Nahisi kama nimefikia hatua ya Kukata Tamaa kiwango cha Mwisho. Naomba msaada wenu Ndugu zanguni

Status
Not open for further replies.
Mimi hupenda Sana kusoma Visa vya ukweli nakushaurina ili kupata experience za maisha .
Lakini nimepitia nyuzi zako mbalimbali , nahisi wewe na mtunzimzuri ungeweka hi kwenye like jukwaa husika coz juzi upatuo uzi was jengo lako na mijusi nyoka, nk
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Kwanza kabisa huyo mwanamke hakufai achana nae pambana juu ya watoto wako,,pole kwa yote
 
Umesema tangu ufukuzwe kwenye nyumba ya kupanga Wakwe zako hawajakupigia simu yoyote na ww uko kimya wala hujawahi fika..Unafikiri uko sahihi kufanya hivyo??unafikiri kwann wameamua kukaa kimya??una mshutumu mkeo kwa kukusaliti kwenye matatizo,ila ww kuwadharau wazazi wake ni sawa tu?kumbuka hao wazazi wake ndio wanaomsaidia sasa kulea watoto wako baada ya ww kushindwa kufanya hivyo..so kitendo cha kutokwenda kuonana nao na kuzungumza nao kuhusu situation unayopitia sasa ni dharau na ndio mana na wao wakaamua kukaa kimya ili waone mwisho wako..inaonekana ni MTU unaependa kuonekana wa hadhi ya juu tu so kitendo cha uchumi kuyumba kidogo unaona aibu kujitokeza kwa wakwe zako ndio maana umeweza kumiliki gari tatu za kutembelea ilihali uko ktk nyumba ya kupanga..na hata mwenye nyumba nadhani ameona unamletea dharau za kutomlipa kodi yake ilihali unarudi nyumbani na gari pengine anategemea hiyo kodi ikidhi basic needs zake..yaan kukosa kazi tu kunakufanya usiwe na uchungu hata wa kuwatembelea watoto wako ukweni kisa kipato kimeshuka??wewe ni baba wa aina gani,ndio mana huyo mtoto mwingine hataki kuongea na ww kwenye simu amehisi huna mapenzi nae..umeona ukaishi kwa rafiki ni bora kuliko kupata ushauri wowote kwa wakwe zako??come on buddy..Jaribu kujishusha haya maisha hayana mwamba ndio mana yakaitwa ni safari kuna kupanda na kushuka so usione soo... Am sorry brother sikua na nia ya kukukejeli kukudhihaki or sina maana sijaguswa na madhila yanayokusibu Ila nimejarbu kufikri kwa namna nyingine kwa lengo LA kujenga ni hayo tu unaweza fanyia kazi ukiona inafaa pole sana mkuu...
My dear; mwanaume yoyote timamu, ukamilifu wake upo kwenye uwezo wake wa kuihudumia familia yake fully. So hakuna kitu kigumu kwa mwanaume kama kupoteza nguvu yake ya kiuchumi (automatically na nguvu za kiume zinapotea kwa kweli); He is as good as dead. How depressing and humiliating it is, kufukuzwa kwenye nyumba, watoto kushindwa kusoma and above all familia yako kurudi kwa wakwe zako. Ni kama unawaambia wakwe zako "i am useless and unfit for your daughter". Anapata wapi nguvu za kwenda kwa wakwe zake jamani?

Mimi nachoona hao wakwe wangemtafuta jamaa na kukaa naye chini vizuri, hata kama hawawezi kumsaidia financially; wakati mwingine kumpa tu mtu moyo kuwa "usijali, ni changamoto tu za maisha, litapita tu" kunaweza kuokoa maisha ya mtu na kumpa mwanga kwenye giza lake. Imagine muda kama huu afu mkeo ndiyo anakugeuka aiseee.
Huyu mtu yupo depressed; he is vulnerable anaweza hata kujiua au kujidumbukiza kwenye ulevi akafia huko. Ni mtu anayetakiwa kupewa msaada, na sio msubiri hadi aje awaombe msaada. Nilishajionea kwa sehemu; it's not easy at all being in this man's shoes

Sodoku "If God brings you to it; He will be with you in it". It shall be well.....
 
My dear; mwanaume yoyote timamu ukamilifu wake upo kwenye uwezo wake wa kuihudumia familia yake fully. So hakuna kitu kigumu kwa mwanaume kama kupoteza nguvu yake ya kiuchumi (automatically na nguvu za kiume zinapotea kwa kweli); He is as good as dead. How depressing and humiliating it is, kufukuzwa kwenye nyumba, watoto kushindwa kusoma and above all familia yako kurudi kwa wakwe zako. Ni kama unawaambia wakwe zako "i am useless and unfit for your daughter". Anapata wapi nguvu za kwenda kwa wakwe zake jamani?

Mimi nachoona hao wakwe wangemtafuta jamaa na kukaa naye chini vizuri, hata kama hawawezi kumsaidia financially; (hajaongelea familia yake binafsi so far). Wakati mwingine kumpa tu mtu moyo kuwa "usijali, ni changamoto tu za maisha, litapita tu" kunaweza kuokoa maisha ya mtu na kumpa mwanga kwenye giza lake. Imagine muda kama huu afu mkeo ndiyo anakugeuka aiseee.
Huyu mtu yupo depressed; he is vulnerable anaweza hata kujiua au kujidumbukiza kwenye ulevi akafia huko. Ni mtu anayetakiwa kupewa msaada, na sio msubiri hadi aje awaombe msaada. Nilishajionea kwa sehemu; it's not easy at all being in this man's shoes

Sodoku "If God brings you to it; He will be with you in it". It shall be well.....
Heaven sent i love you on this one, you have now proved to me how mature you are. Hii ndio maana halisi ya mke anayejua maisha aisee...Jamaa anapitia wakati mgumu too bad he made a bad choice of a patner ila mwanaume ukishakosa nguvu ya kuprovide you are done! Unahitaji mtu very suppportive otherwise utaishia kwenye depression.
 
Nimejaribu kuvaa viatu vya hyu mwamba aisee kuna watu wanapitia mengi!

Acha niendelee kua wa mwisho kumuamini mwanamke!
Mkuu usiombe kukutwa na bwana pepsi.
Hawa wenzetu linapokuja swala la dhiki na alizoea raha ngumu kuvumilia.
Nikupe moyo na pole sana mkuu.
Hawawezagi vumilia dhiki, thus why unatakiwa uwe makini sana kwenyw kuchagua.
 
Nimeusoma huu uzi nimemkumbuka mke wangu kipindi sina shughuli tumepunguzwa kazini. Mungu ni mwema alinishika mkono pamoja na mashinikizo mengi sana kutoka kwa ndugu zake
Ushukuru mungu ulipata mke mkuu, kuna wenzetu wanaooa sikuhizi wanatia simanzi...Unakaa unapimia kwamba huyu mke siku jamaa akiyumba kimaisha hamna rangi ataacha ona.
 
Nakumbukaga enzi hizo kipindi fulani mzee alipata matatizo ofisini kwakwe menejimenti mpya (wabongo) walipokuja wakamletea fitna akafukuzwa kazi

Tukawa juu ya mawe for three f***king years

Na tulikuwa tuko secondary mtu Kama nne hivi halafu bweni

Bi mkubwa akasimima show hio Miaka 3 mzee Hana hata sumni

Marafiki wwnzake wa kwenye vikao vya bia wakakata mguu na baadhi ya ndugu wakala Kona maana walikuwa wanakuja home kila wikiendi

After three years mzee akala shavu mahali flani .

Since then anajua yupi Ni yupi na mchungu wa hela yake vibaya sana

Nyie akina mama muwe wavumilivu
 
kwanini usitumie elimu yako kujiajiri?

kwa kuwa mil. 6 ambayo ulimpa mkeo kwa ajili ya biashara ikateketea(siyo msimamizi mzuri wa biashara)hivyo uza tena hiyo gari ulionayo ili upate mtaji wa kuanzisha biashara yako kwa kuisimamia mwenyewe.
Biashara so kitu cha kila mtu. Sidhani kama ni ushauri mzuri huumazima yani bora hata gari ibakie. Mie sio muumini wa kuuza uza vitu dhiki ikinikaba. Bora uongeze madeni tu kwa watu ila si kuuza vitu vyako.Atapoteza
Kama hii simuliizi ni ya kweli Kwanza kabisa pole na matatizo yalokupata
Mkeo hakufai kabisa kwanin akukimbie kwenye matatizo ?na baba wa watoto watatu kabisa hata kama mngekuwa hamjazaa hakupaswa wala kuthubutu ,anakupenda ukiwa na pesa tu pili kapata kibarua alitakiwa akubebe akulee akutunze kwa kidogo anachopata hadi hapo utakapopata kazi ,kama ni kweli kafanya hivyo hakufai maisha yako yote Mungu anakupa funzo na kukufunua macho uone
Matatizo ni sehemu ya maisha mlilie muumba wako akupitishe kwa haya magumu unayopitia
Pia inatufundisha tusitegemee chanzo kimoja cha pesa tuwe ma vyanzo vingi vingi vya kupata pesa
Nakuombea kila la kheri urudie hali yako ya zamani

Wanawake tubadilike pia jamani tusiwakimbie waume zetu kisa pesa tuishi katika hali yoyotw ile tukiwa pamoja na kubebana

Jaman wenye uwezo wa kutoa ajira toeni kwa huyu kijana
Yani bora leo umeongea mwenyewe maana kwenye mada za kuwachana live mnatuitaga mario. Ila life lina change...Hayo ndio madhara ya pesa yangu ni yangu mwenyewe yako ni yetu. Mke wa aina hii lazma akukimbie kwenye majanga kama hivyo ila kipindi zipo alikuwa anajiachia kisenge na hela za mume. A selfish woman is an evil.
 
Biashara so kitu cha kila mtu. Sidhani kama ni ushauri mzuri huu! Atapoteza
mazima yani bora hata gari ibakie. Mie sio muumini wa kuuza uza vitu dhiki ikinikaba. Bora uongeze madeni tu kwa watu ila si kuuza vitu vyako.
ushauri wako kwake ni upi?

je aendelee kukaa kwa huyo rafiki yake akisubiri kuajiriwa kama zamani?
 
Nakumbukaga enzi hizo kipindi fulani mzee alipata matatizo ofisini kwakwe menejimenti mpya (wabongo) walipokuja wakamletea fitna akafukuzwa kazi

Tukawa juu ya mawe for three f***king years

Na tulikuwa tuko secondary mtu Kama nne hivi halafu bweni

Bi mkubwa akasimima show hio Miaka 3 mzee Hana hata sumni

Marafiki wwnzake wa kwenye vikao vya bia wakakata mguu na baadhi ya ndugu wakala Kona maana walikuwa wanakuja home kila wikiendi

After three years mzee akala shavu mahali flani .

Since then anajua yupi Ni yupi na mchungu wa hela yake vibaya sana

Nyie akina mama muwe wavumilivu
Mkuu hizo ndio aina za wanawake wa kuoa sasa. Mamaako angekuwa mbinafsi angemkimbia mshua amini kwamba. Wanawake wa sikuhizi wengi wabinafsi ni mbegu mbaya sana kuoa mwanamke wa hivyo. Usije ukaoa mke ambaye hawezi hata ku spend buku lake kwako! Utakuja kunikumbuka siku moja.
 
ushauri wako kwake ni upi?

je aendelee kukaa kwa huyo rafiki yake akisubiri kuajiriwa kama zamani?
Hapana mie naona atumie gari lake kama fursa ya kumuingizia kipato mkuu, kama ni Noah which i think it likely is atafute sehemu akatege awe anabeba abiria kama kidala dala itamlipa au atafute watoto wa shule awe anawabeba kistaili. Itamsaidia ila akiuza gari na amezoea hela ya kuchota hamna kitu atafanya.

Angekuwa na spirit ya biashara angeshafanya huyu jamaa from the beggining baada tu ya mambo ya kazi kuanza kuyumba.

Option nyengine atafte sehemu ambayo anaweza likodisha gari wakamlipa kwa week week.
 
Nafikiri pia inategemeana na misingi mliojijengea maana sisi bwana we huwa tunasamehe ila hatusahau. Tunasubirigi siku ulivuruge ndio hapo paap tunakukamatia, labda mtu awe na busara za hali ya juu sana.

I have a friend nae mume wake aliwahi kupitia hali kama hii, ila kutokana na kwamba her husband was always good to her alichukua nafasi yake alisimama na mume wake na akamchukulia mkopo ambao aliutumia vizuri na leo wamesimama kabisa. Lakini kabla ya hapo walikaa chini wakazungumza wakapanga mipango inayotekelezeka na wakawa wana na options kabisa.

Masualaa ya biashara hayahitaji kukurupuka, lasivyo ndio mtu ataona bora akabeti au apeleke kwa matapeli.

Sent using Jamii Forums mobile app
Biashara inataka kujipanga haswa
 
Toka mwaka jana september hana kazi lakini mwezi wa nane mwaka huu walipata mfanyakazi mpya
 
Kabisaa kitendo cha kusema alikua anamiliki gari tatu mbili kubwaa halafu hana kitega uchumi chochote cha kumwingizia hata elfu 10 kwa siku itoshe kusemaa huyu mwamba kichwani hayupo vizurii...
Huyu Ndugu kanishangaza aise gari tatu si mtaji mkubwa sana wa Mpesa huo tena na nyumba ya vyumba viwili na chenji inabaki kabisa kumbe kuna watu wana fursa wanazichezea aise.
 
Nimeshangaa Sana kuna nonsense nyingi kwenye andiko.

Kungekuwa nauwezo wakubadilishana viatu ningempa vyangu anipe vyake ningehitaji nini tena kwa Mungu.
Huyu Ndugu kanishangaza aise gari tatu si mtaji mkubwa sana wa Mpesa huo tena na nyumba ya vyumba viwili na sebule na chenji inabaki kabisa kumbe kuna watu wana fursa wanazichezea aise.
 
Chakii sidhani kama umenielewa hapo niliposema muwatende mema. Kumpa mtu mtaji wa biashara pekee haitoshi. Sisi ni watu wa hisia zaidi. Wanaume mnaposhika pesa huwa mnajisahau sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Utakuwa huna shukurani basi...Na mke wa aina hio wanakuwaga so demanding. Atakuwa alikuwa anamshughulisha sana jamaa. Kila kitu anapewa ila atlast 6M kweli useme mwanaume hana upendo? Watu wanalilia kanga tu hawapewi.
 
" Mimi ni member wa Jamiiforums kwa kipindi kirefu kidogo. Nimekuwa nikishirikiana na kushirikishana nanyi mambo mbalimbali ya maisha na pia ya burudani. Nimewaza kwa muda mrefu sana kabla sijaamua kuandika thread hii.

Nlikuwa nmeajiriwa na Kampuni moja ya Mambo ya IT na usafirishaji pia toka mwaka 2015. Nikifanya kazi katika nafasi mbalimbali Kama Operation Manager, Public Relation Manager na pia nikisaidiana na Managers mbalimbali katika majukumu yao niki coordinate Projects mbalimbali za Kampuni.

Mwaka 2017 Kampuni yetu ilianza kuyumba. Tuliyumba sana kutokana na mambo mbalimbali ya Soko (Wateja wetu wakubwa walikuwa ni kutoka Serikalini na Makampuni Makubwa)

Tukawa kama mtu aliyepata ulemavu wa mguu mmoja. Tulijitahidi sana kupambana na kuzoea hali hiyo ya kutumia mguu mmoja. Hali iliendelea kuwa mbaya. Bahati mbaya mpaka kufika katikati ya mwaka 2019 tukawa hatuwezi hata lipana mishahara.

Tukawa tunapeana posho na hatimaye ikafika hatua hata posho ikawa ngumu. Tuliendelea kujitahidi kupambana hadi ikafikia hatukuwa na uwezo wa kulipwa kitu kabisa. Hivyo mwaka huo kuanzia mwezi wa 9 hatukuwa tunapokea anything in terms of money.na hatimaye Kampuni ikatuomba sisi wengine tuandike barua ya ku resign au tufukuzwe kazi. Binafsi nliona hali ilivyokuwa.sababu before that pia CEO alituomba tuwe free kuacha kazi.

Mimi nlikuwa katika watu wachache ambao niliamini tungepambana tukashinda hali ile.nikaomba niendelee. Nikawa natumia pesa yangu na hatimaye akiba yangu yote kwisha. Nikauza gari moja nipate pesa ya nauli na matumizi nyumbani.

Mke wangu hakuwa kazini. Nilimpa pesa Mil 6. Akafanye biashara. Bahati mbaya sana akapoteza hizo pesa zote katka biashara akichangiwa hasa na Haya makampuni ya GNLD na Q-Net. Mtaji ukaisha.

Tukaamua tena kuuza gari nyingine ili watoto waende shule na pia tujitahidi kumalizia ujenzi. Hapo tulipokuwa tunaishi pia ilibidi tulipe kodi. Hatukukamilisha ujenzi.

