Nafikiria kufungua Office kubwa ya upelelezi, naomba ushauri

Habari za mchana wana bodi.

Kwa jinsi mambo yalivyo magumu huku mtaani hasa biashara nimefikilia nimeona nitumie mtaji wangu wote kufungua Ofice kubwa ya upelelezi yaani niwe na leseni ya Mpelelezi binafsi.

Sasa sijajua kama sheria ya nchi hii itaniruhusu kwa anaejua tafadhari anisaidie hapo kwani najua kupitia wazo langu nitaajiri vijana wengi.

Katika jukumu lako hilo jipya hakikisha tu una namba zote za Waganga wa Kienyeji hapa nchini na pia uwe na tabia za Kichawi chawi hiyo Kazi utaimudu zaidi ya hapo usije ukashangaa hata kabla hujaanza hilo jukumu ukawa umeshapata tiketi yako ya kuungana na " waliotutangulia " kwa Ndugu Godi.
 
Huo mtaji ni bora ukafanye biashara ya kuuza simenti ya Dangote... Zama hizi za simu wtu wanafanya udetective wenyewe. Wananasa wagoni wao na wanaenda kwenye tukio kulianzisha wenyewe. Siku hizi haina haja sana ya kufuatilia mgoni wako thru private detective...
 
Hapo ulipoanza kuleta hii topic tu! watu washaanza kukufanyia upelelezi hadi siku ya kufa.. Chunga sana lengo lako.
 
Huo mtaji ni bora ukafanye biashara ya kuuza simenti ya Dangote... Zama hizi za simu wtu wanafanya udetective wenyewe. Wananasa wagoni wao na wanaenda kwenye tukio kulianzisha wenyewe. Siku hizi haina haja sana ya kufuatilia mgoni wako thru private detective...
si lazima ufanye za kukamata ugoni,kuna upelelezi unahusisha pia na mambo ya biashara ,siasa ,mfano mimi mfanyabiashara naona mpinzani wangu wa biashara anapeta kuliko mimi,nini siri ya urembo,anauza wapi mzigo na kwa bei gani,anatumia logistick zipi,anatoa wapi mzigo na kwa bei gani,anatumia mbinu zipi kupata tenda serikalini etc.
Kama kisiasa mshindani wako ana scandal zipi,background yake etc,vyanzo vyake vya fedha halali ama haramu,etc.

Vitu kama hivyo,waweza anzisha private agency kwa kazi kama hizo na ukatengeza faranga bila wasiwasi muhimu uwe na vijana mahili kwa kazi kama hizo za kunusanusa
 
Your concept is good...
 
Habari za mchana wana bodi.

Kwa jinsi mambo yalivyo magumu huku mtaani hasa biashara nimefikilia nimeona nitumie mtaji wangu wote kufungua Ofice kubwa ya upelelezi yaani niwe na leseni ya Mpelelezi binafsi.

Sasa sijajua kama sheria ya nchi hii itaniruhusu kwa anaejua tafadhari anisaidie hapo kwani najua kupitia wazo langu nitaajiri vijana wengi.

Ukipepeleza maisha binafsi ya watu utapiga pesa
 
Mkuu ukipata shavu naomba uniajiri niko vizuri kwenye hyo sector
Huwa Nakasirika Sana kusikia mtu anaomba kazi huku anavigezo vyote vya kujiajili... Hivi Elimu yetu ni kwa ajili ya kuajiliwa tu? yaani Mtu akishindwa Maisha ndio anajiajili mwenyewe na aliyesoma anaajiliwa na asiyesoma nini maana yake hii?????????????????
 
Mkuu sasa asiponiajiri hyo kazi atafanya mwenyew. Jamani hata anaejiajiri anaajiri na watu wengine. Mfano nikijiajir ntakua mwenyew kiongozi si natafuta wasaidizi.
 
Bonge la wazo, usikatishwe Tamaa wewe amini unaweza. Kusoma Ni formalities tu, asikutishe mtu Shule watu wana kariri. Kuwa wewe utamudu
 
Kuna vitu hutaki kuelewa, unakuwa mbishi tu hujui wanaokuambia wanajua zaidi yako,,, ipo hiv ndugu , yani kwa thread hii tu watu walishafuatilia wanajua ulizaliwa wap? Tarehe ngapi? Wazaz wako ni kina na? Marafiki zako ni kina nan?? Na mengine mengi sana , wanamjua hata mke au dem wako. Kuna mambo magumu mno hasa kwenye nchi hizi ambazo zilikuwa na mifumo ya kijamaa.. Nakutakia kila la kheri ndugu na usinisahau kwenye ajira hata ya kulinda ofisi, japo mimi nitatumia upinde na mishale ya kipare ni hatar bora risasi inaua haraka!!!!
 
Habari za mchana wana bodi.

Kwa jinsi mambo yalivyo magumu huku mtaani hasa biashara nimefikilia nimeona nitumie mtaji wangu wote kufungua Ofice kubwa ya upelelezi yaani niwe na leseni ya Mpelelezi binafsi.

Sasa sijajua kama sheria ya nchi hii itaniruhusu kwa anaejua tafadhari anisaidie hapo kwani najua kupitia wazo langu nitaajiri vijana wengi.
huwezi kupata hiyo leseni
unatakiwa kuwa ulifanya kazi ya upelelezi si chini ya miaka 15,ukiwa na cheo si chini ya SSP kwenda juu.aidha umestaafu au umeacha,cv isiwe na chambe chambe za uhalifu
Labda kama unataka kuwa informer sawa
 
Back
Top Bottom