Nagombea Moshi Vijijini kama mgombea binafsi

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa majaji jana kuwa kushiriki uchaguzi kama mgombe binafsi ruksa.

Nategemea wiki hii kutangaza kugombea jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Ninatarajia kurudi Dsm mwishoni mwa mwezi, karibuni kwenye mkutano wangu wa kujitangaza tarehe 10march, 2010 hoteli ya Rombo Green View kuanzia saa nne
 
Wow...!
Eee bana eee!
Wewe ni mwanajamvi wa 5 sasa kuonyesha wazi nia ya kugombea.
Hivi kumbe we ni mtu wa Moshi!
 
Toa mawasiliano yako ya simu ya mkononi na barua pepe ili waandishi wakutafute. usijifiche tena we public figure bwana waandishi wakuulize nia na malengo yako kisiasa. una tofauti gani na mrema na wengine walio wabunge au wenye nia kama yako.
 
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa majaji jana kuwa kushiriki uchaguzi kama mgombe binafsi ruksa.

Nategemea wiki hii kutangaza kugombea jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Ninatarajia kurudi Dsm mwishoni mwa mwezi, karibuni kwenye mkutano wangu wa kujitangaza tarehe 10march, 2010 hoteli ya Rombo Green View kuanzia saa nne

Ni haki yako ya kikatiba usilaze damu changamkia bwana.
 
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa majaji jana kuwa kushiriki uchaguzi kama mgombe binafsi ruksa.

Nategemea wiki hii kutangaza kugombea jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Ninatarajia kurudi Dsm mwishoni mwa mwezi, karibuni kwenye mkutano wangu wa kujitangaza tarehe 10march, 2010 hoteli ya Rombo Green View kuanzia saa nne

Mie nataka kumvaa mzee wa vijisenti hukoooooooooo Bariadi..wanaJF ntatoa contacts soon.
 
Ndugu yangu
1. Hongera kuonyesha nia kama mgombea binafsi lakin kumbuka kwamba bado wanachi hawajapata elimu ya kutambua kwamba kuna kitu kinaitwa mgombea binafsi.
2. Wewe unatarajia kugombea Moshi Vijijini lakini unataka kutangaza nia yako Rombo Green Viwe hotel,ni kosa kubwa kisiasa.Unatakiwa kutangazia jimboni kwako..Wapiga kura wako wako Moshi na sio Rombo hata kama watakuwepo ni very few..
 
Mie nataka kumvaa mzee wa vijisenti hukoooooooooo Bariadi..wanaJF ntatoa contacts soon.

Malugumangu ongea vizuri naona hilo jimbo tupo wengi hata mimi muda si mrefu nategemea kutangaza nia yangu ya kugombea jimbo la Bariadi Mashariki nimekuwa nikipokea ujumbe mwingi kutoka kwa wananchi wa Bariadi kuwa wananihitaji nikawatumikie na wito huo ninao.
 
Sioni umuhimu wa kugombea kama mgombea binafsi. Chagueni chama mkiimarishe sasa ili muwe mmeshiriki kujenga taasisi itakayotumiwa na watu wengine kuijenga Demokrasia nchini.
Kugombea kama mgombea binafsi ni dalili za woga, uvivu na ubinafsi.
 
Sasa,MWALIMU MAKINI,kama wewe huoni umuhimu ndio iwe kigezo cha hao wanaonuia kuwa wagombea binafsi wasifanye hivyo?

Unazungumzia "kuchagua chama wakiimarishe ili wawe wameshiriki kujenga taasisi itakayotumiwa na WATU WENGINE kujenga demokrasia nchi".Kwa ni hao wanaotaka kusimama kama wagombea binafsi SIO WATU PIA?

Hivi mwoga anaweza kusimama peke yake?Au mvivu atawezaje kumudu pilikapilka za uchaguzi peke yake?Na hilo la ubinafsi linatoka wapi wakati anagombea ili aongoze wengine na sio familia yake binafsi kama ilivyo huko CCM?

