NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
siongei sana, wacha tunyoke moja kwa moja kwenye hizi points zaidi ya 20

Bei ya iphone ipo juu kwasababu haitaki ushindani

rg.PNG

Iphone ni kama unaposafiri safari ndefu kwa basi, huwa kuna ile migahawa ipo highway sehemu ambazo hakuna makazi, bei ya "robo sahani" ya chipsi na vimishkaki vidogo ni elf 5 na huwezi kuwaambia kitu, Android ni kama kwenda mtaa wenye migahawa kibao, hapa kwavile kuna ushindani muuzaji yupo tayari akuuzie chipsi "sahani nzima" na mishkaki ya kushibisha kwa buku tatu na hapo faida yake ni ndogo sana, utalia chips zako kwenye sahani ya udongo, maji ya kunywa yapo bure unajimiminia, kabichi utawekewa, pilipili ipo, n.k..... Bidhaa za iphone kama iphone 13 pro max gharama ya utengenezaji ni milioni 1 lakini wanaiuza milioni 3 na nusu hii ni kwasababu kampuni haitaki ushindani wa kuruhusu makampuni mengine yatengeneze simu zenye system ya iphone, pia iphone wanatumia mbinu ya "prestige oricing", mfano mrahisi ni mkanda imara wa ngozi unauzwa elf 20 lakini mkanda wa manyoya ya paka unauzwa laki kwa sababu una nembo ya Nike, Gucci, n.k.

Kwa upande wa android ushindani ni mkali sana, si ajabu kukuta simu imetengenezwa kwa milioni 1 ikauzwa kwa milioni 1.3, unaanzaje anzaje kwa mfano kuuza chipsi za elf 5 mtaa uliojaa migahawa inayouza chipsi buku 2 sahani nzima, ushindani ni mkali mpaka watu wameamua kuweka viyoyozi, tv, maji bure, n.k ?

Android inaweza kufanya mambo mengi kwa mpigo kirahisi (multi tasking)
vgv.PNG

Kufanya shughuli zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho kimebanwa sana kwenye iphone, mfano ukitaka kuhamia app nyingine wakati upo kwenye video call basi video call itakata ili uweze kutumia app nyingine, Android unaweza kutumia hata apps hata 10 kwa mpigo na ndio maana kuna kitufe maalum katika vile vitatu ambacho ni maalum kwajili ya multi tasking, kwenye android pia kuna split screen ambayo inafanya screen igawanyike katika vyumba kadhaa kwa shughuli unazotaka kufanya kwa mpigo. (Iphone nao wanataka uiweka hii ila sijajua lini)

Kwenye iphone hakuna tundu la kuchomeka earphones
123.PNG

Kitu walichofanya iphone ni kulitoa tundu ili kuwakamua pesa watumiaji wao kwa kuwalazimisha wanunue earphone zao zisizo na waya zinazouzwa kuanzia laki 2 na inabidi uzichaji kila siku, wabongo wengi uchumi ni tatuz huwa wananunua earphone za iphone feki za elf 30, hata iphone wanazonunua ni za mchongo zilizotumika (refurbished) za bei rahisi.

Kwa android uchaguzi ni wako, unaweza uamue kutumia earphone za waya au waweza nunua zisizo na waya kulingana na bajet yako. Earphone za waya zina umuhimu wake, huwa hazihitaji kuchajiwa kila mara, huwa zinasaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia mtu akitaka kukuibia simu yako unastuka.

Usb cable za Android zina nguvu, spidi na rahisi kupatikana.
gvbj.PNG

cable za usb-c zinatumika kwenye simu nyini za androif, redio, camera, tochi, power bank, speaker, n.k. hii inafanya upatikanaji wake kuwa rahisi mno, hata ukienda vijiji vya porini huko unaweza kuazima cable ya kuchajia redio uchajie simu yako ya android. cable za usb-c zina speed kali mno kwenye kuhamisha mafaili, pia cable za usb c zina nguvu kubwa sana ya kuchaji (fast charging). Cable za iphone hapa hazifu dafu.

Android kuna apps nyingi kuliko Iphone
google-play-store-vs.-apple-app-store.jpg

Playstore ya Android kuna apps nyingi kuliko Appstore ya Iphone, Sababu kuu ni kwamba, ili mtengenezaji wa app aiweke app yake kwenye playstore ya android atalipia elf 55 (55,000) mara moja tu lakini kwa upande wa iphone kuweka app kwenye appstore ni lazima ulipie laki 2 na elf 30 (230,000) “kila mwaka”, hapa ndipo watengenezaji wengi wa app wanakimbilia kutengeneza apps za android sababu ni bei rahisi na pia watumiaji wa android ni wengi kuzidi iphone. Iphone walitaka kuzifanya app zao za facetime na i-message ziteke soko kama kile kipindi cha bbm ya blakberry lakini kwa ujio wa whatsapp, telegram, zoom, n.k mpango wa iphone ulidoda.

Iphone huwezi kurekodi simu
m.jpeg

Kwenye android ukiwasha voice / sound tecorder unaweza kurekodi simu, simu nyingine za android zinakuja na feature ambayo unavyopiga au kupokea simu kuna option ya kurekodi simu. Kwenye iphone hii feauture imeblokiwa, hata ukijaribu kurekodi screen wakati upo kwenye maongezi huwa inakataa, kuna njia mbadala kama app ya mimic unayolipia laki kila mwaka ila ni hatari maana kitu kinachofanyika ni kwamba mawasiliano huwa yanapelekwa kwenye server ndio yanayatumwa kwak, mawasiliano yakienda kwenye server tayari mtu mwenye server anaweza kuyasikia.

Simu ya android yaweza kutumika na mtu zaidi ya moja (multi user)
ij.PNG

Hii inaitwa multi user, simu inaweza kutumika na zaidi ya mtu moja bila kuingiliana mambo, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k. utampa simu aitumie bila wasi wasi, wewe unakuwa kama admin flani hivi. Ni nzuri pia kwa mtu anapenda kuazima simu yako ila anapenda kupekua pekua visivyomuhusu.

Iphone inatengenezewa vifaa na kampuni za simu za android
fghjk.PNG

Samsung huwa wanatengeneza simu za android lakini pia wanawauzia iphone vifaa kama vioo, processor, nano flash, n.k. hii ni kutokana na uimara wa vifaa vya samsung ambavyo vilimvutia iphone...

Android utatumia internet bure bila bando
bhb.jpg

Mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, lakini hayo mambo ya kujibana hayapo android maana kuna apps kama ha tunnel, your freedom, n.k. zinafanikisha utumie internet bure. unaweza kutumia GB 100 kwa wiki na wala isiwe habari, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone za milioni 3 matoleo mapya pale mlimani city, shida inakuja kwa hawa wa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja na kila muda simu kaishika mkononi ili watu waione, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

Iphone haina memory card
me.PNG

Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ukasindwa kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card, Lakini pia iphone inaweza kuwa na gb 200 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ila kama ilikuwa na memory card basi utaichomoa kadi yako na ukayakuta mafaili yako yakiwa salama. hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu iende, pia unaweza kuwa na memory card unayohamishia mafaili na kuitunza sehemu salama ili hata simu ukiibiwa isiwe shida.

Iphone unapews GB 5 kutunza picha, Android hakuna kikomo
IiOUnZXJT6w-MQ.jpg

Kwenye iphone kuna icloud ambayo utapewa GB 5 bure za kutunza picha, kwa upande wa simu za android utatunza picha kwenye google photos bila kikomo.

Notch ya iphone inaziba vitu kwenye screen
vgvgvgv.PNG

.Notch ni kile kisehemu cheusi juu kwenye screen chenye camera na sensor, kwenye iphone huwa ni kipana sana na huwa kinakuziba usione video nzima, pia kuna apps nyingine unakuta zinajaa na kupitiliza kwenye screen sehemu ya kwenye notch unashindwa kuona ama kuminya.

Ni shughuli pevu kuperuzi / kuhamisha mafaili ya iphone
Capture.PNG

huku android tunatumia file manager tunaona mafaili yote kirahisi lakini system ya iphones kwa kuwa haishirikiani vema kwenye kushare storage na apps huwa inakuwa kazi ngumu kuperuzi mafaili, shughuli inakuwa pevu zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi. unaweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android ukifika stationary unachomeka waya wa usb kwenye computer unaprint kazi haraka, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes na hapo inabidi anunue bando ili kudownload itunes, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

Iphone haina radio
919+p6SXzfL._AC_SL1500_.jpg

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. ukiwa na android hata kikifika kipindi cha uchaguzi, internet ikikatwa na tcra bado unaweza kuendelea kusikiliza radio.

Mipangilio ya muonekano imebanwa sana iphone
launch.jpg

Kwenye iphone kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa kanzu na android kwasababu kwenye android wanaruhusu kubadili launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako kuanzia muonekano na upangiliaji wa icons, kubadili styles za miandiko, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe actions, scrolling effects, lock screen customization, widgets, n.k. kuna vitu vichache kama widgets za homescreen viliongezewa kwenye iphone mwaka 2020 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo.

Iphone haina always on diplay
aod.jpeg

Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda ukitaka kuangalia muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana, Kuna tetesi matoleo yajayo ya iphones huenda wataweka hii ishu.

Iphone ni lazima utumie bando kuingiza app/game

njn.jpg

Kwenye iphone njia pekee ya kuingiza app ni kuzi download kwenye appstore kwa kutumia bando, huku android si lazima kudownload app kwenye playstore, mfano kama unahitaji app flani na huna bando, unaweza kwenda kwa mwenye hio app akakuhamishia file la app kwenye memory card au kwa usb cable, ukipata file unaingiza app bila hata bando. ukitaka ujue thamani ya hii feature chukulia kwamba app kama game ina gb 7 ambazo kifurushi cha data ni shilingi elf 10, kwenye iphone lazima wekundu wa msimbazi ukutoke ili ushushe app ila kwenye android hutalipia hata senti, lakini pia kama sehemu haina network nzuri itabidi usubirie muda mrefu mpaka app imalize kudownload na kama internet imekatwa itabidi utulie tu.

Iphone wanachelewa sana kuweka mahitaji ya wateja
hjk.PNG

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september na hapo bila milioni 2 huipati, Kwenye android haya mambo yapo toka kitambo sana. Pia Tukija kwenye widgets za homescreen iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo muda mrefu.

Huwezi kuseti ringtone ya muziki kwenye iphone
ghjn.PNG

Ili kuseti ringtone yoyote kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari na ni rahisi, kwenye iphone ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload apps za ziada., hii ndio sababu watumiaji wengi wa Iphones simu zikiita huwa zina mlio kama wa vingoma vya watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

Camera
ca.PNG

kamera zimeboreshwa sana kwa pande zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kamera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inajitahidi, nadhani hizi ishu za kamera kwa sasa tuzichukulie kawaida, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda tutarajie hata simu za elf 80 zikitoa picha kali mno.

Ulinzi
KSY-53-What_is_a_firewall__.jpg

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand kwamba wana simu yenye ulinzi kamili kuna kipindi walikataa kutoa ushirikiano kwenye kuifungue simu ya gaidi ila wataalam wakaichokonoa chapchap ikafunguka bila msaada wa kiwanda cha iphone, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, pia iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. nawakumbusha kwamba sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza password zako utaibiwa akaunti yako, n.k.

Uhuru / Demokrasia
hitl.PNG

Iphone akiamua kutoa kitu flani kwenye simu hahofii chochote kwasababu hana mshindani na wateja wake hawawezi kubisha, kwa vile wako peke yao hata wakitengeneza simu kwa laki 6 na wakaamua bei iwe milioni 4 hakuna wa kuwasumbua, hakuna uhindani hivyo wateja wanaburuzwa kukubali kila kitu kinachoamuliwa na kampuni, hebu vuta picha tu kwambaiphone aliamua atoe tundu la earphone ili tu awakamue wateja laki 4 za wireless earphone. Kwa upande wa android ushindani ni mkali kwa hio mteja anaheshimiwa Zaidi, simu flani ikiamua kutoa kitu flani basi wateja wanaokipenda watanunua simu nyingine, ushindani mkali unawanufaisha wateja maana makampuni ya simu yanazidisha ubunifu Zaidi ili kupata wateja na hii inapelekea bei ziwe fair kwa wateja.

Iphone hairuhusu emulators
sega.jpg

Kama vile ambvyo baadhi yetu tunavyopenda kusikiliza bongo fleva za zamani enzi hizo tukiwa watoto / vijana basi tupo watu ambao tumezimisi gemu tulizochezaga zamani miaka ya 90’s na 2000’s kipindi ambacho tulicheza playstation x, ps 2, psp, sega, n.k. Android imekuwa msaada mkubwa kwa kuruhusu emulators ambazo tunaweza kuchezea hizo games kwenye simu zetu bila kuwa sebuleni kwenye tv. Kwa upande wa iphones hawaruhusu emulators, hata zilizopo ni za kimchongo na hapo bado zina ubora mdogo. (point kutoka kwa chief - mkwawa)

Jail breaking (iphone) v/s Rooting (android)
root-vs-jailbreak-differences-between-modding-android-ios.1280x600.jpg

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.

………………………………………

Ohhh, nashusha pumzi maana vidole vimechoka kuandika, nawaombeni tu niishie hapa, mambo mapungufu ni mengi ila muda umenibana, yani huwezi amini mpaka leo Iphone haina kile kitaa cha rangi cha notification, Aiseee!!!.. mdebwedo ni mdebwedo tu hata uuzwe milioni 3 na nusu 😂😂
 
BEI
View attachment 2166316

Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.

MIPANGILIO YA MUONEKANO
View attachment 2166317

Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.

KUSETI RINGTONE
View attachment 2166320

Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

FILE MANAGEMENT
View attachment 2166322

huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

MULTI TASKING
View attachment 2166328

kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, Android unaweza kutumia calculator, kuandika message, kusoma pdf na kucheki video kwa mpigo, screen ikiwa imejigawanya katika vyumba.

SIMU KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA
View attachment 2166326

Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.

APPS
View attachment 2166329

Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.

FREE INTERNET
View attachment 2166352

Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

MEMORY CARD
View attachment 2166333

Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.

RADIO FM
View attachment 2166334

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.

JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.

KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337

hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.

ULINZI
View attachment 2166338

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada wa kampuni, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.

CAMERA
View attachment 2166341

kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.

IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.

ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.

Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachosha zaidi
Mimi situmii iPhone lakini je wanatumiaji wote hawa hawajui hilo?

Screenshot_2022-03-27-22-21-56-561_com.android.chrome.jpg
 
😂😂😂huachagi kitu fala wewe
ANDROID INAWEZA KUFANYA ZAIDI YA KITU KIMOJA KWA MPIGO (Multi tasking)
View attachment 2166328

kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, Android unaweza kutumia calculator, kuandika message, kusoma pdf na kucheki video kwa mpigo, screen ikiwa imejigawanya katika vyumba.

KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337

hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.

IPHONE IMEPIGWA GEPU REFU KWENYE APPS
View attachment 2166329

Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.

SIMU YA ANDROID YAWEZA KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA (Multi user)
View attachment 2166326

Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.

ANDROID UTATUMIA INTERNET BURE BILA BANDO
View attachment 2166352

Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

IPHONE HAINA MEMORY CARD
View attachment 2166333

Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.

BEI
View attachment 2166316

Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.

NI SHUGHULI PEVU KUPERUZI / KUHAMISHA MAFAILI YA IPHONE
View attachment 2166322

huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

IPHONE HAINA RADIO
View attachment 2166334

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.

MIPANGILIO YA MUONEKANO IMEBANWA SANA IPHONE
View attachment 2166317

Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.

IPHONE HAINA ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.

IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.

HUWEZI KUSETI RINGTONE UNAYOTAKA KWENYE IPHONE
View attachment 2166320

Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

CAMERA
View attachment 2166341

kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.

ULINZI
View attachment 2166338

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada wa kampuni, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.

JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.

Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachoshahua
 
bado vipo vingi sana mwanangu, nimechoka kutype, android kuna taa za notification huku unajua ni mesej ya fulani imeingia kwa kucheki rangi ya taa ya notifications.

IPHONE HAKUNA HII 😂😂😂
Kweli aisee samsung s7 edge yangu hutoa mwanga wa blue meseji ikiingia wakati simu ikiwa kwenye sleep,pia taa ya kijani hujulisha missed call,na blue bahari uashiria text za whatsap ..lakini pia nina iphone 12 pro max nilikuwa nalinganisha baadhi ya vitu kutoka kwenye uzi huu nkagundua ni kweli unayosema aisee🤣

Screenshot_20220327-224127_Gallery.jpg
 
Kweli aisee samsung s7 edge yangu hutoa mwanga wa blue meseji ikiingia wakati simu ikiwa kwenye sleep,pia taa ya kijani hujulisha missed call,na blue bahari uashiria text za whatsap ..lakini pia nina iphone 12 pro max nilikuwa nalinganisha baadhi ya vitu kutoka kwenye uzi huu nkagundua ni kweli unayosema aisee🤣

View attachment 2166424
Hii pcha umeipiga kwa iphone ya mchongo au umeamua kuwa sagia kuguni iphone🤣

ubora upo chini
 
Hii pcha umeipiga kwa iphone ya mchongo au 🤣 naona ubora unatia shaka sana
Nimeipiga na samsung s7 ambayo ndo nimekwambia inatoa vimwanga vya notification..sijaipiga na iphone,maana nsingeweza kwakuwa targeted ilikuwa yenyewe hiyo iphone so i had to take pic with samsung galaxy s7 edge na tena giza ndio limesababisha yote hayo
 
Back
Top Bottom