ndyoko
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,971
- 1,650
Jamani hii kitu imekuwa inanisumbua kwa muda sasa ndani ya nyumba! Hivi karibuni nimefunga cable service kutoka kwenye kampuni moja hapa nnapoishi. Binafsi hawa jamaa wana channel nyingi za mpira, wanyama, cartoon, movies, yaani ni kama dstv kwa asilimia 100. Kwa bahati mbaya-kwangu- na nzuri kwa watoto, ni kwamba kuna channel moja ya movie za akina kanumba-namaanisha za kiswahili.
Kivumbi ni kwamba karibu watoto wote wanapenda kuangalia kama sio movie za kiswahili basi ni katuni. Yaani muda mwingi wamekuwa wakifanya hivyo, na wanaponiona mimi nakuja, utaona kabisa ni kama wanakosa raha maana wanajua, hapa Baba anakuja kubadili channel na kuweka kama sio channel ya mpira, basi ni discovery world au geographic channe, au animal planet au geographic wild, cnn, sky news au bbc. Hali hii nimeiona kwa muda mrefu sasa mpaka nimefika mahali nimeona kama naingilia uhuru wa members wengine wa familia, kwa maana nahisi wanaanza kuniona mimi kama mbinafsi vile. Imefika mahali sasa nimeamua kutokaa sebuleni, najifungia chumbani na kufanya kazi nyingine huku nikijua kuwa kuna mambo ya maana nayakosa lakini ntafayaje sasa watoto wenyewe wana mind wakiona nahamisha program wanazozipenda.
Kwa kuwa nimehisi huenda wanashindwa tu kusema, nami sijui nifanyeje maana kama kuna mpira au kuna issue ambayo ni 'educative' huwa najikuta nahamisha channel ili kuangalia hiyo progam bila kujali hiyo mipicha yao ya kina kanumba.
Hebu wakuu naombeni ushauri wenu, nifanyeje au nyie mnatumia njia gani, ili watoto waone kuwa na wewe kama mzazi unajali interest zao? Nakwazika, sasa kukosa mpira, kisa katoto ka chekechea kamekomalia remote kuangalia katuni/movie za kina kanumba wakati mie nataka nione Arsenal inavyochabangwa na kina Drogba. Nishaurini wakuu njia nzuri ipi nitumie ili watoto wasione kuwa Dingi Mnoko!
Nawasubiria!