Nahau za Nape: Mkulima, nyani na mahindi

Hapa wengi mnapaogopa kwanini?
Nape ni ccm damu tena ile inayowaita wafadhili wa miradi mbalimbali na bajeti mabeberu lakini yeye leo kawabatiza na kuwaita wakulima.
Wananchi mliokuwa mnaifaidi misaada ya wafadhili walioitwa mabeberu na kisha wakulima sasa wana jina jipya ambalo ni nyani!
Sasa wafadhili ( mabeberu/ wakulima) wameondoa michango na misaada yao kwenye bajeti na miradi ambayo leo imeitwa mahindi na kilichofuata ni wananchi/ nyani kufa njaa na kutambua umuhimu wa wafadhili/ wakulima!
Upo sahihi Nape kwani wananchi/nyani njaa hii ikiendelea hivi kwa miezi sita ijayo ule mkanda wa mwl. Nyerere wa mwaka 1979-80s haukwepeki lazima tuufunge na kuukaza sana hadi utukate kiuno!
 
Fumbo mfumbie mjinga mwerevu ulivumbua(kuna issue iko njiani inakuja maana jamaa kabakisha Mwaka mmoja na kila MTU atajijua yupo kundi gani)
 
Kwahiyo kwa akili yako wewe, Nyani ataanza kazi ya ukulima!

hapana, nyani hawezi kulima, lakini hata wakati mkulima analima mahindi hayakuwa na manufaa yeyote kwa nyani, yalikuwa yanalindwa na mwenyewe.

Kwenye reading comprehension hutakiwi kuongeza ya kwako kutoka kichwani. Tumeambiwa nyani walikuwa wanafukuzwa!

Mkulima kafa, na afe, what difference does it make? We weren’t getting the corn anyhow.
 
Tunapiga vita Mabeberu waondoke, na tunafurahi the way wanavyofunguliwa kesi mf, makinikia nk
BUT
siku wakiondoka Jumla ndio tutajua kuwa budget yetu wao ndio walikuwa wana finance
 
Mkulima alikuwa na faida gani kwa nyani kama mahindi yake walikuwa wanafukuzwa wasile?

Nape amechemka.
Nilifikiri bado nahau, fasihi, misemo inafundishwa ulivyojibu inaonyesha Kuna shida mashuleni.

Inahitaji fasihi kuelewa misemo na akili kuipambanua.pole
 
Anazungumzia kuzuia bunge live

Nape alijisahau kuwa yeye ni ccm na ccm ni yeye kumbe hata muazilishi wake aliwahi kusema CCM SIO BABA YANGU WALA MAMA YANGU; lakini Nape amejitoa akili kuwa yeye bila ccm hana maisha tena, na Indio maana wenzie wa kuja watamfukuza!!
 
Back
Top Bottom