Nahau - hebu tujikumbushe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahau - hebu tujikumbushe

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by WomanOfSubstance, May 18, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kiswahili chaenda kikipanuka na kukua kila siku.... hivi kuna nahau gani mpya isije ikawa tuna zilezile za zamani tu ...pia tutofautishe nahau na methali...........tujuzeni wajuzi wa kiswahili.
  Asanteni
   
 2. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Pangu pakavu mama tia maji!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mchakato
  sintofahamu
  mrishonyuma(feedback)
   
 4. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mtarimbo umelala doro
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Mhh we tausi wewe....
  Haya.......
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mh, mada ngumu!! kiswahili kwa wengi enzi za O level kilikua chanzo cha penati kwenye divisions

  kuna semi, nahau, methali na hapo ndio mtihani unaanza... let alone tanakali, takriri, tashtiti na mengineyo

  mwe!
   
 7. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kuna ngeli za majina, vihisishi, mofimu, misimu, viwakilishi, viunganishi, duh kweli kiswahili kiboko....
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  gademu... Umenikumbusha mbali sana preta... Merci! Arusha yenu mvua tupu na tope kiatu kimekua raizoni
   
 9. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  ha ha ha...pole na karibu sana...hii mvua imetukatili lakini tunafurahi kwa kupata neema hii....karibu utembelee na huku Yaeda...nyanyi wameongezeka sana msimu huu
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Na'as desi... But t'laau
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  vivumishi, vishazi, vilai, na tungo tata, usisahau viambatanishi, afu usiombe mwalimu awe mnoko we!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  May 24, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kwa wale ambao wanajiuliza nahau ni nini...nahau kwa Kiingereza ni idiomatic expression....
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mswahili asiyejuwa nahau itakuwa KAACHWA KWENYE MATAA ni nahau nayo kumbe!
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Nimeanza kusahau haya mambo hebu mwageni somo tujifunze kwa upya elimu haina mwisho
   
 15. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Asiyejua maana haambiwi maana.

  Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi

  kusema ukweli vinanichanganya kati ya nahau, methali na misemo.

  Fuata nyuki ule asali

  tembea uone
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  May 25, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mpiga mbizi nchi kavu, uchubua usowe!
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  May 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  NDIO HAPO SASA!
  Methali ni proverbs au?
  na Nahau ni idiomatic expressions..au mnasemaje wajuzi wa lugha?
   
 18. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #18
  May 25, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Nimeamini kuwa ni kweli mimi sijui kiswahili wala kiingereza. Na lugha ya kwetu milimani nayo haipandi.
  Aibu tupu!
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  May 25, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  asante mkuu, yani mie ndio kiazi wa both.... nimejua rasmi kwamba ujanja wangu ni kuunga-unga sentensi tu... nothing more!!!

  kuna hii inasema "mwenda tezi na omo... marejeo ngamani" ina maana gani?
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  May 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tuendelee na nahau mpya...na tutofautishe na methali
  Labda tuangalie idioms ili tuone kwenye kiswahili kuna nini...

  to kick the bucket = to die = kukata kamba = kufa ( Hapa tunaona kuwa haihusiani na kamba wala ndoo)
  can of worms = trouble = kuleta kasheshe = matatizo ( Hakuna cha kopo wala minyoo/wadudu japo vimetumika)
  Being up in arms =to be very angry in protest -=kupandisha munkari/hasira
  A bone of contention = source/locus of argument - mtanange = kinachopambaniwa

  Haya tuendelee kwa mifano zaidi
   
Loading...