Nafasi za kazi za Ualimu serikalini/TAMISEMI

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,410
1,383
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Anuani ya Simu “TAMISEMI” DODOMA Mji wa Serikali – Mtumba,
Simu Na: +255 26 2321607 Mtaa wa TAMISEMI,
Nukushi: +255 26 2322116 S.L.P. 1923, Barua pepe:ps@tamisemi.go.tz 41185 DODOMA.
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA YA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

A: UTANGULIZI
Ofisi ya Rais - TAMISEMI inapenda kuutangazia Umma kuwa Serikali imetoa nafasi za ajira ya Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari. Kwa sababu hiyo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI inawatangazia walimu wenye sifa kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz (Online Teacher Employment Application System - OTEAS).

Walimu wanaotakiwa kutuma maombi ni wenye sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

B. WALIMU WA SHULE ZA MSINGI
  1. Mwalimu Daraja la IIIA – mwenye Astashahada (Cheti) ya Ualimu;
  2. Mwalimu Daraja la IIIB - mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu katika somo la English na waliosomea Elimu ya Awali;
  3. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu wa masomo ya
  4. English, Civics, General Studies, History, Geography na Kiswahili; iv. Mwalimu Daraja la IIIB na IIIC – mhitimu wa Stashahada (Diploma) ya Ualimu (Elimu Maalum) wa masomo ya Lugha, Sanaa, Sayansi na Hisabati.

C. WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI
  1. Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, Physics na Mathematics;
  2. Mwalimu Daraja la IIIB – mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Physics, Mathematics, Biology, Chemistry, Home Economics na Agricultural Science;
  3. Mwalimu Daraja la IIIC – mwenye Shahada ya Ualimu waliosomea Elimu Maalum kwa masomo ya English Language, Geography, Physics na
  4. Mathematics; iv. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu wa masomo ya Physics, Mathematics, Chemistry na Biology.
  5. Mwalimu Daraja la IIIC - mwenye Shahada ya Ualimu wa masomo ya Agricultural Science, English Language, English Literature, Chinese, French, Book Keeping, Commerce, Accounts, Economics na Home
  6. Economics/Food and Human Nutrition; vi. Wahitimu wa Stashahada (Diploma) ya Ufundi na Shahada ya Uhandisi Ujenzi (Civil Engineering), Uhandisi Mitambo (Mechanical Engineering), Uhandisi Umeme (Electrical Engineering) na Electronic Engineering ambao wataajiriwa kama Walimu Daraja la IIIB na Daraja la IIIC; na
  7. Fundi Sanifu Maabara - wahitimu wa Stashahada (Diploma) ya Ufundi Sanifu Maabara na Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara.
D. SIFA ZA JUMLA ZA MWOMBAJI
Mwombaji wa nafasi zilizoainishwa hapo juu awe na sifa za jumla zifuatazo:-
  1. Awe ni Mtanzania;
  2. Awe amehitimu kati ya mwaka 2014 hadi 2019.
  3. Asiwe na umri wa zaidi ya miaka arobaini na tano (45);
  4. Walimu waliowahi kutuma maombi na hawakupata nafasi za ajira wanaweza kutuma maombi upya;
  5. Walimu waliowahi kuajiriwa Serikalini hawatakiwi kutuma maombi; na
  6. Kila mwombaji wa ajira ya Ualimu ahakikishe ana Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA.
E. MWISHO
Maombi yote ya ajira yatumwe kupitia kwenye mfumo wa maombi ya ajira wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kama ulivyooneshwa kwenye tangazo hili. Hakuna maombi yatakayopokelewa kwa njia tofauti na iliyoelekezwa. Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kuanzia tarehe 07/09/2020 hadi 21/09/2020.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
DODOMA.
7 Septemba, 2020
 
Mbona kule tume ya ajira hawana ugumu wa hivi? Hawa mizinguo tuu.
 
Huu ni utapeli mnawafanyia wadogo zetu..tangu juzi nasikia malalamiko yanayoshabihiana kuhusu ugumu Wa kuaccess seva ya TAMISEMI..halafu pia hizo na nafasi ni za kibaguzi. Sijaona wale Wa History na Kiswahili maskini ya Mungu wamekaa miaka mitatu wakimeza madesa bure!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom