Naghenjwa Kaboyoka atangaza kugombea Same Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naghenjwa Kaboyoka atangaza kugombea Same Mashariki

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by bangusule, Jun 22, 2010.

 1. b

  bangusule Senior Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  wananchi walikuwa wanamtaka mama Kaboyoka "mama maendeleo" baada ya kumchoka Ndhira Yona lakini CCM na mama Kilango wakamfanyia mizengwe. wananchi walifikia mpaka kupeperusha bendera za CCM nusu kuonyesha kukasirishwa kwao na mizengwe ya CCM. vitisho na mizengwe ilitumika kuwalazimisha wana CCM wa same mashariki kumchagua mama Kilango.

  mama kilango amekuwa fundi wa kupiga makelele ya ufisadi na kutafuta umaarufu katika vyombo vya habari. huku same mashariki ameshindwa kabisa kusimamia na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

  ELIMU IMEDORORA: kwa kipindi cha miaka mitano, mama Kilango ameshindwa kulikwamua jimbo letu toka kushika mkia mkoani Kilimanjaro katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.

  KILIMO,MAJI,na MAZINGIRA: kuna ufisadi wa kutisha katika ukataji miti na uchimbaji udongo ktk maeneo ya misitu na vyanzo vya maji vya wilaya ya Same. hali hii inatishia kuua kilimo cha umwagiliaji na kusababisha balaa kubwa la njaa wilayani Same. wakati wananchi wamekuwa wakimhitaji nyumbani kuongoza vita vya kupambana na ufisadi huu, yeye amewatupa mkono na badala yake kupigana vita ya kiini macho ya EPA.

  wananchi tunamtaka chaguo letu la mwaka 2005 Naghenjwa Kaboyoka "mama maendeleo."


   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  FMES uko wapi?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  SO LONG AS NI USHINDANI SIDHANI NI ISHU..Go for it my sister Naggy KABOYOKA!!
  Ushindani ni kitu bora na wala kisitafsiriwe kuwa ni uadui.
   
 4. b

  bangusule Senior Member

  #4
  Jun 22, 2010
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  2010 kura yangu kwa Naghenjwa "mama maendeleo"

  Naggy Kaboyoka: Gwiji la kupambana na umasikini wilayani Same

  2005-06-05
  Na Mwandishi Wetu


  Unapofika kwenye kila Kata wilayani Same, Jina la Naggy Kaboyoka ni maarufu kuliko hata wanasiasa.


  Kwa kifupi, kinachompa sifa na umaarufu mama huyu, ni tabia yake ya kujikita katika matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.


  Kutokana na juhudi zake katika maendeleo, mahali penngine hata jina lake halisi hawalitumii tena, bali wanamuita mama Maendeleo.


  Wengine humwita mama Danida, na sehmu nyingine hujulikana kama mama wa Benki ya Dunia (World Bank).


  Nilimuuliza Mama huyo Msomi mwenye shahada Mbili, kisa cha kuitwa majina hayo.


  'Unajua shughuli zote za kuwaletea maendeleo wananchi hawa, nazifanya kwa kushirikiana na wafadhili.


  Kwa mfano miradi mingi ya maendeleo niliyoifanya Wilayani Same husuasan Jimbo la Mashariki, nilikuwa nashirikiana na Shirika la Maendeleo Denmark DANIDA - Ndio maana kule wananiita jina hilo.


  Na ukifika kule Kongwa mkoani Dodoma ambapo Benki ya Dunia imeanzisha mradi mkubwa wa maji , basi wananiita kwa jina hilo,'anasema.


  Huyu Mama Kaboyoka Ni nani? Nipashe ikataka kumjua kabla ya kuingia kwa undani kuhusu kazi anazozifanya.


  Amezaliwa miaka 55 iliyopita huko Gonja Wilayani Same na niwapili katika familia yao ya Mzee Amaniel Mzanyuma, mtu maarufu wilayani hapo kama Mcha Mungu na Mtumishi wa Kanisa.


  Anasema kama kuna mtu anamshukuru hapa Duniani ukiachilia mbali Mungu na wazazi wake, basi ni Mume wake Bw. Kaboyoka, ambaye amemuwezesha na kumpa fursa ya kusoma nje ya nchi na mara nyingine kufanya kazi huko.


  'Mambo ninayowafanyia wanavijiji kule Same, Kongwa au Mkuranga, yanatokana na elimu na uzoefu nilioupata. Nisingepata mambo haya kama sio Mume wangu kunipa fursa hiyo,'anasema.


