DAMAS DAMIAN
Senior Member
- Apr 8, 2011
- 115
- 54
Natamani hata asubuhi nikiamka nikutane na taarifa kwa vyombo vya habari,
Natamani taarifa hiyo ihusu mabadiliko katika baraza la mawaziri,
Natamani katika baraza jipya Mimi nisiwe mmoja wao tena,
Nibaki na nafasi niliyopewa na wananchi wangu,
Maana sina uwezo wa kuonyesha umahiri wangu wa kujenga hoja, sina uhuru wa kuonekana nachapa kazi, nipo kama sipo, sisikiki wala sionekani popote, hii inafifisha ndoto zangu, inaua vipawa vyangu.
Nisipokuwa na kofia ya Utawala nitapaza sauti itasikika, nitajenga hoja zinazowagusa watu wangu itanijenga, nitasimama katika kweli bila woga, hii itakuwa na faida zaidi kuliko sasa.
Nahisi ndivyo wengi wanavyotamani......