Halo wakuu, kama heading inavyosema hapo, nina kuku wa kienyeji kama 150 hv, ambao ninawafuga nusu huria, yaan wako ndani ya fensi, so nawapa chakula ila pia wanajitafutia ndani ya huo uzio, kuna mambo yamejitokeza ambayo yananifanya nashindwa kuwaandalia chakula chenye ule mchanganyiko wote wa chakula( mf damu, alizeti dagaa, mifupa nk) hivyo ninaomba ushauri wa kufanya ili wasikose virutubisho muhimu. Ninaweza kupata kwa urahis pumba za mahindi na lukina, je kuna kitu kingine hata viwili muhimu zaidi naweza kuchanganya na hivyo hapo juu ili at least wasiweze kukosa lishe bora kabisa? Au nifanyeje? Bado sijafikia hatua ya kuamua kuuza kuku. Ahsanten