Igombe fisherman
JF-Expert Member
- Apr 28, 2017
- 2,027
- 3,565
Juzi jumatano nimejiunga kifurushi cha wiki cha UN cha airtel cha tsh 5000 nikitegemea sitonunua tena vocha kwa ajiri ya kuwapigia jamaa ndugu na marafiki. Ila kitu cha kushangaza jana tarehe 19/12/2019 napiga simu naambiwa huduma katika sim card yangu zimethitishwa. Wakati ninadakika zaidi ya 600 ndani ya sim card nilichoka.
Nikafungua data nikakuta wengi wanalalamika hapa jamiiforums nikahesabu maumivu.
Nikalidhika na kutuma sms tu na kuchati fb na jf kupitia hilo salio. Ila kitu cha kushangaza nilipiga simu kimakosa tu. Badala ya kuruhusu card two ifanye kazi mi nikaamuru card one ifanye kazi na simu ikawezeshwa ndio nikagundua wamenifungulia huduma. Tena bila lile tangazo la usajiri wa nida.
Nawashukuru sana airtel kwa kutusikia japo mlikuwa na makosa kutufungia kabla ya muda mnaotuimbia kila siku tukipiga simu. Sasa hivi nalonga bila kiwewe mpaka mtakapoifunga tena tarehe 31/12 maana sina hiyo namba yenu mnayoitaka. Japo kuna watu mnawatumia namba zao na mimi kwenye kujiandikisha katika vitambulisho nilitumia namba yenu katika form. Kama vipi nitumieni nami namba ya NIDA. Maana huku kwa wavuvi mumetawala ninyi tu katika mawasiliano hivyo tukio la jana limetudhuru sana watu wa nyanza
Sent using Jamii Forums mobile app