Nafikiria kuanzisha kampuni binafsi ya upelelezi, je hii inawezekana kwa hapa Tanzania?

sheria inaruhisu kabisa...kama una nia jipange na usirudi nyuma....zipo 2 na zinafanya kazi na idara ya usalama...nakutajia moja tuu...dirty informer..... nkuna ngoma zinawashindaga polisi..... skills na technology..
 
kwa KATIBA hii, utanyimwa ushirikiano na hawa jamaa. mara utakataliwa na hakimu ili mladi tu wao ndio wanaohusika. kwani ujifunzi wanavyukiuka KATIBA kwa MIKUTANO ya VYAMA vya upinzani?
 
Hakuna uwezekana huo kbs kwakuwa kampuni yako itakua inatoa majibu ya kweli yasiyo na kupepesa macho kitu ambacho ni sumu ndani ya chama tawala, jiulize hao usalama wetu wanskuaga wapi mpaka yukio litokee iundwe tume? Soko limeungua hadi leo kimyaaa kama vile wananchi hatutaki kujua kilichotokea. Hii ni nchi ya ujanja ujanja kufanya kitu kamili kama unavyowaza haiwezekani.
 
Sheria zinaruhusu lakini utekelezaji wake utakufa mapema!
Labda uchunguzi wako ujikite kupeleleza mikutano ya chadema ndo utadumu!

Kwasababu uhalifu mwingi una mkono wa ndani, aliyeko ndani anakujua na wewe!
Aliyeko ndani akijua atakusanua na kwasababu anakujua upo,

anawambia wajuba KACHOMOENI betri na Ikiwezekana na ofisi yako itachomwa!

Uharifu mwingi una mkono wa ndani! Ndiyo maana ukitaka kuudhibiti ujambazi piga mkwara sana ndani kuwatimua! Uone kama ujambazi utatokea
Hapo ungemtaja mzee baba late Pombe 😃!.
 
Mkuu nadhani inawezakana, sababu Private investigator wewe hautaingiliana na Police moja kwa moja kwamba uingilie kesi zao za kiupelelezi. Unawateja wako, mtu Akitaka huduma ufanye upepelezi ndio utapeleleza .
Sasa Sioni sababu ya kushindikana Hilo, Private investigator wanadeal na Mambo mengi sio kesi za kipolisi tu.

Kwa wenzetu hata Nikija nikisema nataka ufanye background check ya mtu fulani Kama private investigator hapo wewe ndo utahusika. Police hawana huduma za background check.

Naona Ni Idea nzuri, ifanye Kazi. wateja Utapata.
 
sheria inaruhisu kabisa...kama una nia jipange na usirudi nyuma....zipo 2 na zinafanya kazi na idara ya usalama...nakutajia moja tuu...dirty informer..... nkuna ngoma zinawashindaga polisi..... skills na technology..
Ofisi zao zipo wapi?
 
Mkuu nadhani inawezakana, sababu Private investigator wewe hautaingiliana na Police moja kwa moja kwamba uingilie kesi zao za kiupelelezi. Unawateja wako, mtu Akitaka huduma ufanye upepelezi ndio utapeleleza .
Sasa Sioni sababu ya kushindikana Hilo, Private investigator wanadeal na Mambo mengi sio kesi za kipolisi tu.

Kwa wenzetu hata Nikija nikisema nataka ufanye background check ya mtu fulani Kama private investigator hapo wewe ndo utahusika. Police hawana huduma za background check.

Naona Ni Idea nzuri, ifanye Kazi. wateja Utapata.
Shukurani mkuu
 
Back
Top Bottom