Nahisi kama nimerogwa

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Jamani mimi mwili wangu umekuwa mwili wa magonjwa mpaka sasa ivi na hisi nimerogwa kupona siponi. Nime kuwa mtu wa kubadirisha magonjwa Kama nguo.

Nimetoka kwa hili na ingia kwa hili. Jana nilikuwa nimepigwa na headaches. Nimepona asubuhi. Asubuhi iyo iyo nimeshikwa na ugonjwa mwingine sijui ata Kama ni ugojwa gani.

Maana na hisi tumboni patupu hta nikila wapi, nimekula ugali Lakini wapi kushiba sishibi.

Na sikia tumboni kuna nguruma tu na Nina jamba saana na Kunawaka moto.

Nimesha tumia maziwa wapi bado na sumbuliwa tu na ugonjwa huu.

Na Kuna mda moyo wangu una enda mbio Kama ninakimbizwa na watu.

Yaani sasa hivi na hisi hisi kufa tu
 
Kwa maelezo yako una gesi halafu umekunywa maziwa nayo yameongeza gesi, lazima uhisi kufa. Wewe hujarogwa tafuta dawa ya gesi kama unaujua mvuje chuma majani yake yaoshe halafu yachemshe.

Kunywa gilasi moja asubuhi moja jioni na moja usiku pale unakwenda kulala. Kesho utakuwa na nguvu kama chapa ya Konyagi. Kama utafanya hivyo na utaendelea kuumwa nitasaini kupigwa bakora mia na Baunsa wa Diamonds platinum.


Lunatic
 
Change your life style hasa kwenye kula na mazoezi,kwanza rekebisha mlo wako hakikisha unakula vizuri sio unakulakula tu kisha maji ya Kunywa piga maji ndugu tandika mimaji hiyo sio me siku nzima unapiga glass tatu piga maji!,kula matunda kwa wingi acha uvivu hiyo jero ya soda piga parachichi sometimes Kama vocha haina umuhimu achana nayo chukua chungwa au tikiti uongeze na hamu ya naniliu.

Mkuu kiujumla usijinyime kwenye matunda na upunguze matumizi ya vitu vya sukari hizi zisizo rasmi kwa mwili!.. ujifatile pia sio wanyampanyampa tu kapime na vidonda vya tumbo pia usikute nyie ndo mnasababisha hata tunapata mabadiliko ya hali ya hewa..😂 joke hiyo.

Turudi kwenye mazoezi sasa haya ndo yatakufanya unywe na maji mengi maana yatakutoa jasho na sumu kadhaa mwilini,ikiwa pamoja na damu itazunguka mwilini bila mapingamizi ikisambaza ma oxygen na mavitamini ya kutosha ktk mwili wako.. mkuu si lazima upige mazoezi makali no unaweza ukaanza taratibu na mbio fupi ilimradi mwili hakikisha unapata challenge kadri muda unavyozidi kwenda mwili wenyewe utaanza kuomba mazoezi zaidi!.. hebu jaribu haya ndani ya mwezi mmoja au miwili then ulete mrejesho nakuhakikishia hata ndoto zitabadilika mfumo wake zamani ulikuwa unaota unakimbizwa na shetani linamapembe sasa utaanza kuota unakimbizwa na kabinti kazuri Sasa utafanya maamuzi wewe uendelee kukimbia au usimame mkananiliu,binafsi nasimamaga Kuna raha yake bana..😂
 
Pamoja na ushauri mujarabu wa wanajukwaa lakini pia ukipata nafasi mara moja moja tembelea hospitali kubwa kubwa kuangalia wagonjwa, hasa pale taasis ya saratani ya ocean road au muhimbili kuangalia wagonjwa, hii itakusaidia kukutengenezea maana nzuri zaidi ya "kuumwa" na itakupunguzia kulalamika kwa vitu vidogo kama headaches na kukosa hamu ya kula....
 
Pamoja na ushauri mujarabu wa wanajukwaa lakini pia ukipata nafasi mara moja moja tembelea hospitali kubwa kubwa kuangalia wagonjwa, hasa pale taasis ya saratani ya ocean road au muhimbili kuangalia wagonjwa, hii itakusaidia kukutengenezea maana nzuri zaidi ya "kuumwa" na itakupunguzia kulalamika kwa vitu vidogo kama headaches na kukosa hamu ya kula....
Hii mujarrab ×2.
 
Back
Top Bottom