Nafikiri kuna haja ya kumuamsha Kikwete usingizini afanye maamuzi mazito

politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,507
Sifa ya kuwa rais bora ni kuwa pro active na siyo reactive
Rais jk ni mtu mzito sana kufanya maamuzi magumu kwa wakati na siku zote maamuzi yake yanategemea namna gani watu wengine wanafanya na ni mtu reactive badala ya kuwa pro active. Naamini ili uweze kuwa rais mzuri ni lazima uwe na uwezo wa kutumia uzoefu elimu na kipawa chako kuweza kufanya maamuzi kwa wakati kwa sababu kazi ya urais sometimes you have to make a decision in split of second kwa maana maisha ya watu yanakuwa hatarini.

Uzito wa kufanya maamuzi unaigharimu sana nchi yetu nitatumia mifano ifuatayo:
Ulipotokea mgomo wa madaktari hakuchukua hatua za haraka mpaka presha ya wananchi ilipoongozeka ndipo alipokutana na madaktari hao wakati watanzania wengi walishapoteza maisha yao un necessarily mpk leo sielewi kwanini alichelewa vile??

Mgomo wa wafanyakazi the same thing watu wengi walipata hasara mpk shinikizo la watu kutaka hakutane na wafanyakazi hao ndio likaja kumaliza au kupunguza makali.

Suala la mgogoro wa katiba zanzibar ya mwaka 2010, leo hii nchi ipo kwenye mgongano wa katiba na zanzibar kwa sababu ya jk kwa sababu ya kuamua kwa makusudi kabisa to put his head in the sand. kwanini nasema hivyo nakumbuka mijadala mikali ilikuwa ikiendelea kwy TV nae akiwa anaona huko zanzibar jinsi katiba unavyovunjwa hakukemea wala kufanya ambayo hii ni his constitutional duty kuilinda katiba ya nchi.

Kwenye hili suala la ESCROW ACCOUNT ili JK afanye maamuzi mazito na BORA kuna haja ya watu kuingia barabarani ili kumuamsha usingizini mzito pale magogoni bila hivyo anaweza kuvaa miwani za mbao kujifanya hajui kinachoendelea.

Kwanini nasema kuna haja ya kumuamsha Rais usingizini?

hivi sasa nchi nzima iko kwenye tension kubwa kuangalia ni hatua gani zitachukuliwa juu ya kodi za wananchi zilizoibiwa na maofisa wake ambao wengi ni marafiki zake sasa kitendo chake cha kukaa kinaigharimu nchi kwani nchi iko kwenye tension kubwa na hasa kutojulikana hatima ya hawa wausika wa escrow kunaleta kiwingu kikubwa ambacho hakina sababu kwani yeye anazo taarifa za kutosha kuweza kufanya haitendei haki nchi kwa kukaa na bila kulimaliza kwahiyo naamini kuna haja ya kufanya maandamano makubwa kumuamsha usingizini.

Double standard ktk kufanya maamuzi(selective outrage)
wafanyakazi waliandamana kudai maslahi zaidi jk aliiita wazee wa jiji na kuonyesha na kutoa lugha kali za vitisho kwa wafanyakazi wakati madai yao ni ukweli na halali, leo hii mabilioni ya watanzania yameibiwa mchana kweupe amejifungia ikulu na wala ule ukali haupo hata wazee wa jiji hataki hata kuwaona kwani issue inawahusu marafiki zake wa karibu. mtakaodai dai anaitaji muda zaidi bunge lilipokea ripoti baada ya muda mfupi likafanya maamuzi, yeye urais ni taasisi kubwa alipata ripoti kabla ya kwenda kutibiwa USA hakusema kitu amerudi ameikalia ripoti ikulu hakuna maamuzi mnawezaje kusingizia muda au anajaribu kupima mood ya watanzania ili awalinde marafiki zake??
 
shikamoo mh jakaya mrisho kikwete,awali ya yote pole na hali ya afya namatumaini MUNGU atakusaidia
mh raisi najua upo humu na unapita mara kwa mara,... nikikukmbuka 2005 nikiwa sekondari ulihaidi utatengeneza ajira zaidi ya millioni moja, lakini mpaka sasa unakaribia kumalizia awamu yako mh raisi swala la ajira ni tatizo kuu, wasomi wanaishia kua mtaani,vijana wengi wenye ujuzi wapo mitaano

Hili hali leo mabilioni ya ela yanapotea ,wawekezaji wanakwepa kulipa kodi iyo ela pia ingeweza kuzungushwa ikatumika katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bomu la ajira alilowai kusema ata edward lowassa leo wasomi tupo mitaani atuna la kufanya ,tunalipa kodi mh raisi ,uwizi huu unakosea ,iptl wanalipwa lakini ndani ya izo pesa zinalipwa zikiwa na vat component ndani yake,waziri mkuu yote aya alikua anayajua sie vijana tunaumia,waziri mkuu huyuhuyu yote aya anayajua kwamba leo maelfu ya vijana tupo mtaani kuna nafasi za kazi baadhi ya taassi za serikali ,watu wana udugu utumishi wanawaagiza waende kwenye vituo vya kazi pasipo kutangaza ,interview zinakua ushahidi pia watu wanachanganya.,,...
mh raisi mimi ni mwana ccm ila ntatafakari uanachama wangu kama hautawawajibisha viongozi wazembe hawa walioshindwa kuokoa kodi zetu,kama viajana hatuna ajira mwanasheria mkuu anasema hakukua nakod ya serikalii,vijana hatuna ajira waziri muhongo anasema hakuna ela ya serikali
 
Yote uliyoyasema ni kweli kuwa Rias anachelewa kuchukua maamuzi, lakini je pale anapochukua maamuzi anatatua tatizo? nadahani jibu ni ndiyo mafano alitatua mgogoro wa madaktari na wafanyakazi wengine. Mimi nadahani kutokuwa na papara kwa rais ni vizuri ila kufanya maamuzi sahihi kuliko kukurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.
 
  • Thanks
Reactions: gsu
Hatutamwonea mtu wala kumpendelea mtu - CCM.

Nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sharia; sio kamatakamata au fukuzafukuza ovyo; nchi itatikisika wengine wana hela nyingi wakienda mahakamani wanaweka mawakili wazuri; watashinda kesi.
 
Urais ni taasisi kubwa sana pengine siyo kila jambo ukilipata leo kesho unaliamua hapana ukifanya hivyo utaumiza watu wengi sana kwahiyo kila anachoambiwa Rais lazima akifanyie kazi kwakuchanganya na zake ndipo afike uamuzi.
 
kwa mujibu wa kichwa cha mada yako, maazimio aliyopelekewa mezani mheshimiwa rais hata akiyatekeleza kwa pupa unavyofikria hayawezi kurudisha pesa hizo zinazodaiwa kuibiwa. Yeye ametakiwa tu kuwawajibisha watendaji wake, suala kurudisha ama kutorudisha pesa ni la kisheria zaidi.
 
[h=2]Raisi wangu jk amua haraka swala hili la uwizi wa escrow huku mamilioni ya vijana hatuna ajira[/h]
shikamoo mh jakaya mrisho kikwete,awali ya yote pole na hali ya afya namatumaini MUNGU atakusaidia
mh raisi najua upo humu na unapita mara kwa mara,... nikikukmbuka 2005 nikiwa sekondari ulihaidi utatengeneza ajira zaidi ya millioni moja, lakini mpaka sasa unakaribia kumalizia awamu yako mh raisi swala la ajira ni tatizo kuu, wasomi wanaishia kua mtaani,vijana wengi wenye ujuzi wapo mitaano

Hili hali leo mabilioni ya ela yanapotea ,wawekezaji wanakwepa kulipa kodi iyo ela pia ingeweza kuzungushwa ikatumika katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bomu la ajira alilowai kusema ata edward lowassa leo wasomi tupo mitaani atuna la kufanya ,tunalipa kodi mh raisi ,uwizi huu unakosea ,iptl wanalipwa lakini ndani ya izo pesa zinalipwa zikiwa na vat component ndani yake,waziri mkuu yote aya alikua anayajua sie vijana tunaumia,waziri mkuu huyuhuyu yote aya anayajua kwamba leo maelfu ya vijana tupo mtaani kuna nafasi za kazi baadhi ya taassi za serikali ,watu wana udugu utumishi wanawaagiza waende kwenye vituo vya kazi pasipo kutangaza ,interview zinakua ushahidi pia watu wanachanganya.,,...
mh raisi mimi ni mwana ccm ila ntatafakari uanachama wangu kama hautawawajibisha viongozi wazembe hawa walioshindwa kuokoa kodi zetu,kama viajana hatuna ajira mwanasheria mkuu anasema hakukua nakod ya serikalii,vijana hatuna ajira waziri muhongo anasema hakuna ela ya serikali
 
Yote uliyoyasema ni kweli kuwa Rias anachelewa kuchukua maamuzi, lakini je pale anapochukua maamuzi anatatua tatizo? nadahani jibu ni ndiyo mafano alitatua mgogoro wa madaktari na wafanyakazi wengine. Mimi nadahani kutokuwa na papara kwa rais ni vizuri ila kufanya maamuzi sahihi kuliko kukurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Hii ndiyo mantiki ya utawala bora lazima maamuzi yafanyike kukiwa hakuna mashaka yoyote juu ya jambo lolote ambalo lipo mezani kwa Rais hapo utakuwa unatenda haki kwa yeyote.
 
Kufanya maamuzi siyo lazima ushinikizwe mwacheni apime ataamua kwa wakati baada ya kuwa amebaini paso shaka kwamba kunamakosa yalifanyika siyo kwa mashinikizo.
 
Watu wanashangaza sana humu mitandaoni, yaani rais amuogope REGINALD MENGI? upuuzi gani huu jamani.
 
yote uliyoyasema ni kweli kuwa rias anachelewa kuchukua maamuzi, lakini je pale anapochukua maamuzi anatatua tatizo? Nadahani jibu ni ndiyo mafano alitatua mgogoro wa madaktari na wafanyakazi wengine. Mimi nadahani kutokuwa na papara kwa rais ni vizuri ila kufanya maamuzi sahihi kuliko kukurupuka na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

mbona hueleweki?
 
Urais ni taasisi kubwa sana pengine siyo kila jambo ukilipata leo kesho unaliamua hapana ukifanya hivyo utaumiza watu wengi sana kwahiyo kila anachoambiwa Rais lazima akifanyie kazi kwakuchanganya na zake ndipo afike uamuzi.

hawa wanasahau kuwa pamoja na kwamba PAC walitafuniwa kila kitu na CAG na PCCB lakini bado iliwachukua muda mrefu sana kusoma ripoti yao bungeni, sasa iweje taasisi ya Rais yenyewe iletewe ripoti leo, kesho itoe maamuzi? hapa ndipo napata mashaka kuwa maazimio kutoka Bungeni kwenda kwa rais yana msukumo usiyo wakawaida kutoka nje, hii ni hatari sana na Rais lazima awe makini sana.
 
Nimegundua Jk ni rais ambaye hakika Watz hatutomsahau na hatupaswi kumsahau,ametoa uhuru hata wa kumtukana akakaa kimya,wa kumshinikiza na bado akawa calm,wa kujaribu kuichezea na kuijaribu serikali yake na bado akakuvumilia.Neno moja kwenu nyie vibaraka wa wasaka U-rais,wafanyabiashara madalali na wengine wenye kariba ya kutotaka kuona mwenzio anaweka historia ya kuitumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa,wakati Rais Kikwete anaingia madarakan ni asilimia 6 wa wananchi wote walokuwa wanapata umeme,leo hii Watz asilimia 35 wanaaccess na umeme hasa vijijini,barabara za rami ameongeza kwa asilimia 25 network ya barabara za rami,huduma za afya karibu kila kijiji kina zahanati na kila kata kuna kituo cha afya,na mengine mengi,juzi mmepata kuskia tunafanya vizuri katika kupambana na rushwa.Ila siwalaumu sana ila ndo tulivyo na itabaki kama challenge kwa rais ajaye,ila kwa ufupi serikali hii imejitahidi sana tena sana bt one word kwenu vibaraka,mipango yenu na mabeberu wa magharibi inajulikana na mtashindwa
 
Wewe ndio msema ukweli really great thinker unatumia elimu yako kuona ukweli well done!huna element za ulaza credibility yako kubwa sana..You are very knowledgeable mkuu
 
hawa wanasahau kuwa pamoja na kwamba PAC walitafuniwa kila kitu na CAG na PCCB lakini bado iliwachukua muda mrefu sana kusoma ripoti yao bungeni, sasa iweje taasisi ya Rais yenyewe iletewe ripoti leo, kesho itoe maamuzi? hapa ndipo napata mashaka kuwa maazimio kutoka Bungeni kwenda kwa rais yana msukumo usiyo wakawaida kutoka nje, hii ni hatari sana na Rais lazima awe makini sana.

Actively engaged in politics mkuu unatendea haki elimu yako sio hao wahuni vilaza unataka Rais atoe maamuzi eti kwafaida ya mchanga
 
[h=2]Raisi wangu jk amua haraka swala hili la uwizi wa escrow huku mamilioni ya vijana hatuna ajira[/h]
shikamoo mh jakaya mrisho kikwete,awali ya yote pole na hali ya afya namatumaini MUNGU atakusaidia
mh raisi najua upo humu na unapita mara kwa mara,... nikikukmbuka 2005 nikiwa sekondari ulihaidi utatengeneza ajira zaidi ya millioni moja, lakini mpaka sasa unakaribia kumalizia awamu yako mh raisi swala la ajira ni tatizo kuu, wasomi wanaishia kua mtaani,vijana wengi wenye ujuzi wapo mitaano

Hili hali leo mabilioni ya ela yanapotea ,wawekezaji wanakwepa kulipa kodi iyo ela pia ingeweza kuzungushwa ikatumika katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na bomu la ajira alilowai kusema ata edward lowassa leo wasomi tupo mitaani atuna la kufanya ,tunalipa kodi mh raisi ,uwizi huu unakosea ,iptl wanalipwa lakini ndani ya izo pesa zinalipwa zikiwa na vat component ndani yake,waziri mkuu yote aya alikua anayajua sie vijana tunaumia,waziri mkuu huyuhuyu yote aya anayajua kwamba leo maelfu ya vijana tupo mtaani kuna nafasi za kazi baadhi ya taassi za serikali ,watu wana udugu utumishi wanawaagiza waende kwenye vituo vya kazi pasipo kutangaza ,interview zinakua ushahidi pia watu wanachanganya.,,...
mh raisi mimi ni mwana ccm ila ntatafakari uanachama wangu kama hautawawajibisha viongozi wazembe hawa walioshindwa kuokoa kodi zetu,kama viajana hatuna ajira mwanasheria mkuu anasema hakukua nakod ya serikalii,vijana hatuna ajira waziri muhongo anasema hakuna ela ya serikali

Elimu gani hiyo advance diploma?
 
Ona huyu elimu yake ndogo!

Elimu ya ndogo lkn udogo wa elimu yangu haujaninyima upeo wa kuona udhaifu wa viongozi wetu mfano Jk,elimu yangu ndogo haijanifanya nitetee wezi wabadhirifu wa mali za umma,elimu yangu ndogo haijanifanya kujua nchi inaendeshwa kwa mikopo na misaada toka nnje,bora elimu yangu ndogo inayotetea watz walio wengi kuliko elimu yako kubwa inayotetea wabadhirifu wachache wanaongamiza taifa letu
 
Nakubaliana na wewe 100% tezi dume aamshwe usingizini
Haingilii akilini kwa Rais kuingilia pesa za umeme tuliopewa na PAP tukamdhulumu pesa zake
fuatilia vizuri hili sakata sio kumfunga kila mtu kwa matakwa ya mtu mmoja
JK alishajilaumu kusimamisha watu hovyo kwa ajili ya majungu
Wabunge haa bado miezi 6
AG Werema kamaliza muda wake
Muhongo si wa kupigiwa kura ni baada ya JK kuondoka Disemba 2015 atakaso moja kwa moja hicho Cheo
Tusubiri Mahakama hapo 08 Disemba 2014 Sakata Taarifa ya CAG km kweli ni pesa za UMMA ndipo mumshuritishe Rais wetu kuwa kalala.
LA SIVYO MUDA WAO SI MBALI SAKATA ZIMA HALITAMALIZA MWAKA KM WATABAKI NI MAAMUZI YA RAIS MAANA HAKUJA JINSI YA KUMLAZIMISHA RAIS By Simbachawene
 
Back
Top Bottom