Napenda kuamini kuwa jina lako la MWALIMU MAKINI halina mahusiano na umakini wako
 
Sioni umuhimu wa kugombea kama mgombea binafsi. Chagueni chama mkiimarishe sasa ili muwe mmeshiriki kujenga taasisi itakayotumiwa na watu wengine kuijenga Demokrasia nchini.
Kugombea kama mgombea binafsi ni dalili za woga, uvivu na ubinafsi.

25 divided by 5 is equal to 14.......lol
 
Nasubiri kusikia comments za Sitta kuhusu issue hii. Maana ilipoletwa na mtikila na mahakama kufikia uamuzi kama huu, Sitta akiwa waziri wa sheria alifanya janja, nasubiri kwamhamu sana kumsikia sasa.
 
Nimefurahishwa sana na uamuzi wa majaji jana kuwa kushiriki uchaguzi kama mgombe binafsi ruksa.

Nategemea wiki hii kutangaza kugombea jimbo la Moshi Vijijini kwa tiketi ya mgombea binafsi.

Ninatarajia kurudi Dsm mwishoni mwa mwezi, karibuni kwenye mkutano wangu wa kujitangaza tarehe 10march, 2010 hoteli ya Rombo Green View kuanzia saa nne

uamuzi mzuri sana huo, hongera. sasa swali dogo tu kwa nini iwe Rombo Green View na isiwe popote pengine?
 
Habari Njema kukusikieni ndugu mkionyesha nia ya dhati kugombea. Nasisitiza nia ya dhati maana hili ni jamvi la watu makini na sitegemei mtu aje na habari ambazo hajazifanya maamuzi.

Kwakua hili ni jamvi la waelewa na watu wenye busara na uwezo wa kuchambua mambo na washiriki kutoka kila kona ya taifa hili na dunia hii. Nashauri tuanzishe thread ya wagombea toka humu JF ambapo kila mwenye nia ya dhati atajitokeza kuelezea nia yake, jimbo, chama na wadau na wanazi wa siasa wa huku wanaweza kusaidia aidha kwa kutoa mchango hadharani au kwa kumPM mgombea mwenyewe ili November tukirudi hapa baada ya uchaguzi, tuwe tumesaidia kuongeza idadi ya wabunge wanajamvi.

Nawakilisha
 
Uwanja wa mapambano upo Moshi, wewe wataka kutangazia nia yako Dar ama watumia missiles kaka 'mpiganaji', teh? Nenda katangazie Moshi walipo hao unaotaka kuwaomba ridhaa and actually labda watakuhisi mwenzao rather than nao kukusikia tu kwenye media.
 
Vyama vya siasa vinapewe ruzuku kwa ajili ya kampeni, je wewe utapewe au umesha jiandaa?
 
Majaji wetu wanatupitisha mahali pa kihistoria. Naamini Mtikila atavishwa taji la ushujaa kwa mapambano haya aliyoyaanzisha kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Wengine wamebaki kudai katiba mpya wakati kuna vipengele ndani ya katiba vinanyima raia haki za msingi na vinaweza kabisa kupingwa mahakamani na haki ikajitokeza, lakini hawajafungua hata kesi moja. Changamoto: Chadema na Wakili Tindu Lisu saidieni kwa kupitia njia hii kurekebisha sheria ambazo zina utata na ambazo ni kikwazo katika utawala bora.
 
Ningependa usilete utani, uwe siriasi. kama unatania apologise please. haya mambo si ya masihara.
 
Sioni umuhimu wa kugombea kama mgombea binafsi. Chagueni chama mkiimarishe sasa ili muwe mmeshiriki kujenga taasisi itakayotumiwa na watu wengine kuijenga Demokrasia nchini.
Kugombea kama mgombea binafsi ni dalili za woga, uvivu na ubinafsi.

katiba ya mgombea binafsi itakuwa na mambo binafsi mengi kuliko mambo ya jamii. Ubinafsi utakuwa mwingi zaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom