Nafasi za kuteuliwa zinaondoa ufahamu na akili

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
4,121
2,000
Nikiwa nafuatilia jinsi hawa wateule wanafanya kazi nahisi wako kama watumwa. Kuna mda naona kabisa sisi ambao tuko kitaa tuna furaha na amani kuliko wao.

Kuna haja ya wateuzi kuwaambia wawe huru kwenye kazi zao. Mfano Rais anakuja kuzindua mradi uliobuniwa na kujengwa na mtangulizi wake, wateule wake wanajitutumua na kumwambia tunashukuru kwà juhudi zako

Hii huwa hainiingii akilini.

Mfano Mwingine ni pale mteuliea anaamua kudanganya umma ili amfurahishe mteuzi wake. Mfano mteule anashindwa kuwaambia mteuzi kwamba Tanzania Kuna uhaba wa madarasa, Madawati, na kwamba Maji Dar hayatoshi. Mnaishia kumsifia sifia tu hadi sisi Wana nchi tunashangaa jinsi mteule alivyopoteza uhuru wake.

Poleni wateule. Ila kwà nini huwa munakuwa hivyo?
 

JF Member

JF-Expert Member
Dec 14, 2014
4,121
2,000
basi kuwa makini maaana kuna tatizo kubwa kwa baadhi ya vijana wa kitanzania kushindwa kutofautisha matumizi ya "a" na "h", lkn pia "r" na "l"
tusiharibu lugha yetu adhimu.
Ujumbe umefika. Ila kikubwa mawasiliano na kuelewana.
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
6,414
2,000
Anayesifiwa ni yule aliyepo madarakani, basi wewe nenda kamsifie marehemu uone shughuli yake..
 

Ivan said

Member
Feb 14, 2021
82
150
Si kosa kumshukuru mama kwa sababu nia yetu ni kuona ustawi wa jamii na uchumi kumilikiwa na wengi. Tumtie mama moyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwetu sisi watanzania.

Umoja, mshikamano, kuheshimu uhuru wa habari, maoni na kujieleza, demokrasia kwa vyama siasa kwa maana ya kufanya mikutano yao bila kubughudiwa, haki kwa kila mtanzania, strong institutions and not strong personalities ni miongoni mwa nguzo muhimu za Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom