Nafikiria kuanzisha NGO ya kuwasaidia walioshikiliwa korokoroni, mahabusu na wafungwa nchini

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,406
2,000
Habarini,

Nimefikiria sana jinsi watu wanavyoteseka kwa kukosa dhamana wakiwa polisi na mahabusu na pia wafungwa waliofungwa kwa kuonewa au wanaocheleweshewa kesi zao pasipo sababu za msingi.

Pia kuna ambao ni wagonjwa hawana msaada kabisa hasa linapokuja kwa maswala ya matibabu.

Kuna ambao wanakosa msaada wa kisheria hata kuandaa hati za rufaa hawawezi.

Wengine hawana mavazi ya kujistili kiasi kwamba wanatia huruma.

Wengine wanaachiwa kwa rufaa au kumaliza vifungo bado wanakosa hata nauli za kurudia kwao.

Na kikubwa ninachofikiria ni kuwawezesha wale walioachiwa magerezani wenyekuwa na mwenendo mzuri na ujuzi ili kuwawezesha baada ya kuwafundisha nini cha kufanya na wao kufaulu vigezo husika eg. nidhamu.

Kwa kuanzia nimeanza kutoa nguo zangu,viatu,sabuni,dhaman(kwa dhamana za ahadi),n.k

Karibuni kwa maoni!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom