Nafasi za Kazi ya Uhandisi mwisho tarehe 25/3/2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za Kazi ya Uhandisi mwisho tarehe 25/3/2012

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Yeccotltd, Feb 19, 2012.

 1. Yeccotltd

  Yeccotltd JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NEMBO YA YECCO.jpg


  Kampuni yako ya Kizalendo ya YECCO (T) LTD ishughulikayo na Building & Civil Contractor, Electrical Contractor & IT. inatangaza nafasi za kazi ya uhandisi:

  Sifa:
  A) Awe amehitimu elimu ya Building, Civil, Electrical and IT kuanzia ktk ngazi ya Advance Diploma na kuendelea,

  B) Awe amehitimu ktk chuo kinachotambuliwa kitaifa na kimataifa,

  C) Kwa Electrical awe na leseni ya EWURA.

  D) Awe na elimu ya ya utangulizi ya kompyuta.

  E) Asiwe aliwahi kuwa Technical Director ktk kampuni yoyote CRB


  Maombi ya tumwe kwa anwani ya kimtandando yeccotltd@yahoo.com , au kufika ofisi zetu zilizopo mtaa wa Samora,Posta, Dar es salaam, Tanzania, Coronation House,Ghorofa ya pili, jirani na Baraza Kiswahili.

  Bila kusahau CV yenye kopi ya vyeti vya taaluma yako, cha zaliwa na Picha mbili za pasipoti ktk maombi hayo!

  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25/5/2012​
   
 2. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu,maelezo yako hayajajitosheleza,kampuni yenu ni class gani?
  Wahandisi mnaowahitaji ni wa aina gani?Kuna Graduate registered Engineer na Proffessional Registered Engineer au Engineer based on Experience.Fafanua.
  Hapo kwenye nyekundu,wahandisi hatuna leseni za EWURA ila kuna vyeti vya usajili vya ERB.
   
 3. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nashukuru ila kwa msaada wa wengine ambao tunapenda kuwa na knowledge tofauti haswa ya classes kwa jinsi ulivyo-oanisha hapo juu ni nini? Je ERB katika professionalism inahusikaje?

  I just wanted to know Mkuu
   
 4. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu Lasikoki,
  ERB ni kifupi cha Engineers Registration Board,kwa kiswahili ni bodi ya usajili wa wahandisi hapa Tanzania.Ili mtu yeyote aweze kufanya kazi za taaluma ya uhandisi ni lazima awe amesomea na kusajiliwa na bodi tajwa hapo juu.Unapohitimu shahada ya uhandisi unatakiwa ujisajili kwenye bodi ambako utajulikana kama graduate engineer,baada ya miaka mitatu au zaidi ya ufanyaji wa kazi za fani yako unatakiwa uandike ripoti ambayo inapitiwa na wataalamu wa bodi ndipo wanaweza kukusajili kama Proffessiona Engineer.Nilipoandika Engineer based on experience nilimaanisha wale senior technicians ambao wapo kwenye fani muda mrefu na wamekua wakifanya kazi za wahandisi na wengine wamekua wakijiita Wahandisi.Ila ukweli ni kwamba ili uitwe mhandisi lazima uwe na shahada.Nadhani utakua umenielewa.
   
 5. Yeccotltd

  Yeccotltd JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kwa ushauri tumerekebisha na kuainisha vema wataalamu tunaowahitaji, tupo class 7
   
Loading...