Nifupishe habari. Toka mwaka jana mwezi wa 9 nmepambana sana kutafuta kazi.lakini sikufanikiwa pesa hizo nlizokuwa nazo ilibidi pia niingize kwenye matibabu kwa sababu ya ugonjwa nliokuwa nao mguu wa kulia una tatizo la maumivu makali kwenye mfupa na kushoto kiasi.

Nimehangaika sana Aga Khan, Hindu Mandal na Moi. Walinipa ushauri wa kupunguza uzito na kutotembea sana (Ugonjwa unaitwa Heel Spurs) so ikabidi pia nibakize gari moja liwe ndo la kutembelea.so nikabaki na gari dogo.

Maisha yalizidi kuwa magumu na hatimaye kodi ikawa ngumu kulipa.ikapita miezi 2 mwenye nyumba akashindwa kutuvumilia. Akaja tukatoa vitu nje. Watoto wangu wawili walikuwa wanasoma Elimu ya Msingi(mmoja hajaanza bado nina watoto watatu) wakarudishwa nyumbani.

Siku tunalazimika kutoa vitu nje it was a very humiliating day. Mimi, mke,dada wa kazi na watoto wetu watatu.Mke akaamua kuita gari lije chukua vyombo kupeleka kwao. Siwezi sahau siku hiyo.Ndo siku ya mwisho kumwona mke wangu mpaka leo hii hatujaonana tena.

Vitu vilipakiwa kwenye gari ikawa inatakiwa kulipia tsh 150,000 mke wangu akataka nitoe pesa, sikuwa nayo. Wife akapiga simu kwa mdogo wake akamtumia. They left mimi nikiwa sielewi nifanye nini.

Nlitoka na gari nikaenda park sehemu nikakaa mpaka usingizi uliponipitia nlikuja shtuka saa 2 usiku sina pa kwenda kulala.mfukoni nina tsh 7000 tu. Nlitumia 1000 kununua mihogo na 6000 nikaweka kama balance. 1000 nilienda lipia wanapolaza magari.nami nikashusha kiti nikalala kwenye gari mpaka asubuhi.

Kwa siku 3 nlikuwa nahangaika sina cha kufanya. Nilipata wazo la kuwasiliana na rafiki yangu wa shule ya msingi. Nlimweleza tatizo langu akanishauri niende kwake ana chumba cha wageni nikaishi naye.

Kiukweli kwa umri wangu wa miaka 30+ nlijisikia vibaya sana.nlienda ishi naye.sikuwa na namna.

Nashukuru kuna marafiki wachache ambao hawakunitupa ktk jambo hili hata kwa kunitia moyo na mwingine kunisaidia hata pesa ya voucher au usafiri.

Katika kipindi hiki nimepoteza sana marafiki. Wengi walikata mawasiliano kabisa.hata napopiga kuwasalimia.(si kuomba pesa) wamekuwa hawapokei simu zangu.

Nmekuwa hata natuma texts kuwasalimia na sometimes kuwaomba wanikumbuke zinapotokea nafasi za ajira. Wameacha kujibu.

Binafsi nilikuwa ni mtu ninayeshirikiana na kila mtu.sikuwahi bagua mtu au mtendea mtu ubaya. Maisha yangu sikuwahi kunywa pombe au kuvuta sigara.

Nimekuwa na majonzi hasa kutengwa na familia yangu. Mke wangu amekuwa si wa mawasiliano ya karibu nami. Ni kama amesusa. Watoto kila napoongea nao wanalia na kutaka turudi kuishi pamoja. Mmoja ameamua kabisa kutoongea nami hata napoomba kumsalimia.Hataki.

Nashindwa kwenda kwa wakwe kuisalimia familia yangu. Lakini nashindwa zaidi kwenda mikono mitupu kuonana na familia yangu. Wakwe zangu hawakuwahi nisemesha lolote hata baada ya kuona mke amerudi kwao. Nimewaelewa pia kwa hilo.

Mke wangu alifanikiwa kupata kazi sehemu. Lakini bado amekuwa akitaka nimtumie pesa za matumizi hata ndogo ndogo ambazo angeweza saidia mwenyewe.nafahamu anafanya hivi kuniumiza zaidi au kuonesha kuwa ni mwanaume irresponsible.

Naumia sababu wazazi wangu ambao nlipaswa niwe nawasaidia wao ndo wanatuma pesa kiasi wapatacho kuisaidia familia yangu. (Wao wanaishi Mwanza) Baba yangu alishastaafu.hana kazi.mama yangu pia anafanya tu ufugaji mdogo mdogo.