  Akiendelea kusimulia historia yake ya utumishi kwa watu, wakati huo akiwa mtumishi wa DANIDA, Mama Kaboyoka anasema alikuwa anatoka kuwasaliamia wazazi wake Gonja Mjema kule katika milima ya Same, alipofika eneo la Tambarare alikutana na watu wamembeba kwenye machela mama mjamzito.


  Anasema mama yule tayari alishafikia hatua ya mtoto kutoka tumboni huku mwenyewe akiwa na matatizo ya afya.


  Anasema ilibidi ageuze tena gari ili limpeleke mama yule kuokoa maisha yake na yule kichanga.


  Anasema kuanzia hapo akaanza kujiuliza 'Tatizo liko wapi? Mbona wananchi hawa wanabidii na juhudi za maendeleo, Kwanini wapo nyuma?


  Mama Kaboyoka anasema baadae akajilaumu kidogo, lakini akajipa moyo kwa vile kosa alilolifanya lilikuwa halijapitiliza, na wakati bado ulikuwepo wa kulirekebisha.


  Kosa gani hilo? Anasema alikuwa ameishi Ulaya muda mrefu lakini hakutumia Elimu yake, uwezo wake, na umaarufu kuwaletea maendeleo watu waliomzunguka.


  Ni kosa kubwa sana kwa wanawake kudhani hawawezi kuleta maendeleo, vilevile ni kosa kubwa kwa wanajamii kuwadharau na kuwapuuza wanawake wanaojitoa mhanga kuleta maendeleo,'anasema.


  Bi. Kaboyoka anasema baada ya kujua watu wa vijijini hususan wilayani Same wana matatizo sugu ya Maendeleo, alikaa chini na kuainisha moja baada ya jingine na jinsi ya kuyatatua.


  Anasema tatizo kubwa aliloliona ni Mawasiliano. Barabara hakuna licha ya wananchi kujitolea mara nyingi kutengeneza.


  Tatizo jingine ni elimu, afya na ukosefu wa miradi ya kuwaongezea kipato wananchi hao.


  Vilevile tatizo jingine alilokutana nalo, ni ukosefu wa maendeleo shirikishi, kwa maana kwamba, hapakuwa na mawasiliano, wala majadiliano ya kimaendeleo, baina ya wananchi na viongozi wao.


  'Cha kwanza kwa kushirikiana na wafadhili niliwapelekea wananchi gari la wagonjwa katika Hopitali ya Misheni ya Bombo,'anasema.


  Anaongeza kuwa lengo la msaada huu ni kuwezesha kuchukua wagonjwa, kufanikisha chanjo kwa watoto na kupeleka kliniki za muda kwa wanamama wa vijiji vya mbali.


  Pia alisambaza vitanda vya wagonjwa na vile vya kuzalishia wajawazito katika hospitali ya Wilaya ya Same.


  Mama Kaboyoka anasema wakati anashughulikia tatizo hilo alishangaa kuona katika Shule Moja ya Sekondari (Dindimo) wasichana walikuwa wamegeuza darasa kuwa Bweni.


  Yaani usiku wanaweka virago wanalala humo, asubuhi wanaondoa virago linakuwa darasa.


  Anasema ikabidi tena ajenge mabweni pamoja na kuongeza madarasa katika shule hiyo.


  Anasema habari njema za msaada zikaenea kwa haraka na kujikuta anafuatwa na shule nyingi kama Ile ya Suji ajenge mabweni, jambo ambalo alikubali na kuchangia ujenzi wa Sekondari ya Kimala Mpinji.


  Anasema mwaka 1997 aliunda mfuko wa Maendeleo WOYEGE, kwa ajili ya kuwainua wananchi kiuchumi na kijamii.


  Lakini kwa bahati nzuri akarudi London kuendelea na shughuli zingine.

  Hata hivyo, baada ya kurejea hadi sasa yeye ndiye mkurugenzi Mtendaji wa WOYEGE.


  Mkurugenzi huyo anasema kila alipojitosa kushughulikia tatizo moja, alikua akigundua matatizo mengine kibao ya wananchi.


  'Kwa mfano niligundua wananchi hasa kina mama, hawana kipato, hivyo nikaamua kujikita katika kuwaanzishia miradi midogo midogo,'akaongeza.


  Anasema aliwapelekea gari la mizigo ili kuwasaidia akina mama wa Halmashauri ya Same.


  Miradi mingine ni kuwajengea Bwawa la samaki akina mama wa Kata ya Chome ili waweza kuzalisha Mbegu na kuzisambaza kwa wale wenye vibwawa vidogo, na wakati huo huo, wakiuza samaki na kupata Kitoweo.


  Kusambaza maji Same mjini, ili kuwarahisishia kina mama kupata maji na kuwaanzishia kina mama hao mradi wa kufuga nyuki kwa ajili ya kuuza asali na Nta.


  'Kwa kweli niliona akina mama wanamatatizo mengi ya kiuchumi na kijamii, nikawapatia mashine za kusaga akina mama wa Kata za Vunta na Makanya, ambao hapo awali, ilibidi wabebe vichwani mahindi na kutembea nayo zaidi ya kilometa 20 kwenda kusaga,'anasema na kuongeza 'Pia nikaona akina mama hawana sehemu ya kubadilisha mawazo, wala sehemu ya kuonyesha vipaji vyao katika uzalishaji, hivyo tukawajengea Centre kwenye Kata ya Mpinji,'


  Anasema ili kutatua tatizo la barabara, alianzisha mradi uliokuwa na mafanikio makubwa, kukarabati Barabara ya Kizangaze hadi juu ya Mlima yaani Bombo.


  Mwingine ni kuwajengea vijana wa Kata ya Bwambo kiwanda kigogo kwa ajili ya kazi za Stadi.


  Anasema katika kutekeleza miradi yote hii, alikuwa bega kwa bega na wananchi, hivyo utekelezaji wake ukawa rahisi.


  Anasema kiongozi ambaye anawashirikisha wananchi kujiletea maendeleo ndiye anayefaa kwa wakati huu.


  Uliwezaje Kutekeleza miradi hii? Na nichangamoto gani ulizokutana nazo katika harakati zako?


  Mama Kaboyoka anasema Jambo la kwanza ni elimu yake, pili juhudi, tatu, kuaminiwa na nawafadhili hasa wa nje ya nchi na nne, kuwashirikisha watu.


  Anasema licha ya Shahada zake mbili za Mambo ya Maendeleo ya Jamii huko The Hague Uholanzi, lakini hakuishia hapo bali amehudhuria kozi mbalimbali zaidi ya saba katika nchi mbalimbali za Ulaya.


  Pia anasema Katika sehemu alizokaa na kufanya kazi kama Ufaransa, London, Uholanzi, alijijengea uaminifu kutokana na juhudi katika kazi.


  Anasema ni kutokana na kuaminiwa ndio maana anapata kipaumbele katika misaada.


  Anasema amekutana na Changamoto nyingi kuhusu maisha ya watu wa vijijini na jinsi walivyo na kiu ya kupata maendeleo.


  Anasema hivi sasa anayo habari njema kwa wanavijiji hao, kwamba WOYEGE imepata mlezi ambaye ni waziri wa mambo ya Katiba wa Uingereza Bi. Harriet Harman.


  Anasema mama huyu ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Camberwell na Peckham huko Uingereza, amepewa jukumu la kumshauri waziri mkuu Tony Blair kuhusu mambo ya Umaskini barani Afrika.


  Anasema anamshukuru Waziri huyo, ambaye alitembelea nchini kwa kumpa mwaliko.


  'Nitakwenda London mwezi ujao, kuitikia mwaliko huo, na nitatumia fursa hiyo, kupata uwezo zaidi wa kuwasaidia wananchi wa vijijini na ikiwezekana kuanzisha miradi mipya ya maendeleo,'anasema Bi. Kaboyoka.


  Mkurugenzi huyo anasema licha ya kujikita zaidi kwa Wilaya ya Same, lakini WOYEGE pia ipo katika wilaya zingine, ambapo Wamejenga Wodi tatu katika Hopitali ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.


  Kueneza elimu ya Afya ya uzazi wa mpango, Kusaidia yatima wajane na kuwaanzishia miradi ya kuku mbuzi wilayani humo.

  Pia anasema Benki ya Dunia imemteua kuwa mtaalam mshauri (Consultant) katika mradi mkubwa wa kusambaza maji wilaya ya Kongwa kule Dodoma.

  Kuhusu matarajio, Mama Kaboyoka anasema anakusudia kuanzisha miradi mingine mikubwa ya kuwasaidia wanavijiji, mara atakaporudi Uingereza.


  'Nia yangu si kujidai, wala kutafuta sifa, bali kuonyesha jamii kwamba hata wanawake wanauwezo mkubwa wa kusaidia nchi yetu.

  Ni jambo la aibu tupu kuona barabara za vijijini kule Same hazipitiki, mazao ambayo yangewaingizia kipato yanaozea shambani, kwa vile magari hayafiki.

  Wakati wazee wetu na vijana wanapata taabu, wasomi tunaoaminiwa hata nchi za nje tupo 'Kweli hii ni aibu, mimi nimeamua kuifuta,' anasema.
   
 5. Mavella

  Mavella JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2014
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Namkumbuka mama huyu wangekuwepo watu kumi ambao sio wabinafsi kama yeye natumaini jimbo la same mashariki lingekuwa na maendeleo.
   
Loading...