Nafikiria sana CCM ikishindwa watu wake, hasa viongozi wake

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,930
3,803
Nimefungua redio kusikiliza matokeo nasikia CCM imepoteza Uchaguzi Mkuu na sehemu nyingi imeshindwa kutetea ubunge,ghafla matangazo yameisha inayofuata ni nafasi ya Uraisi nayo CCM imepoteza.

Shangwe na vifijo nchi nzima ni zaidi ya siku kuu unasikia vituo vya redio vya kila aina vikiuponda utawala wa CCM, maafande nao wanasikika na kuonekana vituoni wakiwa wamefurahi na ni kama wamepata likizo ya muda mrefu baada ya kazi ngumu.

Inatilisha huruma sana, unajua binadamu tuna hulka za kufanya kitu haswa maamuzi magumu baadae ukaingia simanzi na kuwafikiria wale uliowatolea yale maamuzi.

CCM chama chenu kinaelekea kushindwa na kwa kweli ni maangamizo ya karne kwa Chama kikongwe kupumzishwa na sio kupumzishwa bali kushindwa.

Nafikiria sana kama zile ofisi na bendera zake zitamudu kuwepo muda mrefu mitaani, naona kama imekuwa kiama kwao na ndio mwisho wao wa kusikika tena, walio wengi wao hawatoweza kuvaa tena nguo zao zenye Jembe na nyundo.

Naelewa aibu itatawala kwenye nyuso zao,yale majigambo ya kuwatisha na kuogopewa na wananchi yatakuwa hawanayo tena,sijui wataishi ishi vipi, maana tunajuana na ubaya na vizingiti vyao bado makovu hayajapotea,japo tumepona kwa ghafla, maana kuanguka kwa CCM ni tiba mbadala ya maendeleo ya Mtanzania.
 
Amini amini nakwambia, Hii ndo itakuwa hali ya hapo November 2020 wakati wa utangazaji wa matokeo ya uchaguzi!

Historia kubwa sana inaenda kuandikwa mwaka huu Tanzania. Dunia itashangaa, Africa Itashangaa na itakuwa furaha Kuu Tanzania!
 
Viwanja vyote vya mipira tunavirudisha serikali, majengo yote yaliyomilikishwa chamani yanarudi serikalini, sheria zote kandamizi zinatupiliwa mbali, katiba mpya na tume mpya kipaumbele cha kwanza, wahalifu wote wa awamu za nyuma mahakamani, wasiojulikana tunawanywa supu, itakuwa ni zaidi ya kushinda Biko ya milion300!
 
Mzee mkapa kasepa kabla dhahama haijamkuta.
 
Amini amini nakwambia, Hii ndo itakuwa hali ya hapo November 2020 wakati wa utangazaji wa matokeo ya uchaguzi!

Historia kubwa sana inaenda kuandikwa mwaka huu Tanzania. Dunia itashangaa, Africa Itashangaa na itakuwa furaha Kuu Tanzania!
Cdm ni hivi hamuwezi kishinda uchaguzi huu kama mlindwa 2015 Lindi mlipoungana mnajidanyana . Tuwaambie tu ukweli Tanzania kuongozwa na upinzani bado sana!
 
Amini amini nakwambia, Hii ndo itakuwa hali ya hapo November 2020 wakati wa utangazaji wa matokeo ya uchaguzi!

Historia kubwa sana inaenda kuandikwa mwaka huu Tanzania. Dunia itashangaa, Africa Itashangaa na itakuwa furaha Kuu Tanzania!
Kwa wagombea Aina ya Salum Mwalimu na Lissu ndo waende ikulu Hawa? Hiyo labda wakapange ikulu kwa baba mkwe wao Kama walivyofanya pale ufipa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Kwa wagombea Aina ya Salum Mwalimu na Lissu ndo waende ikulu Hawa? Hiyo labda wakapange ikulu kwa baba mkwe wao Kama walivyofanya pale ufipa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Makosa makubwa sana kumpagisha mtu nyumba kwa muda mrefu siku ukitaka kumtoa anaweza kukupiga ngumi anafikiri nyumba yake hata Lissu tunampa mkataba wa miaka mitano tu itategemea tukipendezewa na yeye akikubali tunaweza kumuongezea mitano mingine sio lazima ccm ikulu sio mali ya lumumba acha ushamba
 
Back
Top Bottom