Naishi kwa fadhila za wadogo zangu na rafiki yangu huyu ambaye namwonea huruma pia. Nina Elimu ya Degree (naomba nisitaje ya nini/nisitoe details nyingi isipokuwa kwa mtu ambaye tutawasiliana inbox privately ikiwa atakuwa na namna ya kunisaidia)

Leo nimeandika kwa majonzi thread hii baada ya kutumiwa tsh 5000 kwenye simu na msichana ambaye alikuwa housemaid wetu akiwa huko aliko na wife. Yeye ananikumbuka.

Nmeumia kwa alichoandika (baba najua unaumia huko uliko pokea hiyo hata ya vocha mimi nakuombea ufanikiwe) nmejaribu kumrudishia hiyo pesa ametuma zaidi 7000 na kutaka nitumie.

Juzi nlipata simu kwa mtu ambaye nikiwa kazini aliwahi patwa na tatizo la kikazi alipokuwa ameenda kikazi Kampuni flani na kushawishika kuiba kitu flani. Nikiwa PR nlienda shughulikia jambo hilo.bahati mbaya ushahidi ww CCTV Camera ulimwonesha yule bwna mdogo akitenda jambo hilo. Muda huo akiwa amewekwa chini ya ulinzi na gari ya Kampuni imezuiliwa. Nlimsaidia akatolewa na siku mreport kazini zaidi ya kumwonya na kumshauri.

Alionekana kujutia kosa lake sana. Mwaka na nusu umepita juzi kanikumbuka nikiwa sina hata tsh 500. Mfukoni akanitumia tsh 30,000. Nlishamsahau.akanambia tu "Boss nimekuumbuka naomba hiyo uweke mafuta" nlimshukuru sana. Hajui kama sina kazi.

Haya mambo yananiumiza zaidi na kuona nina deni zaidi kwa familia yangu,rafiki zangu na wanaonizunguka.

Ndugu zanguni. Nipo katika msongo wa mawazo. Naona i have failed my family. I have failed my parents and relatives. Nliwaza kumeza dawa nyingi sana kukatisha maisha yangu. Mara kadhaa yananijia hayo mawazo.

Nashindwa nifanye nini. Nahangaika kuomba kazi na kutafuta kazi.tatizo langu la miguu halinipi nafasi ya kufanya kazi ambayo ntasimama sana, au ntatembea sana.

Nmetengwa nimebaki peke yangu.najiona mzigo kwa huyu rafiki yangu na familia yake.naona pia nmekuwa so humiliated.

Naombeni msaada wa kazi. Kazi katika upande wa kusimamia projects,kusimamia hata madereva pia naweza kuwa dereva wa mtu(gari ndogo) gari nayotumia haiwezekani kuwa Uber najua kuna mtu anaweza nishauri hivyo.ilikataliwa kwa namna ilivyo.

Pia nina uzoefu katika kufundisha ngazi za certificates na diploma masomo ya management, customer care, social skills,communication skills, development studies.

Ni mzuri katika kuongea na kuandika pia english and swahili ( do not consider this article it is informal)

Najua watu wengine wata kebehi,watanidharau na kunikashifu.nitayapokea yote. Kwa mtu ambaye atakuwa radhi kujadiliana nami jambo hili in person nipo radhi. Nahitaji kazi niweze saidia wengine pia. Si vyema nikaendelea pokea misaada toka kwa watu wengine. Nahitaji pia kuishi na familia yangu.

Nipo Dar Es Salaam kwa sasa naishi Bunju. Asanteni"
Umeshachukua mafao yako?
 
Mkuu hizo ndio aina za wanawake wa kuoa sasa. Mamaako angekuwa mbinafsi angemkimbia mshua amini kwamba. Wanawake wa sikuhizi wengi wabinafsi ni mbegu mbaya sana kuoa mwanamke wa hivyo. Usije ukaoa mke ambaye hawezi hata ku spend buku lake kwako! Utakuja kunikumbuka siku moja.
Mbegu ilipandwa Beijing na imemea kweli kweli. Tunaona matunda yake. Dada zetu wametekwa na dunia. Zile morals za til death part us hawana mpango nazo. Mpango ni "wanawake na maendeleo". Wasomi wengi ndio wahanga.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom