alifariki alioa mdada mweusi. Mdada alimloga jamaa kumbe bwana mzungu aliambiwa na mdangaji kazi na alipelekwa kwa mganga.

Alipozinduliwa alimfurumusha mke kama takataka.
 

Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
3,788
2,000
mkuu hayajakukuta niliishi manyoni singida kwa miezi sita bila kujijua.ilikuwa Kama ndoto iliyojaa mahaba sku hyo akili inanijia nlikuwa niko chini ya mti mkubwa nilaamua kupumzika nipate kivuli baadae akili zinakuja kumbe yule manzi nliekuwa naishi nae pale ni kwake halafu niko mkoani mwake swali lakujiuliza nilifikaje kwake wakati nlkutana nae mkoan kwangu nikatongoza Kama demu wa kuzugia nahisi yule bibie alinipenda kweli na alijua simuhitaj ilibidi ahame na Mimi baada ya kun'gatuka palepale hata viatu sjui nltupa wapi ila skurud kwa Yule manzi ilibidi nidandie fuso wanibebe kishkaji lilikuwa linatoka shinyanga nililikuta pale singida town stendi bahat nzuri lilikuwa linaenda tanga kwa hyo nikafika Home kila mtu alinishangaa nlkuwa wap miezi yote sipatikani wengine walijua nimepotea huu sjui ni uchawi sjui ni limbwata maana Yule nilianza kumpenda kwelikweli hakutaka nitoke hata nje sku hyo nlivyotoka ndo ilikuwa salama yangu laasivyo ningeoa na kutokomea huko kabisa wakazi wa tanga kuna ule unaitwa kupigwa "kipapai" nazani naufananisha na huu

onyo tuwe makini, tufanye ibada tusiwe waongo kama huna mpango nae usimpotezee mda mwambie ukweli ila haimaanishi nitaacha kudanganya maana nshakutana na vitimbwili zaidi ya hivi

samahani kwa uzi wangu mrefu ulikuwa ni ushuhuda tu
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
50,204
2,000
Ukiwa na pesa alafu ukawa bahili utapigwa limwbata na litakukolea vizuri sana, mpaka ukija kugutuka ushachelewa...

Ila ukiwa na pesa alafu mtoaji na muhudumiaji mzuri, hata mwanamke mwenyewe hakufikiri mabaya...

Mchawi pesa...


Cc: mahondaw
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom