NAFUMUA MSHONO: Simu za iPhone ni mdebwedo, wanaozitumia ni watu wa kufuata mkumbo bila reasoning. Simu za Android ndio mpango mzima!

Navizia kama kutakuwa na xiaomi mi 12 ultra niidake, maana mi 11 ultra mwaka jana ilifunika karibia takataka nyingi kwenye camera(Dxomark na Gsmarena ni mashahidi wa hili).

Umesahau Iphone mpaka leo hawajafanikiwa kuiondoa ile notch, tetesi zinasema Iphone 14 itakuwa na punch hole. Hawa majamaa washukuru tu wana mboyoyo mingi.
 
1. Sasa nimegundua kuwa hujawahi kutumia iphone ama umeitumia zamani sana. iOS ilianza kuwa multi tasking kuanzia iOS 4.0 back in 2010.
Ikaja kuwa pure multitasking baada ya kuanza kutumia 64 bits processorsna ilipotoka iOS 6. It seems you are living in the past the future will never find you.

2. Ebu nitajia highend flagship phone ya android ambayo ina sehemu ya kuweka memory stick kwa sasa? Usinitajie flagship za zamani, nitajiw flagship za kuanzia 2021.

3. Saaa kama mpaka ukaangalie mitortorial, na bado kuna threads kibao za kuuliza na kulalamika kuwa wameshindwa kuroot humu which means wanazidi kukaza. Hiyo ni same road kama ilivyo iOS maana before jailbreaking was easy ila day after day ikafungwa mpaka now imefungwa kabisa. Android inaenda kuwa closed tu kama iOS ndio maana kila toleo rooting inazidi kuwa ngumu. Na nimekuuliza, mbona huongelei now android kulimit apps kuaccess baadhi ya folders za system? 🤣🤣

4. Sijaingia vichwani mwao ila ndivyo ilivyo. Nadra sana kumkuta mtu anayeafford kununua gari la mils 300 ukakuta amelipimp na kulibandika ma spoilers, ila sasa mwenye alteza sasa, amelibandika ma stickers, sijui spoilers, sijui takataka gani. Same hata kwenye simu. Watu wanaoafford kununua simu za dollar 800+ hawana hayo mambo ya customization.

5. Wanaoleta hizo battle ni watumiaji wa android, ni kama vile hawajiamini wanajifeel vizuri kwa kujicompare na iPhone.

6. Nishakujibu kuwa iOS ni multitasking wewe unapotosha watu sawa na wale wa vijiweni wanaosemaga iPhone kwanza apps zote zinauzwa 🤣🤣 kumbe hata kuitumia hajawahi.

7. Unajua, product za Apple watu wanazipenda sio kwa sifa moja, bali as a whole package. Apple ni mzuri wa kuchanganya design, performance, simplicity, ecosystem.
The result of both inakupa kitu safi kabisa.

Sasa unakuta wengine simu inasifa mbili, mfano ina kamera kali, ina storage kubwa lakini kwingine hovyo.
Samsung S22 itapata support kwa miaka minne na security patch kwa miaka mitano ka sikosei, Xiaomi 12 pro itapokea miaka mitatu na nahisi 12 ultra itapata zaidi ya hapo(kumbuka hiki ndio kigezo kikubwa cha watumiaji wa iphone kuwachapa watumiaji wa android).
 
1. Hata samsung s22 na nyingine high end android phones hazina eearphone jack. Kama kawaida uwa akianza iPhone anapondwa hadi na samsung wenyewe nao baadae wanafuata.
Aliacha kuweka charger akapondwa nao wakafuata.
2. Unasema huwezi kufanya multi tasking kwenye iPhone, mkuu umewahi kuitumia au unasema tu?
3 Kuhusu apps, hivi ni bora kuwa na nguo chache lakini za maana au kuwa na bag la nguo nyingi hata ambazo hazina maana yani ukiivaa ukajitazama kwenye kioo unaivua. Ndivyo playstore ilivyo. Ina apps nyingi ambazo unaistall unakuta haifanyi hata walichosema inafanya unaiondoa. Kwasababu ni rahisi kuweka app playstore wakati istore wanamchakato serious.
4. Mwendo wa kustream ndio maana kuna maspotify na stations ziko kwenye mtandao.
5. Kuhusu kujailbreak, hata android kila toleo anakaza nati ili simu iwe ngumu kuroot. Android 11 au 12 sio sawa na android 6 hata kuroot si kawaida au rahisi. Ipe miaka 3 mbele utaona atakavyokaza kabisa.
6. Shida mkuu unasahau kuwa iPhone anatoa simu ambazo ni highend tu, ni kwa miaka ya hivi karibuni ambapo ametoa simu midrange hizi SE. So ukicompare simu zake highend compare na bei ya samsung ya mwaka huo.
Pia hata midrange anaweka processor ya highend. Mfano SE ya mwaka huu ina A15 bionic chip ambayo ndiyo chip yenye nguvu kwa sasa na ndio iko kwenye iPhone 13.
Natumia android kwa sasa, ila iOS ni habari nyingine.
Jinsi inavyofanya kazi, ilivyo smooth, vitu vinainteract, ecosystem ya apple, yani safi kabisa.
You are really wasting your time.

Ukisoma bandiko lake mwanzo mpaka mwisho ni childish content.

Na most of them wanatumia either midrange au low end phones.

High end android phones hazina tofauti sana na iphone.
 
Mm sio iphone user na wala sijawahi kuzipenda ila mengi uliyoyataja apo yapo pia kwa android...mfano flagships nyingi za android sa hv hazina radio, hazina sd card expansion,hazina earphone jack(samsung wameenda mbali zaidi wametoa mpk kwny midranges zao), price ya Iphone 13 pro max na S22 ultra they match toe to toe,pia nimetumia highends nyingi za samsung hazina hzo radio...ifike mahali kila mtu abaki na OS yake anayoiamini sio hz useless attacks zisizo na msingi!

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
Ukiona hivyo ujue anatumua tecno. Angetumia s22 ultra asingeongea huu utoto.
 
Watu weusi sisi tuna shida sana..
Mngejua Samsung wanaingiza hela ndefu kwa kufanya biashara na Apple kuliko kuuza hizo simu zao..

80% ya hardware za Apple products anauziwa na Samsung..

All in all simu ni simu tu, kila mtu na mahitaji yake, ila hua nawaonea(ga) huruma sana baadhi ya watumiaji wa iPhone wanavyo hangaika, nakubaliana na mtoa mada wengi wanatumia kwa mikumbo..
Weusi wamefanya nini? Huwa nawashangaa sana watu kama wewe kidogo tu weusi this weusi that.

Hii battle ya android(samsung) v Ios inaanzia kwa watasha huko huko sisi huku hatugusi hata robo kwa hilo.
 
ANDROID INAWEZA KUFANYA ZAIDI YA KITU KIMOJA KWA MPIGO (Multi tasking)
View attachment 2166328

kufanya shughuli Zaidi ya moja kwa urahisi ni kitu muhimu ambacho hakipo kwenye iphone, Android unaweza kutumia calculator, kuandika message, kusoma pdf na kucheki video kwa mpigo, screen ikiwa imejigawanya katika vyumba.

KWENYE IPHONE HAKUNA TUNDU LA KUCHOMEKA EARPHONES
View attachment 2166337

hakika huu uamuzi haukuwa na maana, ni uamuzi uliofanyika kibiashara zaidi bila kujali mahitaji ya wateja, kitu walichofanya ni kulazimisha wateja kununua wireless earphone zao au kama watahitaji kutumia earphone za waya basi wanunue kiunganishi chao cha ziada. Kwa android uchagyzi ni wako uamue kutumia za waya au wireless, binafsi headphone za waya zimewahi kunisaidia simu ikianguka isigonge sakafu na pia kuna Rafiki yangu alitaka kuibiwa simu, ilipovutwa alistuka mwizi akakimbia.

IPHONE IMEPIGWA GEPU REFU KWENYE APPS
View attachment 2166329

Sio siri wala kitu cha kubishana, Android kuna apps nyingi sana kuliko Iphone, Sababu kuu ni kwamba ili kuweka app kwenye playstore ya android gharama yake ni elf 50 mara moja tu lakini kwa upande wa iphones kuweka app kwenye apple store ni laki 2 unalipia kila mwaka, pia kwenye android unaweza kudownload na ku install apps ambazo hazipo playstore.

SIMU YA ANDROID YAWEZA KUTUMIKA NA MTU ZAIDI YA MOJA (Multi user)
View attachment 2166326

Hii inaitwa multiple user, simu inaweza kutumika na Zaidi ya mtu moja bila kuingiliana taarifa, mfano unaweza kumtengenezea account mtoto wako awe anachezea game bila yeye kuona message zako, picha / video zako, apps zako, mawasiliano yako, n.k, utampa simu aitumie bila wasi wasi. simu muhimu ikipigwa unaweza kuseti iite ili akuletee, ukimaliza maongezi unampa simu akaendelee. Unaweza kutengeneza hata accounts 4 za watu tofauti zitumike ofisini. Kwa iphone hawana hii.

ANDROID UTATUMIA INTERNET BURE BILA BANDO
View attachment 2166352

Hapa ndo napopenda aisee! mtu wa iphone atajibana bana anunue kifurushi cha GB 2 kwa wiki, hizo mambo za kujibana hazipo huku android kwenye apps kibao kama ha tunnel, napster, n.k. unacheza tu na settings unaanza kuserereka, unaweza kushusha hata gb 20 kwa siku na wala isiwe habari lakini kwa iphone itabidi ununue kifurushi cha elf 30 ili upate hizo gb, Nikiri kusema kwamba hili si tatizo kwa wale wanaonunuaga iphone matoleo mapya pale mlimani city mtu haoni taabu kulipia milioni 3 na hio simu anaiweka mfukoni, ishu ni hawa ambao wanaokwepa panga la bei kali kwa kununua iphones za kimchongo zilizotumika (refurbished) tena matoleo yaliyochuja, hawa wengi wao wana changamoto za kiuchumi kwa hio hata mabando ni ya kutumia kwa machale.

IPHONE HAINA MEMORY CARD
View attachment 2166333

Iphones hazina memory card, Iphone inaweza kuwa na gb 64 na ikajaa ikaleta changamoto kuongeza nafasi ya ziada maana hakuna tundu la memory card , Lakini pia simu inaweza kuwa na gb 500 lakini haiondoi umuhimu wa Memory card maana funguo mbili za gari ni bora kuliko moja, simu yako inaweza kudondoka, kuungua, kupata hitilafu, n.k ikashindwa hata kuwaka ukapoteza kila kitu, ila kama ilikuwa na memory card, hata ikidondoka utachomoa memory card utakuta mafaili yako, hata ukiwa katika mazingira ya kuchukuliwa simu yako, unaweza kutoa memory kadi yako chap chap ukaiacha simu.

BEI
View attachment 2166316

Bei kali ya simu ya iphones ni kwa sababu ya kampuni ya apple kucheza na akili za watu kwenye branding, Kwenye swala zima la bei wanatumia mbinu inaitwa “prestige pricing” kwa mfano mwepesi ni kwenda duka la nguo ukakuta kuna t shirt zenye ubora wa hali ya juu zinauzwa elf 20 lakini nyingine zina ubora wa kati zinauzwa elf 60, ukiuliza kwanini unaambiwa kwasababu ina nembo ya Nike, Gucci, n.k. wanacheza na saikolojia ya mtu ajione yupo juu kwa kununua bidhaa hio, Kwa hapa bongo watu wachache sana wananunua iphones pale mlimani city, wengi hawana pesa kwa hio wananunua iphones za mchongo zilizotumika (refurbished), wengi zaidi hupendelea matoleo ya nyuma zaidi ili kupunguza makali ya bei (umelipenda boga kwanini uchukie maua yake ?), Kwa upande wa Android huku unaenda kuchukua mzigo wako mpya dukani kulingana na bajeti yako, utaamua wewe ununue daraja la juu “Flagship” mfano Samsung galaxy s22, daraja la pili Mid range mfano OnePlus 8T, daraja la bajeti hapa kibongo bongo kampuni ya Transission holding imekamata soko kwa kutengeneza simu zote za Tecno, Infinix na Itel.

NI SHUGHULI PEVU KUPERUZI / KUHAMISHA MAFAILI YA IPHONE
View attachment 2166322

huku android tunatumia file managers tunaona mafaili yote kirahisi kwenye folders lakini system ya iphones haishirikiani kwenye kushare storage na apps kirahisi hivyo inakuwa ngumu kuperuzi mafaili yako, Hali inakuwa mbaya zaidi unapotaka kuhamisha mafaili kwenye iphone kwa computer / laptop, yani inabidi uwe na program ya itunes kwenye pc ili ufanikishe hili zoezi, Mimi naweza kuwa na pdf file kwenye simu ya android nikifika stationary nachomeka fasta tu naprint file, kwa upande wa mwenye iphone inabidi ambembeleze mwenye stationary aingize program ya itunes, na hapo inabidi anunue bando ili kudownload hio software, yani hadi amalize hii shughuli anakuwa ametumia muda mwingi na kagharamika kununua bando.

IPHONE HAINA RADIO
View attachment 2166334

Simu za Iphone hazina radio, hapa labda uwe unatumia bando kusikiliza radio za online. Nikiwa na android yangu hata kile kipindi cha uchaguzi internet ilivyokatwa niliweza kuendelea kusikiliza vipindi vya redio navyovipenda.

MIPANGILIO YA MUONEKANO IMEBANWA SANA IPHONE
View attachment 2166317

Kwenye iphones kwenye swala la mipangilio ya muonekano (User inteferace customization) wamepigwa gepu refu sana kwasababu android unaweza kuweka launcher, hii launcher itakuruhusu kupangilia muonekano mzima wa simu yako, utaweza kujipangilia icon kwa kuweka unazotaka wewe, kuzifinya na kuzitanua, n.k kucheza na elements zozote utakavyo kwenye home screen, kuficha apps kirahisi kwenye home screen, kuseti mitindo ya app drawer, kuseti gestures, kucheza na swipe commands, scrolling effects, lock screen customization, n.k. kuna vitu vichache kama widgets vimeongezewa kwenye iphone mwaka 2020 toleo a ios 14 lakini haya mambo yalikuwepo android toka kitambo, ajabu ni kwamba hapo zamani watumiaji wa iphones walikuwa wanadai wdgets za android zilikuwa hazina maana ila walipowekwa kwenye iphones wakaanza kuzisifia, kwa hakika sizitaki mbivu hizi.

IPHONE HAINA ALWAYS ON DIPLAY
View attachment 2166345
Kwenye simu za android utaweza kuzima screen ya simu yako ila itaendelea kuonyesha vitu muhimu kama saa, notifications, n.k. Hutakuwa na haja ya kuwasha screen ya simu kila muda. Huna haja ya kuhofia matumizi ya battery kwa sababu hii feature inatumika kwenye vioo vya kisasa vya Amoled ambavyo vinatumia charge kidogo sana ukitumia hii feature, Hadi sasa hii feature muhimu haipo kwenye iphones officially.

IPHONE WANACHELEWA SANA KUWEKA MAHITAJI YA WATEJA
View attachment 2166343

Huwezi amini kwamba iphone ya kwanza kuwa na line 2 ilitoka mwaka 2018 september, Tukija kwenye widgets za homescreen, iphone iliziweka mwaka 2020 wakati android zipo kitambo sana.

HUWEZI KUSETI RINGTONE UNAYOTAKA KWENYE IPHONE
View attachment 2166320

Ili kuseti ringtone yako kwenye android ni kitu ambacho kipo tayari, utaweza kuweka mziki wowote uwe ringtome. kwenye iphones hii kitu hakuna, ni mpaka uwe mtundu mtundu ufanye kudownload app ya garageband, uingize mziki kwenye app, ufanye ku save ndio utaweza kuset hio ringtone, shida yote ya nini hii jamani? Hii ndio sababu wengi simu zao zina ringtone ile inalia kama vingoma vya Watoto, tulu tutu tu tu tu tu tu, ndi ndi ndi ndi.

CAMERA
View attachment 2166341

kamera zimeboreshwa sana kwa simu zote, hiki kigezo kwa sasa hakina uzito sana kama zamani picha zilipokuwa na ubora mdogo, Nimetoka kucheki simu zenye kanera kali nimeona inayokimbiza ni android pixel 6 pro, ila nimecheki ubora wa picha za iphone 13 pro max nimeona nayo inatoa picha kali tu, hizi ishu za kamera nadhani kwa sasa zipewe kigezo chepesi maana teknolojia ya kamera imekuwa mno, hata simu za laki 2 siku hizi mtu anakutumia picha safi tu ambayo ina ubora standard si haba, kadri miaka inavyoenda sitashangaa simu za elf 80 zikitoa picha kali sana.

ULINZI
View attachment 2166338

Hakuna system ambayo haipenyeki, ndio maana hata iphone wanao jibrand ni simu yenye ulinzi kamili walipoombwa kiroho safi waifungue wenyewe simu ya gaidi ila wakakataa, wataalam wakaingia kazini wakaifungua chapchap bila msaada, hata I-cloud nayo ilidukuliwa zikavuja picha tupu kibao za mastaa, iphone hadi leo watu wanai jailbreak, n.k.. kwa iphone naweza kusema ulinzi wake umezidi ulinzi wa android kwa asilimia kadhaa ila sio kwamba ni ulinzi kamilifu. Pia nawakumbusha sehemu dhaifu kwenye ulinzi wa kifaa huwa ni mtumiaji, iwe ni iphone au android haiwezi kukuzuia kutuma hela kwa namba ile, ukiingia ukurasa feki wa facebook ukaingiza nywila zako utadukuliwa tu, n.k.

JAIL BREAKING (IPHONE) v/s ROOTING (ANDROID)
View attachment 2166335

Jail breaking kwenye iphones itakuruhusu kufanya mambo mengi ambayo tayari yapo kwenye android kwa mfano customization, kwa upande wa rooting inayofanyika android unapata full controll ya kucheza na system kadri unavyotaka.

Ohhh mambo ni mengi sana jamani, wacha niishie hapa nisije wachosha zaidi

Mult tasking
Unaandika sms huku unafanya hesabu kwa calculator huku unaangalia video huku unasoma PDF.....
I reserve my comment

No headphone jack
Hii ndio habari ya dunia kwa sasa sema ni vile haufahamu umezoea kutumia simu za kichovu
Simu zote za kampuni nguli kwenye Flagship zao wamemfuata Apple hawana hizo takata za mashimo

Wingi wa Apps
Tatizo huwa sio wingi wa App bali ni UBORA wa Apps
Appstore kuna apps zote MUHIMU na BORA Duniani
Playstore kuna app muhimu na mataka taka kibao

Multi user
Simu ni a very private thing, huu ushamba wa simu moja kutumia ukoo mzima ni USHAMBA..... not a big deal

Free internet
Unasifia UHALIFU hadharani kwamba ni sifa ya simu?
Huo ni udhaifu wa Simu na Os kwamba zina ruhusu watu kufanya uhalifu

No Memory card
Tunarudi pale pale, hii ni kutokana na kutumia low budget phones
Flagship zote za kibabe hazina hiyo takataka zimemfuata Apple

Bei ghali
Bado tupo pale pale, swala la bei ghali ni kutokana na level zako za kipato na simu unayotumia
Iphone kwa kiasi kikubwa wanatengeneza High-end phone ambazo zipo daraja moja na Flagship za manguli wa Android phones na bei wakati mwingine iphone anasubiri

Files
Huo ugumu unao usemea ni upi mkuu
Unaweza kutuma na kupokea file lolote na ukalifungua kwa Whatsap, Telegram, email, Messenger, Xender nk

No Radio Fm
Tupo pale pale
Flagship zote za kibabe zimemfuata Iphone hazina FM Radio

User interface
Haya mambo ya “kitoto kitoto” hayana nafasi kwenye simu classic

Always on
Watumiaji wa iphone muda wanaangalia kwenye saa ya mkononi sio unataka kuangalia saa unachomoa lisimu mfukoni kuangalia eti saa ngapi
Ikitokea ulazima wa kutumia simu si unakandamiza tu home button

Ringtones
Aliyekudanganya huwezi kuweka ringtones unazotaka ni nani?

Jailbrake
Ukiona unahangaika na jailbrake ujue iphone sio kaliba yako
Kanunue Tecno

Nimejibu kama mtani wa jadi
 
1648487994221.png
 
mi situmii iphone wala sitaki kuiona mbele yangu lakini kuna fact lazima tuzikubali.

1.iphone ndo simu pekee duniani ambayo huwezi badili imei.

2.ios iko optimized kuliko android, hili lazima tulikubali maana ukiachana na premium hardware, 2gb ram ya iphone 6s. ina run ios 15.4 very smooth.

mtoa mada amekurupuka, au ufahamu mdogo.
 
Mult tasking
Unaandika sms huku unafanya hesabu kwa calculator huku unaangalia video huku unasoma PDF.....
I reserve my comment

No headphone jack
Hii ndio habari ya dunia kwa sasa sema ni vile haufahamu umezoea kutumia simu za kichovu
Simu zote za kampuni nguli kwenye Flagship zao wamemfuata Apple hawana hizo takata za mashimo

Wingi wa Apps
Tatizo huwa sio wingi wa App bali ni UBORA wa Apps
Appstore kuna apps zote MUHIMU na BORA Duniani
Playstore kuna app muhimu na mataka taka kibao

Multi user
Simu ni a very private thing, huu ushamba wa simu moja kutumia ukoo mzima ni USHAMBA..... not a big deal

Free internet
Unasifia UHALIFU hadharani kwamba ni sifa ya simu?
Huo ni udhaifu wa Simu na Os kwamba zina ruhusu watu kufanya uhalifu

No Memory card
Tunarudi pale pale, hii ni kutokana na kutumia low budget phones
Flagship zote za kibabe hazina hiyo takataka zimemfuata Apple

Bei ghali
Bado tupo pale pale, swala la bei ghali ni kutokana na level zako za kipato na simu unayotumia
Iphone kwa kiasi kikubwa wanatengeneza High-end phone ambazo zipo daraja moja na Flagship za manguli wa Android phones na bei wakati mwingine iphone anasubiri

Files
Huo ugumu unao usemea ni upi mkuu
Unaweza kutuma na kupokea file lolote na ukalifungua kwa Whatsap, Telegram, email, Messenger, Xender nk

No Radio Fm
Tupo pale pale
Flagship zote za kibabe zimemfuata Iphone hazina FM Radio

User interface
Haya mambo ya “kitoto kitoto” hayana nafasi kwenye simu classic

Always on
Watumiaji wa iphone muda wanaangalia kwenye saa ya mkononi sio unataka kuangalia saa unachomoa lisimu mfukoni kuangalia eti saa ngapi
Ikitokea ulazima wa kutumia simu si unakandamiza tu home button

Ringtones
Aliyekudanganya huwezi kuweka ringtones unazotaka ni nani?

Jailbrake
Ukiona unahangaika na jailbrake ujue iphone sio kaliba yako
Kanunue Tecno

Nimejibu kama mtani wa jadi
You have spoken my mind.
 
Samsung S22 itapata support kwa miaka minne na security patch kwa miaka mitano ka sikosei, Xiaomi 12 pro itapokea miaka mitatu na nahisi 12 ultra itapata zaidi ya hapo(kumbuka hiki ndio kigezo kikubwa cha watumiaji wa iphone kuwachapa watumiaji wa android).
Watumiaji wa iPhone ni the entire ecosystem ndio inawafunga.
Kuna mtu alisema Apple I'm built this amazing product, and built services and other products around this amazing products.
Apple amekuwa kizipa support simu zake kwa miaka mingi, kama Samsung nao wameanza basi heko kwao.
 
Mshkaji wangu ana iphone 6s

Nadiriki kusema sijashuhudia simu inayoisha chaji kama hii ya jamaa.
 
Back
Top Bottom