Nafasi za mafunzo ya Ualimu ngazi ya Astashahada ya ualimu elimu ya Awali, Msingi na Stashahada ya Ualimu Elimu Sekondari mwaka wa masomo 2021/2022

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
836
1,000
KUMBUKA KUZINGATIA UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI KAMA IFUATAVYO
 1. Wahitimu wa kidato cha nne waliohitimu kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 wanaruhusiwa kutuma maombi.
 2. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu katika vyuo vya Ualimu vya Serikali wanatakiwa kujisajili na kufanya maombi kielektroniki kupitia tovuti (tcm.moe.go.tz)
 3. Waombaji wa Mafunzo ya Ualimu kwa vyuo visivyo vya Serikali watume maombi yao moja kwa moja katika vyuo wanavyotaka kusoma na vyuo husika viwasilishe sifa za waombaji Baraza la Mitihani Tanzania kwa uhakiki.
 4. Waombaji wa mafunzo ya Ualimu katika Vyuo vya Serikali watachagua tahasusi hadi tatu (03) kwa kuanza na ile anayoipenda zaidi
 5. Waombaji wa nafasi za mafunzo walio kazini wanapaswa kuwa wamehitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti, Stashahada au Shahada.
 6. Walimu Kazini watapaswa kuambatisha barua ya ruhusa kutoka kwa waajiri wao;
 7. Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na Mafunzo ya Ualimu yatatolewa kupitia “account” aliyotumia mwombaji kuomba mafunzo ya Ualimu (kuanzia 15/06/2021 ) na katika Vyuo vya Ualimu walivyochaguliwa.
 8. Barua na fomu za kujiunga na Mafunzo zitatolewa kupitia tovuti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (moe.go.tz) na Chuo atakachopangwa mwombaji kwa kutumia anuani yake. Waombaji wote wanashauriwa kuandika anuani kamili, barua pepe na namba ya simu inayopatikana kwa mawasiliano zaidi.
 9. Mwisho wa kutuma maombi kwa Mafunzo ya Ualimu ni tarehe 31/05/2021.

Tanbihi: Masomo ya Dini hayatatumika kama kigezo cha sifa ya kujiunga na Mafunzo ya Ualimu. Na kwa maelezo ya utangulizi, sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu na aina ya mafunzo na sifa basi bofya >>> Tangazo la nafasi ya kujiunga na vyuo vya ualimu ngazi Astashahada na Stashahada

Kwa mawasiliano zaidi piga 0620198019. Namba hiyo inatumika siku za kazi (Jumatatu hadi Ijumaa) muda wa kazi 1.30 asubuhi hadi 9.30 alasiri. Pia unaweza kutazama vyuo vinavyotoa mafunzo hayo na muda wake kupitia jedwali katika PDF niliambatanisha hapa.
 

Attachments

 • File size
  331.4 KB
  Views
  47

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom