Nahisi kuwa mnyonge sana, nahitaji ushauri kwa wenye ujuzi na hili

Pole sana binti mwenye mawazo ambayo kikweli yanavuruga. Jali afya yako Kwanza, mtoto ni majaliwa ya mwenyenzi Mungu. Mbona wapo wengi tu ambao hawana mtoto hata mmoja na wanaishi maisha mazuri!
Sikushauri ubebe ujauzito tena kwa hali uliyonayo kwa sasa. Laiti ungekua mke/mchumba wangu tu nisingekubali uendelee kuteseka hadi wakati huu. Nenda kapate tiba mapema iwezekanavyo, afya yako haina spea. Mawazo uliyonayo ukichukua ujauzito ni kusogeza kifo karibu
Sawa sawa nimekuelewa mkuu.
 
Rudi kwa Mungu anaweza kukusaidia, yeye huanzia pale ambapo akili za kibinadamu kufikia ukomo.. Mtafute yeye kwa imani anaweza kukusaidia..
 
Ishi maisha yako, kama una uwezo wa kulea watoto wako bila mume na unaona hii ndiyo fursa yako ya kuongeza mtoto fanya hivyo.
Mume anaweza kukuacha lkn watoto wako siku zote watakuwa furaha yako.
Zaa mtoto wa kipare
Haya mkuu nimekuelewa ila lazima uangalie mara mbili mbili kabla ya kutenda na sio kukurupuka.
 
Pole sana dada angu ,, mshukulu mungu amekupa mtoto kabla basi haina haja ya kuzaa tena wala kuolewa kwa haraka ili uzae , uhai wako ni bora zaidi ,, usiache mwanao awe yatima sababu ya kuzaa tena
 
Huyo daktari gani anakutisha hivyo?? mbona hayo mauvimbe ni kawaida tu na yanaisha na watu wanaendelea na maisha.

Ushauri wangu badili kwanza hospital nenda Muhimbili lakini pia geukia tiba ya asili, kuna mdau hapo juu kakushauri Mlonge ni kweli kabisa Mbegu za mlonge unasambaratisha hayo mauvimbe wala hautahitaji oparesheni na mimi nakuongezea mafuta ya Habbat Sauda anza sasa kuyatumia kwa kunywa na hata ukipata unga wake pia tumia.

Utakuja kuleta mrejesho hapa ila huo ushauri wa daktari hahaha sijawahi sikia aiseeee.
 
Back
Top Bottom