vipik2
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 2,803
- 2,185
Ni wazi mchezo wa siasa wa uchaguzi wa mwaka huu upo tofauti kabisa toka kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi!.
Wameunguliwa zaidi ya wabunge 50 wa upinzani ambapo hajawahi kutokea, uongozi wa Tume Juu mpaka wa chini wote wanatenda kazi kwa niaba ya Mwenyekiti & Mkurugenzi wa Tume ambao wote ni wateuliwa wa JPM.
Kwa mazingira yaliyopo ya huo uongozi CHADEMA kupata hata viti viwili vya ubunge ni sawa na ndoto ya mchana ila ukiwaangalia Lissu & Mbowe inaonekana kabisa wanajua hilo na inaonesha wana njia mbadala katika hilo. Je ni kitu gani wamekipanga? na watakifanikishaje?
Tukirudi upande wa Serikali na CCM kwa mazingira yaliyopo ni kama wanatumia kila njia kujua nini ambacho CHADEMA wanaki-plan, kitu ambacho inaonekana bado ni ngumu kung'amua.
Kingine kinacho nisumbua kichwa kwa nini CCM hawataki kabisa upinzani katika bunge lijalo?
Sote tunajua kuwa pamoja na wananchi wengi maelfu Ku support upinzani but kama hakuna kitu kitakacho intervene hamna mbunge wa upinzani hata moja Tanzania bara 1 atakayekwenda Bungeni.
Mkuu ukiangalia Trend yao vizuri utaona kuwa Wapinzani hasa Tundu Lissu graph yake inaendelea kupanda na kujitanua kila pale anapopata upenyo wa kufanya hivyo akitumia zaidi majukwaa na Social Media zilizo huru ambapo utakuta yeye na supporters wake kuna wakati wanatafsiri kwa kingeereza mambo kadhaa ili wanaoitwa mabeberu wajue kila kinachoendelea
Kwa upande wa chama tawala wao ni kama vile bado wana test mitambo ambayo iliwahi kutumika na wanapoona sasa mahala fulani hapafanyi kazi kwa ufanisi basi huanza kufanya marekebisho kitu ambacho kinawachelewesha kwani mda ni mchache sana na imekuwa kila wakitia mguu wanaona kama maji ni mengi lakini wanaamini vyombo vyao vitasaidia na watavuka
Tatizo ambalo wengi hatujalijua ni kwanini mabeberu hawajakaribishwa lakini wapo karibu sana na uchaguzi huu kiasi ambacho tunaweza kusema kuwa safari hii kuna jicho la tatu? safari hii wote wote wanadukuana kama kawaida na hawana wasi wasi kila mmoja akitegemea kile alichopanda
Mwisho huu ukimya wa watawala kwa huyu Tundu Lissu sio bure kuna kitu wanakijua ndio maana kila mara wamekuwa watu wa kujiuliza s ingawa Tume ya uchaguzi nayo imeelekea kuwa na shingo ngumu kwa kuingia mchezoni bila PPE