Nafikiri kiingereza kingekuwa ni somo la kawaida kutoka shule ya Msingi mpaka Chuo kikuu

Naona tuige Kenya au Uganda, tuwe makini na kiingereza kwani ni lugha ya dunia. Tupo nyuma kielimu kwa sababu hatukutilia maanani kiingereza.
 
Sasa ajabu ni Wizara ya Elimu sijui hata kama imefanya utafiti kubaini hitaji la wananchi,maana walio na kipato na ufahamu wa mambo yanavyoenda wanapeleka watoto kwenye shule za "english medium"
Swali kwa Wizara ya Elimu:
1.Je?Wizara ya Elimu mna Kitengo cha Utafiti?
2.Je?Mmeshajaribu kufikiria namna ya kubadili mfumo wa Elimu, ili twende na mfumo wa "English medium"
3.Je?Wizara inafahamu kuwa nchi inapata changamoto toka kwa nchi jirani na Dunia kwa ujumla:
a)wahitimu wetu hata wazo la kutafuta kazi katika nchi zinazotuzunguka hawana kwa sababu ya mfumo wa elimu tulionao.
b)Sera za nchi ni kushirikiana na kufungua milango ya kiuchumi kwa mataifa mengine, lakini elimu yetu ipo nyuma katika mipango ya kuimarisha teknolojia kwa wanafunzi , kila siku tunazungumzia kujenga madarasa huku tunasahau kujenga nyumba za walimu.
c).Mfumo wa usimamizi shule na walimu umekuwa haulengi kuleta tija katika ufundishaji;Walimu wanatishiwa kila siku na viongozi wa kisiasa,kupewa majukumu ya kusimamia miradi ya ujenzi(walimu walipaswa kukabidhiwa miundombinu),Walimu kutopewa motisha.
 
Mimi nilikua nafikiri kiingereza kingekua ni somo la kawaida kutoka shule ya Msingi mpaka Chuo kikuu.

Alafu masomo mengine yote kuanzia shule ya Msingi mpaka chuo kikuu yangefundishwa kwa kiswahili.

Ila katika upande wa Kiingereza tungehakikisha kinakua ni kile kiingereza kigumu ambacho na kwenye sayansi kinatumika.

Mtoto akifaulu kwenda kidato cha sita ajifunze kiingereza kile chenye terminologies za masomo anayosomea na chuo nako iwe hivyo hivyo.

Nadhani hapo watanzania wangeweza kuelewa vizuri sana kile wanachokisomea.

Wakuu ni mawazo tu lakini maana lugha inaweza kufanya kitu kuwa rahisi.

Wanafunzi wengi wanakalili kwasababu hawaielewi lugha ya kiingereza.

Mfano mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka mzima hupotea kwakuzikalili definition na importance hakuna chochote ambacho huwa wanaelewa pale zaidi ya kukalili.

Sasa huyu mwanafunzi angeendelea kusoma bayolijia ya kidato cha kwanza kwa lugha ya kiswahili unadhani angekuwaje.


Kama kuna nyongeza karibuni.
Nakumbuka hata tukiwa secondary school kuna watu wengi walipata F za Kiswahili hawaelewi maana ya kiwakilishi, kitenzi sijui mashairi ,
 
Itachukua miaka mingi sana kwa Waafrika kutambua kwamba wakoloni walituweza.
 
Naunga mkona, maarifa mengi yako ndani kwenye lugha ya kiingereza, na ili kuyapata lazima tukijue
Pia tukitumia lugha ya kiingereza kuna Mambo mengi ya sekondari Ni marudio ya primary tofauti Ni lugha tu,
So tunaweza kuyafuta tukapungaza idadi ya vidato, tokafocus kwenye elimu yenye tika kwa vizazi vyetu
 
Nakumbuka hata tukiwa secondary school kuna watu wengi walipata F za Kiswahili hawaelewi maana ya kiwakilishi, kitenzi sijui mashairi ,
Vipi shule ya msingi ulikuwaje zile maarifa ya jamii. Umeingia secondary umeishia kushika point tu. Wakati ilitakiwa usome maelezo yote general na uyaelewe.
 
Back
Top Bottom