Nafikiria kuanzisha kampuni binafsi ya upelelezi, je hii inawezekana kwa hapa Tanzania?

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau,

Nimekuwa nikawaza mda mrefu kufungua kampuni binafsi ya kufanya upelelezi na kutoa ulinzi wa VIP's yaani wale watu maarufu na familia zao kama Mo-Dewji, Diamond n.k

Kampuni yangu pia itahusika katika kufanya upelelezi kwa watu binafsi na serikali na kukabidhi repoti kwa wateja wangu.

Mfano hivi karibuni kwenye suala la Hamza, kuungua kwa soko na mambo mengine mengi ambayo Serikali imekuwa ikiangaika kuunda tume za kuchunguza ambazo zinaonyesha zinachelewa kutoa majibu kwa wakati Serikali inaweza kuipa kazi kampuni na kushughulikia suala hilo fasta na kutoa majibu.

Wasiwasi: Je ili suala linawezekana kwa hapa Tanzania?
 
Sheria zinaruhusu lakini utekelezaji wake utakufa mapema!

Labda uchunguzi wako ujikite kupeleleza mikutano ya chadema ndo utadumu!

Kwasababu uhalifu mwingi una mkono wa ndani, aliyeko ndani anakujua na wewe!
Aliyeko ndani akijua atakusanua na kwasababu anakujua upo,

anawambia wajuba KACHOMOENI betri na Ikiwezekana na ofisi yako itachomwa!

Uharifu mwingi una mkono wa ndani! Ndiyo maana ukitaka kuudhibiti ujambazi piga mkwara sana ndani kuwatimua! Uone kama ujambazi utatokea
 
Kwa nchi za Africa ni ngumu kulikubali wazo hili maana serikali za uongo ndio zinaongoza nchi na viongozi wote karibia ni matapeli na hawapendi kusikia ukweli.

Hivyo wazo hili halitapata nafasi na unaweza kufunguliwa mashtaka kwa kupeleka wazo tu
Kuna sheria inakataza?
 
Linawezekana kabisa, zipo kampuni ambazo zimejikita katika ukusanyaji wa taarifa hasa katika nyanja za kibiashara, mfano muwekezaji akitaka kuwekeza kwenye eneo fulani anawapa tenda kampuni ya upelelezi inaanza kumkusanyia data zote muhimu za wazi na nyeti. Hii inawezekana!

Ila unayotaka wewe ni ngumu labda upewe mkataba na Serikali ufanye ushushushu kwa niaba yao,mfano mzuri upo yapo makampuni mbalimbali yanayomilikiwa na Idara za Usalama.
 
Back
Top Bottom