Nahamia Mwanza kusaka maisha ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 ambapo pia huduma za kijamii zinapatikana kwa urahisi?

Kilimahewa ,nyasaka kiloleli, nyakato meko,nungu,national,buzuruga,kiseke,kona bwiru na maduka 9 ni sehemu zenye mishe na hazina uswahili zaidi ukilinganisha na kirumba,mabatini,igogo na the like

Kwa igoma ni mbali pia pamepooza akishindwa sn atleast pasiansi

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Nimeamua kubadilisha mazingira ya utafutaji kutoka Dar kwenda Mwanza.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili natarajia kusafiri, naomba msaada wa kufahamu ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 na kuna huduma za maji, umeme na usafiri wa kwenda mjini ni nafuu na wa uhakika, na hakuna vibaka na wahuni wengi.

Nawasilisha
Up wap kwa sasa
 
Mwanza rocky city

Karibu sana ule sato sangala ugalia wa udaga

Njoo ukae mitaa dampo town unatembea tu
😆🤓😂
 
Wakuu,

Nimeamua kubadilisha mazingira ya utafutaji kutoka Dar kwenda Mwanza.

Mwanzoni mwa mwezi wa pili natarajia kusafiri, naomba msaada wa kufahamu ni mitaa ipi nitapata chumba cha elfu 30 na kuna huduma za maji, umeme na usafiri wa kwenda mjini ni nafuu na wa uhakika, na hakuna vibaka na wahuni wengi.

Nawasilisha

Kama Dar umefeli basi mwanza hautoboi.


"New York, if you can make it here, you can make it anywhere
We still here! And we buildin four more new towers" - Diddy
 
Tafuta mabatini.

Kuna gari nyingi zinazoingia ruti hio hata usiku.

Usiende kirumba wala kitangiri wala igogo.

Huko kuna ushenzi mwingi, hasa igogo.

Ukipenda nipigie 0744033555.

Nimeikimbia Mwanza nimekuja Dar na mafanikio nayaona. Nabana matumizi kama vile ntazikwa na hela haha
Mkubwa nasikia kuna wababe wanakaba watu hata mchana hapo Igogo
 
Kapange kirumbaa ama ghana waweza pata vyumba kwa bei hiyo na ni sehemu ya karibu na mjini,,,,,,,,,,ukitaka nje ya mjini nenda buhongwaaa maisha ni marahisi kuna soko la vyakula linalolisha sehemu kubwa ya Mwanzaa utajifunza mengi,na vyumba vipo vya bei hio ,nauli to town tsh400

Kila la kheri
Mkubwa vipi mafuriko mvua zikinyesha hapo Buhongwa
 
Mkubwa nasikia kuna wababe wanakaba watu hata mchana hapo Igogo
Igogo ni kiini cha ujambazi na ushenzi toka enzi

Watu walivamia sana hayo maviwanda na kuiba mafuta na wengi walitajirika sana

Igogo ina mpangilio mbaya sana wa makazi, kama.ilivyo manzese buguruni and the like...

Ngoja mdau aendw huko ajifunze mengineyo
 
Kwanini unaondoka Dar mkuu?, kama ni biashara imekuwa ngumu Dar basi sikushauri kabisa kuchomoka hapo. Labda kama una sababu tofauti au biashara unayoenda fanya Mwanza ina link na Dar hapo sawa

Ila vinginevyo, komaa na Dar tu.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom