Nahamia Mwanza: Mitaa ipi ya uswahilini ni mizuri kuishi?

ChamaDola

JF-Expert Member
Dec 23, 2016
3,432
2,804
Wakuu,

Niko mbioni kuhamia Mwanza,kwahiyo ningependa kukaa mitaa ya uswahilini.

Nimeishi Tandale Beo Beo,Tandale Lindo la Kuni,Mwenge na Tegeta kwa Dar.

Kwahiyo ningependa kupata mitaa kama hiyo Mwanza ukiacha Tegeta

Maeneo yawe vyumba vya 10,000-15,000 yenye muingiliano mkubwa wa watu,magenge na kwenye kupata mahitaji mengine kirahisi!
Shukrani.


Rockcity.jpg

Mods:I Appreciate your service!
Thanks for the photo uplift!
 
Wonderful ahahaha kwamba nalikimbia jiji kwa sababu ya albadiri!?
Mkuu miye japo ni kada mtiifu kwa Chama,ila ni die hard pro-Lissu number one fan...fuatilia threads na michango yangu humu!

Lissu ni mtani wangu,miye Mnyiramba,halafu ni mwanasheria in the making,kwahiyo ni rais wangu pia wa TLS!
 
Kichwa Kichafu nimeishi tandale karibu nusu ya maisha yangu,na sidhani kama maisha ya mwanza yatakuwa laisi kuliko Dar!
Nataka nibadilishe mazingira!
 
Igombe itakufaa. tsh 600 kwenda mjini. usafiri unaondoka kila baada ya nusu saa. Sangara na sato bei chee, chumba haizidi tsh 20000
 
Back
Top Bottom