vvm
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 6,303
- 10,334
UPDATE: INTAKE MPYA 2024 INAENDELEA MWISHO NI TAREHE 10 JANUARY 2024.
Mabadiliko ya Vigezo vya elimu isomeke;
“Elimu ya darasa la saba na kuendelea mpaka chuokikuu. Kwa mwombaji wa darasa la saba ni lazimaawe amepitia mafunzo ya JKT kwa kujitolea au Mafunzo ya Mgambo”
Kampuni ya ulinzi ya GardaWorld Security. Yenye ofisi yake Capripoint mbele kidogo na Kamanga Fery Mwanza na ofisi kuu Mikocheni B Dar es Salaam, Inatangaza nafasi ya kazi Ya ulinzi.
VIGEZO
- Elimu: Kidato cha nne na kuendelea.
- Uwezo wa kusoma, kuandika na kuongea kiingereza.
- Umri wa miaka 23 - 42
- Urefu futi 5.7 na kuendelea (kwa wanaume)
- Afya njema
- Asiwe na makosa yeoyote ya jinai
- Awe tayari Kazi Mkoa wowote wa Tanzania.
- Mwombaji Afike na barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa mkono na mwombaji kwa kiingereza
- Nakala za vyeti na vyeti halisi, cheti cha kuzaliwa au hati ya kiapo.
- Barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
- Barua za wadhamini wawili (zipiigwe muhuri kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa juu ya picha na Wasiwe walinzi au wanafunzi).
- Mdhamini awe na kitambulisho halali.
- Mwombaji awe na picha 5 za pasipoti zilizopigwa hivi karibuni
- Mwombaji awe tayari kwa mahojiano na usaili.
Usaili utafanyika , Ofisini kwetu Capripoint Mwanza kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja jioni.
Epuka matapeli, Hakuna rushwa ni vigezo tu vinazingatiwa.
Last edited: