Nahisi kutapeliwa jamani!!!! Na utaratibu mbovu wa Bodi ya Mkopo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahisi kutapeliwa jamani!!!! Na utaratibu mbovu wa Bodi ya Mkopo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtumishi Mkuu, Jan 26, 2012.

 1. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wakuu, mimi ni mmoja wa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu. Fedha tulizopew/kopeshwa zilitokana ka kodi za wananchi. Kinachokataa kuniingia akilini ni jinsi ambavyo tunatakiwa kulipa hizi fedha. Wengi ni mashahi kwamba kuna idadi kubwa ya waliomaliza elimu ya juu na bado wapo mataan wakibangaiza kuendesha maisha, kwa maana ya kwamba hawana ajira rasmi. Hii kwa namna moja imechangiwa na mfumo tulionao kitaifa.

  Kwa waliobahatika kuajiriwa, wengi mishahara yetu kwa kweli ni midogo na isyokidhi mahtaji ila mbaya zaidi kodi tunayokatwa ni kubwa sana. Ninachokiuliza ni kwamba;
  1. Kwa nini kodi tunayokatwa wafanyakazi kiasi fulani kisitumike kwenye elimu na kuwasaidia wanaohitaji msaada wa elimu ya juu?
  2. Ni kwa nini wanaotakiwa kulipa ni wahitimu wa kuanzia mwaka 1994 na sio wahitimu wote wa vyuo ambao wamefaidika na fedha hizi?
  3. Ndani ya bodi kuna madudu mengi ikiwemo ya ufujaji wa fedha za mikopo, je hii haikatishi tamaa wale wanaolipa?
  3. Utoaji wa mikopo umegubikwa na kasoro nyingi ikiwemo wasiostahili kupewa mikopo mikubwa na wale haswa walengwa wakiachwa bila mikopo. Majuzi hapa kuna mfanyakazi wa bodi ameshutumiwa kwa wizi wa kutumia majina hewa na kijipatia kiasi kikubwa cha fedha, ila bado tunaambiwa waliofaidi mikopo ni lazima walipe na haijalishi kama mtu ana ajira au la. Tunaenda wap jamani?????????
   
 2. W

  Wenger JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Silipi ,Nadhani JK na wote waliosoma bure nao walipe kwanza hapo itaeleweka kidogo ,sio wa kuanzia 1994, BIG NO
   
 3. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #3
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hapa ni kweli tunatapeliwa. Tusubiri baada ya hizo siku walizotoa tujue nini kitafuata.
   
 4. N

  Ndole JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mimi nashangaa sana. Nimeona kwenye website ya loan board jina langu nimiongoni mwa wadaiwa sugu wakati wanakata 30,000/= kuanzia mwaka 2009. Hizi wanazonikata zinaenda wapi kama loan board haioni hela zangu huko???
  Sijui nani anaweza kusaidia hapa kwani hili ni tatizo kubwa sana. Nasubiri mtu aniguse tu ndo ataona cha mtema kuni. Halafu siku nikiona jina langu linatangazwa tena gazetini naenda mahakamani.
   
 5. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mimi nilishaanza kukatwa siku nyingi, sikuwa na ujanja kwani niko kwenye taasisi zilizo karibu na bodi kwa hiyo nilijikuta nimeshaingizwa kwenye makanjanja yao wanakula sehemu ya mshahara. Nimeamua kulipa nikitegemea siku CDM wakiingia magogoni, fedha yangu itarudishwa bodi na watanzania wengine haswa watoto wa wakulima waweze kusoma.

  Kama huna uhakika wa hata mlo, wacha wakukamate wakupeleke segerea ukapate hata mlo mmoja kwa siku.
   
 6. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na bado.....
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu ukiona watu wasiokuwa makini ni hao bodi!! Mimi pia wanakula hizo hela, lakini nimeona jina langu!! Sasa kama wanataka tujikumbushe Makunji, tunasubiri kwa hamu!! Ni upuuzi sana. Watu wenyewe tumesoma kwa shida sababu mikopo haitolewi kwa utaratibu mzuri. Hivi tatizo ni nini haswa kwenye hizi taasisi za serikali? Ni ulafi wa kutaka kutajirika haraka haraka kupitia jasho za wengine au ukenge tu unawasumbua?
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Binafsi nilishaapa zamani kwamba kamwe sintalipa labda wanitundike kamba shingoni ndo ntalipa. na kila wakileta mifomu yao huwa naitupilia mbali, ya nini nijaze wakati najua kina chenge, ra na el ndo wanaenda kuzila hizo hela zangu. Narudia tena sintalipa kamwe, hiyo hela ilikuwa ni halali yangu.

  kodi nnayokatwa kwa mshahara ndo malipo yangu ya hiyo loan nilochukua, full stop!
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  labda waitishe sensa ya wadeni wa HESLB ndo wanaweza kunipata. wao waendelee tu na hao kina eliza wao, watuache walalahoi tuendelee na maisha yetu
   
 10. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kimsingi kama kungekuwa na mfumo mzuri wa kitaasisi nadhani watu wengi wangekuwa tayari kulipa. Ila ukiangalia scandal zinazozikumba taasis hizi halafu bado tukatwe hela...jaman ht wao hawaoni aibu kudai. Kodi tunayokatwa inatosha wasitake kutukamua hadi itoke damu.

  Otherwise warekebishe mwenendo wao na wajisafishe kwanza maana sasa napata picha kwamba serikalini kuna fedha nyingi ila walafi wachache wanazihamishia mifukoni mwao! Alaaa!
   
 11. M

  Makunga JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 772
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 80
  Mi mwenyewe nilishasema haitatokea siku nikalipa hiyo hela,kwsbb najua ni kodi ya wazazi wangu ndo iliyonisomesha.
   
 12. howard

  howard Senior Member

  #12
  Jan 26, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  cha umuhimu tunza salary slip ndio ushahidi wa kupeleka mahakamani kweli
   
 13. S

  Snitch Senior Member

  #13
  Jan 26, 2012
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hoja hapa ni kulipa mkopo sio chadema wala CCM na hata chama tukichukua nchi mkopo na kodi ni lazima jamani...

  Suala tunapenda wengine wawajibike ila sisi hatutaki kuwajibika sasa kosa liko wapi kulipa mkopo.... Na umeshasema ni mkopo kwa mantiki hiyo hata Hawa tuanaosema ni Watoto wa wakubwa wamepata percent kubwa watalazimika kulipa Zaidi so let's just be realistic na Kama kuna mapungufu haya ndio yakuyapigia kelele
   
Loading...