Nafasi za RPC na OCD ziwe za kuomba na kufanyiwa usahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za RPC na OCD ziwe za kuomba na kufanyiwa usahili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mawazoyangu, Oct 3, 2011.

 1. mawazoyangu

  mawazoyangu JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Naamini muda umefika kwa nchi yetu hii sasa kuwa na utaratibu utakaoleta tija kwa taifa. Na kwa kuanzia inatakiwa makamanda wa polisi wa mkoa (RPCs) na wilaya (OCDs) wasiwe wanapewa hizi nafasi kwa kufahamiana au kwa ushemeji kwani hili linafanya kazi zilizokusudiwa zisifanyike ipasavyo kwa kuogopa kuwa ataondolewa na aliyemweka hapo endapo atasimamia haki ambayo aliyemteua anaona haina maslahi kwake. Hizi nafasi naona zinafaa ziwe za ushindani ndani ya jeshi la polisi watu wafanye application, wahojiwe na tume ya ajira yenye wataalam kisha mwenye sifa apewe nafasi. Hii pia itumike kwa wakuu wa mikoa na wilaya kama wanastahili kuwepo japo kwa mimi binafsi naona hawastahili kuwepo kwani kwanza hakuna elimu yeyoye anayotakiwa awe nayo, mkulu anachagua tu awe mzee, kijana sawa ilimradi ulaji na ajue kulinda chama tawala kilichopo madarakani sasa.
  Hii itapunguza kuona rpc na ocd anawapa askari wauaji, wezi, walioko kizuizuini wasaa wa kutembea mjini, kunywa bia mtaani ambapo wananchi wanawaona kisha baadaye kuwaambia warudi kizuizini. Ndio wataogopa kwani wanajua sio shemeji yao au mjomba ndo amewaweka hapo kwenye nafasi aliyonayo ila ni elimu, ujuzi, uadilifu na utendaji kazi
   
 2. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Uko sahihi mkuu!
   
 3. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Na kisiasa nafasi za ukuu wa wilaya ZIFUTWE na Mkuu wa Mkoa achaguliwe na wananchi.........
   
 4. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  wafutwa tu wakurugenzi ndio wapatikane kwa njia hii unayopendekeza
  lakini hawa ma RC, DC waondolewe wanasababisha double standard
   
Loading...