Nafasi za Ungozi wa Serikali kwa Furaha ya Rais

peche luke

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
365
106
Tumesikia mh waziri mtenguliwa mmoja akituelezea kuwa uteunzi wake wa kuwa waziri, mh Rais aliufanya kwa furaha yake yeye Rais. Ina maana kuna nafasi nyingine nyingi za kuteuliwa na Rais ambazo watu wapewa kwa furaha ya Rais. Mkuu wa wilaya/mkoa kwa furaha ya Rais nk, nk.

Sasa basi kwa vile tunaendelea na mchakato wa katiba mpya na jana Rais kasema wakati wa bunge la katiba wabunge waruhusiwe kufikiri nje ya rasimu (nje ya box).

Mimi nilikuwa na mapendekezo haya, kwenye kifungu cha katiba mpya kinacho zungumzia nafasi za uteuzi zinazo fanywa na Rais kiongezee huu uteuzi wa furaha ya Rais (president's pleasure appointments) Hii itamfanya Rais afanye mambo kisheria zaidi.

Pia kama ikiwezekana wananchi nao wapewe nafasi ya kumshawishi Rais au kumuomba amteue mtu anayefaa katika nafasi fulani ya kiuongozi kwa furaha yake Rais.

Na wakati wananchi wanafanya ushawishi au mapendekezo haya kwa Rais waruhusiwe wakitaka au wakipenda wafanye kwa kukemea, kama vile baadhi ya watumishi wa dini wanavyo kemea majini na pepo wachafu.

Kwa mfano waseme hivi, "kwa furaha ya Rais so n so ndg X awe waziri wa mali asili, katika president pleasure na sisitiza".


Wadau naomba tuchangie hili wazo kwa kuliboresha zaidi.

Ni watakie wote heri ya mwaka mpya 2014.
 
Alitumia maneno haya: "... is by the pleasure of the President". Pleasure!? Hilo neno alivyolitumia sikupenda asilani! Angalau angetumia "... ni kwa mamlaka yake mwenyewe ..."; lakini sio kwa "matamanio" ya Rais jamani.
 
Alitumia maneno haya: "... is by the pleasure of the President". Pleasure!? Hilo neno alivyolitumia sikupenda asilani! Angalau angetumia "... ni kwa mamlaka yake mwenyewe ..."; lakini sio kwa "matamanio" ya Rais jamani.


Kwa mchango wako huu popote kwenye neno furaha mtu akipenda aweza weka neno matamanio. ASANTE MKUU.

Nikee, "kwa furaha/matamanio ya Rais dudus awe mbunge wa bunge la katiba mpya, katika pleasure president na sisitiza" amen.
 
Back
Top Bottom