Nafunga Novena kuna Supervisor ameutesa sana moyo wangu pale jalalani

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Ameniumiza sana, umeuvunja moyo wangu vipande vipande. Kinachoniuma zaidi si yeye kunichelewesha nisimalize shule kwa wakati bali ni maneno ya dharau na kejeli ambayo amekuwa akinitamkia.

Amenifanya mimi ni kiumbe duni kabisa nisiyesitahili heshima wala kuthaminiwa. Nimevumilia na kuwa myonge kwa muda mrefu. Kwa sasa nimeamua kufunga novena Mungu wangu atanitetea tu.
 
Mkuu pole
Kuna watu wamesoma PhD miaka 5-6 wengine Masters miaka 4-5..ni huzuni kwa kweli. Ukiuliza sababu ni kucheleweshwa kwa kazi toka kwa Supervisors. Watu wanalia imagine mtu umetokea kazini, ruhusa inaisha bado kitabu kibichi.

Pambana na uvumilie haswa, jifanye mjinga umalize tu hakuna namna.
All the best rafiki!!!
 
Asante mkuu
 
Ameniumiza sana, umeuvunja moyo wangu vipande vipande. Kinachoniuma zaidi si yeye kunichelewa nisimalize shule kwa wakati bali ni maneno ya dharau na kejeli ambayo amekuwa akinitamkia.

Amenifanya mimi ni kiumbe duni kabisa nisiyesitahili heshima wala wala kuthaminiwa. Nimevumilia na kuwa myonge kwa muda mrefu. Kwa sasa nimeamua kufunga novena Mungu wangu atanitetea tu.

Mkuu elimu haina shortcuts unless unataka degrees na PhD za kina msukuma na zile za chupi. Huo muda wa kufunga novena utumie kufunga na kusoma mahitaji ya kumalizia degree yko na sio kumnuwia supervisor, ninaamini hakuna supervisor anaeza kukubania bila sababu za msingi
 
m

Nafahamu kabisa hakuna shortcut kwenye elimu ya juu kama hii. Kinachoniuma ni huyu jamaa amenitamkia maneno mabaya sana kwa muda mrefu, chuki yake kwangu iko wazi kabisa.
 
Ndo maana wajanja anachukua supervisor ambaye anaona wataenda sawa.......otherwise huyo supervisor yuko frustrated with your progress, anaona kama hakuna madini ya kutosha kwenye hatua uliyofikia....
 
Ni jinsi gani ya kufunga novena mkuu, na mimi nna jambo langu.

Kuhusu maswahibu yako, pole sana ndgu.
Novena inaendana na namba Tisa hivyo omba kwa kutumia hiyo namba Tisa labda funga masaa Tisa au siku Tisa, sali jambo lako mara Tisa huku ukichagua watakatifu gani waungane na wewe kukuombea.
 
Back
Top Bottom