Nafasi za kugombea kuwa mtumishi wa wananchi, sio vita ya kufa na kupona

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Tanzania nchi yetu kama ilivyo kawaida kila baada ya miaka mitano, tunafanya uchaguzi mkuu wa kupata viongozi wa kututumikiakatika kipindi kingine cha miaka mitano

Sasa tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020,Kwa muda mrefu kumekuwepo na dhana potofu juu za nafasi za kugombea za kuwatumikia wananchi, kuna baadhi ya watanzania wachache wenye kuamini kupata nafasi ya kuwatumikia wananchi ni mapambano ya kufa na kupona

Kwa mtizamo wangu, nafasi za kugombea kuwa mtumishi wa wananchi, sio za kukimbilia wala kupambana na kupigana vikumbo, kuna mambo matatu(3) muhimu ya kuzingatia

Kwanza , ni mwenyezi Mungu , yeye pekee ndiye mwenye uwezo na mamlaka ya kuamua nani awe wapi na kwa wakati gani, ni sahihi kwa mtu huyo kutumikia wananchi wa eneo husika

Pili , ni wananchi wenyewe, wao kwa umuhimu walionao, wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya tathimini na kuamua nani awe mtunishi wao na kwa wakati gani

Mwisho , japokuwa sio mwisho kwa umuhimu, ni chama unachoamini kwenye itikadi zake, Chama kama taasisi wana sheria, taratibu na kanuni zinazoendesha zoezi la kuamua nani awe mtunishi wa wananchi na katika eneo gani la uwakilishi,
Chama kama taasisi wana utaratibu wa kufanya tathimini ya nani anafaa kuwa mtumishi wa wananchi kwa kuzingatia vigezo walivyojiwekea

Kwa hiyo, ukiyazingatia hayo hapo juu, nafasi za kuwa mtumishi wa wananchi sio za kukimbilia, sio za kupambana wala sio kufa na kupona
 
Kwahiyo unataka kusemaje kwani, mbona kuna mtu anaweweseka sana na urais wakati alisema alisukumizwa, sio ndio muda wake sasa wa kuondoka alikosukumizwa kwa hiari au kutolewa na waliomsukumiza.
 
Back
Top Bottom