Nafasi za kazi nchini Botswana

MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
705
Waungwana,

Je, kuna Watanzania waliopo nchini Botswana ambao wanaweza kuniunganisha nafasi za kazi huko? Je, mtu akitaka kwenda huko lakini akajiajiri mwenywe, inawezekana, au aanze kwanza kama mwajiriwa kisha ataweza kujiajiri mwenyewe kidogo kidogo?

Masharti, vigezo, sifa za kuajiriwa nchini Botswana, ni yapi?

Nitashukuru kwa msaada huu.

./Mwana wa Haki

P.S. Maisha ni popote, ili mradi mkono unaenda kinywani.
 
chungulia www.naombakazi.com kuna nafasi kibao za kazi hata hivyo bado nashangaa pamoja na uzoefu wako wote katika ICT bado unafikiria kuajiriwa tu hujaweza kuja na kitu chako ambacho unaweza kukufanyia kazi tokea nchini tanzania == ukitaka mkopo utapewa
 
mkuu kama kuajiriwa ni kazi aina gani?.wewe unaprofesional gani?
kama ni kujiajiri unataka kwenda kuanzisha biashara gani?.mtaji unazo shg ngapi?
please expain
 
Hawa jamaa kwa muda mrefu walisimamisha ajira kwa wageni isipokuwa doctors na hivi karibuni wameanza kuajiri walimu. Kama una fani za aina hiyo all the best
 
kama wewe ni civil/structure/highway engeneer pia kama ni doctor (MD) una posibility kubwa ya kupata kazi huko
 
Kazi za uhandisi, Usoroveya, Unesi, Udaktari zinapatikana sana. Ukitaka kuwa mjasiriamali inatakiwa uwe na ushahidi wa kumiliki angalau dola za kimarekani elfu 20 ili uweze kusajiriwa kama "Mwekezaji" katika fani yoyote na hapo utapewa kibali cha kuishi Botswana kwa miaka 5 kwa kuanzia.

Masharti ya kuajiriwa ni kama hapa kwetu Bongo Dar es Salaam kwani yanatofautiana kutokana na aina ya kazi, ukubwa wa kampuni, nafasi unayoomba na mshiko utakaolipwa.
 
kwani kukoje huko botswana, malipo yake yakoje, range yake ya mishahara ikoje mpaka watu wanakung'ang'ania kiasi hicho?
 
mkuu kama kuajiriwa ni kazi aina gani?.wewe unaprofesional gani?
Kama ni kujiajiri unataka kwenda kuanzisha biashara gani?.mtaji unazo shg ngapi?
Please expain

mkuu komaa popote achana na wanaokukatisha tamaa
hao wameshalipwa na mafisadi kupitia jf wakapata ,itaji wanakuenjoy
kuajairi unaatakiwa uwe na taaluma na vigezo si kuamka na kuuza chips utaishia kuwauzia wenzako maisha
 
Botswana ya sasa si kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.Pata mtu aliyeko kule akupashe habari maana yasemekana Wazimbabwe wamevamia soko la ajira na wanaajiriwa kwa malipo kidogo sana.

Fanya utafiti wa kutosha na pia waweza jaribu UK Tier 1 Visa maana wamerudisha points kwa watu wenye bachelor degree pia (30 points).
 
Fanya utafti wa kutosha kwa mtu aliyeko kule,ila alternative ni wewe kwenda na CV yako na pesa za kujikim kama dola elf 2, utafikia kwenye hotel.kaa kama wk moja, ndani ya wki hiyo sambaza CV yako kwa maofisi. kisha rudi zako bongo. wakikuitaji watakutumia detail na working permit, na other requirements,hivyo vitakusaidia kupita mipakani kirahisi. kwa mara ya kwanza ukipita sema ni business purpose, ila watakupekua sana, kwani wana discourage watu wanaoingia kwao kwa nia ya kutafuta kazi.Sina uzoefu na ICT,ila kazi za Udaktari, enginnering related fields,zinapatikana sana, ila kozi za sociology zimejaa zana pale UB ( University of Botswana), Mishahara hutegema na mji utakao kaa, ukikaa Haboroni( Gaboron) mshahara ni mkubwa kwani maisa yako juu, ila na saving ni kubwa, ukienda Francis Town, mishahar ipo chini kidogo.Generally hawapendi wageni, wana waita wakwere kwere.</p>
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom