Nafikiri kupanda kwa gharama za mawasiliano kwa Mitandao ya Simu kuna baraka zote za Serikali

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,666
8,498
Haiingii akilini kama Serikali na mamlaka zinazosimamia hii mitandao ya simu hazijui hizi gharama za kinyonyaji za hii mitandao.

Walianza Tigo kupandisha gharama zaidi ya 100%. Sasa hivi Voda nao wamepandisha.

Serikali imebariki huu wizi ili ipate kodi kubwa kwa ajili ya hii miradi yake.
 
Unazungumzia serekali ipi??! Tokea lini serekali ambayo haina kibali cha wananchi ikashughulika na matatizo ya wananchi?Yaani serekali iingie madarakani kwa wizi wa kura kisha ishughulikie matatizo ya wananchi?Una kichaa?

Yaani serekali iliyoshindwa kuzuia bei ya mafuta ya kula ambayo ni bidhaa pendwa ya wanyonge kupanda kiholela ndiyo ikashughulikie mambo makubwa ya mitandao ya simu?Stay tuned the worst is yet to come!
 
Unazungumzia serekali ipi??! Tokea lini serekali ambayo haina kibali cha wananchi ikashughulika na matatizo ya wananchi?Yaani serekali iingie madarakani kwa wizi wa kura kisha ishughulikie matatizo ya wananchi?Una kichaa?...
Ongeza sukari, sementi, nondo. Vyote hivyo serikali imeshindwa kushughulikia ambavyo vinamtatiza mwananchi wa hali ya chini.
 
Huyu Bwana anapenda Sana kutoza Kodi kuliko kubuni uzalishaji.

Hakuna nchi ikiyowahi endelea kwa kubuni vyanzo vipya vya kupora fedha wananchi kupitia Kodi mpya kwa vyanzo vilevile.Nchi uendelea kwa kuchochea uzalishaji na sio kukazania Kodi mpya kwa watu walewale.
 
Wapandishe tu hata kwa 500%. Wizi ule mkubwa wa kura lengo lilikuwa CCM ifanye mambo yake bila bugdha.

Naona kuna watu wanataka kuleta chokochoko. Tuwe wazalendo wa kuitikia chochote kilichoridhiwa na Serikali ya CCM.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom