Nafasi za kazi na fani mablimbali jeshi la polisi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nafasi za kazi na fani mablimbali jeshi la polisi...

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Mkeshahoi, Jan 7, 2011.

 1. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwa hisani na NAOMBA KAZI BLOGU....

  NAFASI ZA KAZI JESHI LA POLISI

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA


  TANGAZO LA AJIRA

  Jeshi la Polisi Tanzania linatangaza nafasi za ajira ya kazi ya Polisi kwa waombaji wenye sifa kama ifuatavyo:-

  SIFA /VIGEZO VYA JUMLA:
  (a) Muombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
  (b) Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
  (c) Awe hajaoa/kuolewa
  (d) Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
  (e) Awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani na nje ya
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  A. Kwa waombaji wenye elimu ya kidato cha nne:
  - Awe amemaliza kidato cha nne kati ya mwaka 2008 na 2010
  na kufaulu angalau kwa kiwango cha daraja la nne, Pointi 28.
  - Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.

  B. Kwa waombaji wenye elimu ya kidato cha sita:
  - Awe amemaliza Kidato cha sita kati ya
  mwaka 2008 na 2009 na kufaulu.
  - Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.

  Waombaji wa kundi A na B wenye sifa zilizoainishwa hapo
  juu wanatakiwa kupeleka maombi yao kwa njia ya barua
  kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) katika Wilaya wanazoishi.

  C.Kwa waombaji wenye ujuzi/utaalamu.

  (1) Mafundi Pikipiki (nafasi 23).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:-
  (a) Elimu ya Kidato cha IV/VI pamoja na Cheti cha Trade
  Test grade I - III kilichotolewa na VETA au na chuo
  kingine kinachotambuliwa na VETA.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Waombaji wawe wamefanya kazi kwa vitendo walau
  kwa muda usiopungua mwaka mmoja.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Kikosi cha Matengenezo ya Magari,
  S.L.P. 9141,
  DARES SALAAM.

  (2) Wataalamu wa Afya:

  (a)(i) Maafisa Tabibu (nafasi 10).
  (ii) Tabibu meno – Dent Therapists' (nafasi 2).
  (iii) Mtaalamu wa dawa ya usingizi Anaesthesia (nafasi 1).
  (iv) Maafisa Uuguzi – (nafasi 4).
  (v) Wafamasia wasaidizi – (nafasi 5).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:-
  (a) Elimu ya Stashahada katika fani hizo.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.

  (b) (i) Fundi Sanifu maabara – Lab Tech. (nafasi 5)
  (ii) Wauguzi – Enrolled Nurses (nafasi 2)
  (iii) Wauguzi Wasaidizi/Wahudumu wa Afya (nafasi 8)

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV pamoja na Vyeti katika fani
  hizo na uzoefu katika huduma za Hospitali.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Afya,
  S.L.P 9791,
  DAR ES SALAAM.

  (3) Wataalam wa muziki (Brass Band/Jazz Band) (nafasi 28).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:-
  (a) Elimu ya Kidato cha IV/VI
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Vyeti vya kufaulu katika fani ya muziki vilivyotolewa na vyuo
  vya sanaa vinavyotambuliwa na Baraza la Sanaa laTaifa (BASATA)

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Bendi,
  S.L.P.63194,
  DAR ES SALAAM.

  (4) Mafundi Ushonaji:- (nafasi 27)

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu, waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya kidato cha IV pamoja na cheti cha ujuzi katika fani hiyo kutoka VETA au Vyuo vinavyotambuliwa na VETA.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.
  (c) Uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika fani hiyo.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Kikosi,
  Ghala Kuu la Polisi
  S.L.P 2228,
  DAR ES SALAAM.
  (5) Wanamaji:
  (i) Manahodha (nafasi 5).
  (ii) Mafundi Meli (nafasi 5).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya kidato cha IV/VI
  (b) Stashahada ya fani hizo kutoka Chuo cha Wanamaji (DMI).
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  (iii) Wazamiaji: (nafasi 10)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV.
  (b) Uzoefu katika fani hiyo.
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  (iv) Mafundi Rangi za Meli (nafasi 10)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a) Elimu ya Kidato cha IV.
  (b) Cheti kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na VETA.
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Mkuu wa Polisi,
  Kikosi cha Wanamaji,
  S.L.P, 3010,
  DAR ES SALAAM.

  (6) Wataalam wa masuala ya Jamii (Social Workers- nafasi 150).
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:
  (a).Elimu ya Kidato cha IV na kuendelea.
  (b).Stashahada/Vyeti kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa
  na Serikali katika fani za:
  - Maendeleo ya Jamii (Community Development)
  -Kazi za Jamii (Social works)
  -Sayansi ya Jamii (Social Science/Sociology).
  (c) Umri usiozidi miaka 25.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Inspekta Jenerali wa Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi,
  S.L.P 9141,
  DAR ES SALAAM.

  (7) Waombaji Wenye Elimu ya Vyuo Vikuu/Vyuo vya elimu ya juu katika fani za:-
  (i) Sosholojia (nafasi 20).
  (ii) Menejimenti ya raslimali watu (nafasi 20)
  (iii) Sheria (nafasi 15)
  (iv)Washauri nasihi (Counsellors) (nafasi 25)
  (v)Utawala katika utumishi wa Umma (Public Admin). (nafasi 20)
  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji
  wawe na:-
  (a) Shahada/Stashahada ya juu katika fani hizo.
  (b) Umri usiozidi miaka 27.

  Waombaji watume maombi yao kwa:
  Inspekta Jenerali wa Polisi,
  Makao Makuu ya Polisi,
  S.L.P 9141
  DAR ES SALAAM.

  NB:Jinsi ya Kuomba:
  (1) Kila mwombaji anatakiwa aandike barua na kuambatanisha vivuli vya vyeti vyake vya kuhitimu shule (Leaving Certificates) vyeti vya kufaulu (Academic Certificates), cheti cha kuzaliwa
  (Birth Certificate), na picha tatu za passport size za rangi.
  Hati ya kiapo (affidavit) haitakubaliwa.
  (2) Kila mwombaji anatakiwa awe na wadhamini wawili wanaomfahamu vyema na awaorodheshe majina yao, anuani na mahusiano yao na mwombaji.
  (3)Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 27 Desemba, 2010 kwa anuani zilizoorodheshwa hapo juu.

  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15 Februari, 2011.


  (N.I. MASHAYO – DCP)
  Kny: INSPEKTA JENERALI WA POLISI
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,000
  Trophy Points: 280
  Sitaki kazi iliyo laaniwa hata kwenye vitabu vitakatifu.
  Mungu alinipa mikono, miguu na akili safi inayoniwezesha kujiajiri.
   
 3. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kufanya kazi ya upolisi ni sawa na kuolewa.Kwa mujibu wa dini yangu ya kikristo mwanaume kama mimi kuolewa na mwanaume mwenzangu ni dhambi ya kumkufuru roho mtakatifu.Pili sijakata tamaa ya maisha kiasi icho.na tatu kama bujibuji alivyosema na naongezea,ni afadhali mwanaume muuza maandazi kuliko polisi wa Tanzania mana muuza maandazi yuko makini na anajua faida na hasara tofauti na polisi ye hasara kwake hakuna wala cha faida.Maisha ya kukopa kopa kwenye vijiduka mitaani eti mpaka tarehe 24 au tano ni maisha ya kitumwa.Nawajua kiundani sana hawa watu na ndo maana na uhakika na ninayoyasema.
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  duuu, chuki hii si bure. Nchi hii siku moja yaweza kuwa Liberia ya Sam Doe to C Taylor. Bora polisi wahame uraiani wanaweza kuwa massacred wote at a go.
   
 5. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  asusa wenzio wala, acha ambao wanamitazamo mipya wakalete mabadiliko huko manake ukabila na undugu ulishaharibu sana tu huko, wala rushwa wasikanyage.
   
 6. WA MAMNDENII

  WA MAMNDENII JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Jun 5, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  nyie mnaoponda kazi ya upolisi nawaona kama akili zenu zimekengeuka kwa kiasi fulani kwani umuhimu wa polisi mnaujua pamoja na matatizo kadhaa ya kiuendeshaji wa jeshi hilo, NAOMBA NYIE MNOKASHIFU KAZI YA JESHI LA POLISI MNIJIBU HILI SWALI, SIKU UMERUDI TOKA KWENYE MISHUGHULIKO YAKO UKAFIKA HOME NA HAMAD NYUMBA IMEVUJWA VITU VYOTE NDANI KWAKO VIMEIBWA VYOTE, NA KATIKA UCHUNGUZI WAKO WA AWALI UKAWAHISI WALIOKUIBIA, JE HATUA YA KWANZA UTAENDA KUTOA TAARIFA KANISANI, MSIKITINI , KWA BOSI WAKO, KWA MJOMBA, KWA SHEMEJIYO, WAKILI WAKO, HOSPITALI, FUNDI UMEME AU UTAKAA KIMYA UVUMILIE?
   
 7. H

  Hute JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,044
  Likes Received: 3,912
  Trophy Points: 280
  polisi hawajalaaniwa, wala kazi yao haijalaaniwa, ila waliambiwa ya kuwa, WARIDHIKE NA MISHAHARA YAO, NA WASICHUKUE RUSHWA. kazi zote duniani ni mbaya, kama mtu ana ubaya moyoni...
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Nimeipenda hiyo Avatar yako UMOSOFIA IN LONDON
   
 9. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #9
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,030
  Likes Received: 298
  Trophy Points: 180
  2) Wataalamu wa Afya:

  (a)(i) Maafisa Tabibu (nafasi 10).
  (ii) Tabibu meno – Dent Therapists' (nafasi 2).
  (iii) Mtaalamu wa dawa ya usingizi Anaesthesia (nafasi 1).
  (iv) Maafisa Uuguzi – (nafasi 4).
  (v) Wafamasia wasaidizi – (nafasi 5).

  Pamoja na sifa za jumla zilizoainishwa hapo juu waombaji wawe na:-
  (a) Elimu ya Stashahada katika fani hizo.
  (b) Umri usiozidi miaka 25.

  Hapo kwenye nyekundu hapajatulia kwa mfumo wetu wa elimu kufikia level ya stashahada below 25 years ni tabu, kidogo kwa sasa watu wameanza kumaliza wadogo, vinginevyo wanataka watu wakafoji vyeti vya kuzaliwa

   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  wewe ukiwa polisi, how long can you survive na mshahara wa kipolisi if you have a wife and only one child and you live in dar es salaam.

  Kwa tz bila rushwa kazi ya upolisi haiendi.
   
 11. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #11
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  ainisheni na malipo ya kila fani!
   
 12. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ntaisaka ATM card na kufanya shopping upya!ya nini nkaende kurudisha vitt used? Nakutania mkuu,kazi ni kazi tu!
   
 13. m

  mbeshere Member

  #13
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfarisayo niko pamona na wewe hiyo itakuwa copy paste haiwezekani mtabibu mahiri ukawa na umri usiozidi 25yrs''' labda wanganga wa kienyeji
   
Loading...