mawazoyangu
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 324
- 65
Naamini muda umefika kwa nchi yetu hii sasa kuwa na utaratibu utakaoleta tija kwa taifa. Na kwa kuanzia inatakiwa makamanda wa polisi wa mkoa (RPCs) na wilaya (OCDs) wasiwe wanapewa hizi nafasi kwa kufahamiana au kwa ushemeji kwani hili linafanya kazi zilizokusudiwa zisifanyike ipasavyo kwa kuogopa kuwa ataondolewa na aliyemweka hapo endapo atasimamia haki ambayo aliyemteua anaona haina maslahi kwake. Hizi nafasi naona zinafaa ziwe za ushindani ndani ya jeshi la polisi watu wafanye application, wahojiwe na tume ya ajira yenye wataalam kisha mwenye sifa apewe nafasi. Hii pia itumike kwa wakuu wa mikoa na wilaya kama wanastahili kuwepo japo kwa mimi binafsi naona hawastahili kuwepo kwani kwanza hakuna elimu yeyoye anayotakiwa awe nayo, mkulu anachagua tu awe mzee, kijana sawa ilimradi ulaji na ajue kulinda chama tawala kilichopo madarakani sasa.
Hii itapunguza kuona rpc na ocd anawapa askari wauaji, wezi, walioko kizuizuini wasaa wa kutembea mjini, kunywa bia mtaani ambapo wananchi wanawaona kisha baadaye kuwaambia warudi kizuizini. Ndio wataogopa kwani wanajua sio shemeji yao au mjomba ndo amewaweka hapo kwenye nafasi aliyonayo ila ni elimu, ujuzi, uadilifu na utendaji kazi